Nimepokonywa simu yangu na polisi

kisanzala

JF-Expert Member
Aug 3, 2014
439
252
Habari zenu wanajamii,

Jana katika harakati zangu za utafutaji nimepatwa na mkasa ambao nimeona niulete humu huenda nikapata msaada ni wapi nianzie niweze pata simu yangu, niliwa mjini mida ya mchana nimebeba CPU ambayo nilipatiwa na jamaa yangu ili nimlekebishie nikiwa njiani wakatokea watu wawili wakajitambulisha kwamba wao mapolisi wakaniambia CPU niliyobeba niyawizi na imeibiwa na vitu vingi sana basi wakanipeleka kituo kidogo.

Tulipofika nikaingia ndani na mmoja wao akanimbia nitoe vitu nilivyokuwa navyo nilipotoa simu yangu akastuka na kuanza kuoji nimetoa wapi simu kama ile nikamjibu nimepewa na rafiki yangu akaichukuwa akakaa nayo nikawapa namba ya simu ili wampigie aliyenipa ile CPU.

Yule jamaa akaja akajielezea kuwa ile niyakwake na si ya wizi wakamuelewa wakamgea.Utata ukabaki kwenye simu yangu yule polisi akagoma kuitoa akanigea line tu akasema nitaipata simu nitakapomletea risit ya simu.

Utata nikwamba ile simu haina risiti kwakuwa niliipata kwenye begi la mtumba ambayo alikuwa anauza rafiki yangu ilikuwa betri lake bovu na madukani hakuna akaamua anigee mimi niiangaikie nikafaniwa kutengenezesha betri la kufoji ikakakuba najua hata ningekuwa na risiti asingeikubali kwakuwa yule jamaa aliipenda tu ile simu, sasa ili niweze kuipata nitumie vgezo gani?
 
Ungekuwa unajua karate ingekusaidia sana. nafanya kumvizia tu siku moja.........hunha hunha ka ka hunha halafu unasepa. Hatarudia tena
 
Nakubaliana na wewe. Hata mimi sina risiti ya simu hii. Nenda kwa mkuu wa kituo na waanze kukuthibitishia kuwa simu ni ya wizi. Na alieibiwa aje kituoni muanze kuangalia serial # za simu nk. Huu ni uonevu.
Nenda kwa mkuu wa kituo umwelezee hiyo issue utarudishiwa
 
Huo ni uonevu wa waziwazi ktk jeshi la polisi! Anza na mkuu wa kituo kama hujapata msaada unapanda ngazi za juu then utatumia media na hata wanasiasa au viongozi wa serikali
 
Ok,ukifika kituoni eleza nataka kumuona mkuu wa kituo,utaelekezwa mpwa hapo ndio uta muelezea mwanzo mpaka mwisho
 
Vijana wengi wa mtaani wanaporwa vitu vyao kwa jinsi hii hasa viatu, nguo, vidani, saa, culture na hizo simu
 
Ocs ndio nani na anapatikana wapi..eleza kwa urefu kidogo mkuu sio wote tunaojua ivo vyeo.. asante
Muwage mnajisomea na nyie Mara kwa Mara, mambo ya kushinda kwenye facebook, whatsapp, sijui nstgram na nini vile haijengi uelewa hata wa mambo madogo madogo tu! Sasa elimu mpaka chuo kikuu bado hujui OCS ni nani? Huyo ni Mkuu wa kituo ni kifupi cha Officer Commanding Station, mwingine anaitwa OC-CID (Officer Commanding CID), OCD (Officer Commanding District). Hivi vitakusaidia siku nyingine!
 
Unaitwa nani vile? Kisanzala? Mgogo? Wewe umeibiwa! Ilijuaje kwamba wale ni Polisi na siyo matapeli? Watakuwa waliiona sura ya kigogo wakaambiana hapa hapa! Kukabidhi vitu vyako Polisi huwa kuna daftari la kuandikisha na wewe unasaini na unaandikiwa na kengine unaondoka na nakala! Sasa kijana wangu wa kigogo ukilikuta jamaa limetinga maguo ya Polisi utalitambua kweli?
 
Ni kituo gani cha polisi?. Nenda kwa mkuu wa kituo ukamueleze suala lako kama ulivyoshauriwa. Usipo pata msaada kama ni jirani ya kituo cha wilaya nenda kwa ocd au oc cid. Usipopata msaada ni PM.
Ninaimani jeshi la polisi, halikuwafundisha askari wake kufanya vitendo vyovyote vile vya uonevu kwa raia, hiyo ni tabia mbaya ya huyo askari.
 
Muwage mnajisomea na nyie Mara kwa Mara, mambo ya kushinda kwenye facebook, whatsapp, sijui nstgram na nini vile haijengi uelewa hata wa mambo madogo madogo tu! Sasa elimu mpaka chuo kikuu bado hujui OCS ni nani? Huyo ni Mkuu wa kituo ni kifupi cha Officer Commanding Station, mwingine anaitwa OC-CID (Officer Commanding CID), OCD (Officer Commanding District). Hivi vitakusaidia siku nyingine!
Tunashukuru mungu wewe umesoma..mungu akubariki sana. Na wanaosoma wanakuwa sio wachoyo kuwapa wenzao elimu kama wewe vile. Sawa mkuu nitajitahidi kusoma na kujua vyeo vyote vya jeshi la polisi.
 
Halafu huwa wanaangalia sura za kusumbua. Polisi akikustopisha ukawa calm tu ukamsalimia na kumtolea macho, anasema nenda. Haulizii hata leseni. Aisee siwapendi polisi manake huwa waonevu mno!
Hiyo sentensi yako ya kwanza kabisa ndio iliyomgharimu jamaa.
Nisingewaelewa, kirahisi rahisi tu ni rudi nyumbani bila ya simu!!, eti mpaka waone risiti!!
Kuna watu kweli wapo Duniani hapa kwa ajili ya kuonewa tu.
 
Usipopata msaada ni PM.
Ninaimani jeshi la polisi, halikuwafundisha askari wake kufanya vitendo vyovyote vile vya uonevu kwa raia, hiyo ni tabia mbaya ya huyo askari.
hiki kipengele na hiyo ID yako navuta picha nini kinafuata

Jigo
 
Last edited:
Back
Top Bottom