Nimepokewa na kilio cha wife

Nimepokewa na kilio cha wife

kzba

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
1,355
Reaction score
790
Habarini wana JF wenzangu.

Mwenzenu yamenikuta leo, ile narudi home toka job nimepokewa na kilio kutoka kwa mke wangu kuuliza kulikoni mama ananijibu amechoka na maisha ya kukaa nyumbani, labda nieleze kwa kifupi ni kwamba mke wangu ni graduate ana degree ya leasure and hospitality toka makerere.

Kama miaka miwili iliyopita alipata kazi kwenye moja ya taasisi za kibenki hapa nchini wakati huo tulikuwa tunaishi Arusha, sasa kwa bahati nzuri mimi nilipata kazi nyingine ikabidi nihamie Dar yeye kwa upande wake alikataliwa uhamisho wa kuja huku Dar.

Ili kuiokoa ndoa yake ikabidi afanye maamuzi magumu ya kuacha kazi kwa kutegemea tukishahamia hapa Dar tutatafuta kazi nyingine tangia kipindi hiko hatujabahatika kupata kazi na juhudi zote tumezifanya ila bado hatujafanikiwa, na nilishatumaga uzi hapa atakaenisadia kumpatia mke wangu kazi nitampa asante ya milioni 1.

Nilimshahuri nimfungulie biashara akaniambia hawezi coz biashara ni wito, sasa leo ndo nimemkuta katika hali hiyo kwa kweli nimejiskia vibaya sana na hata kula hataki, naomba mnisaidie waungwana wenzangu nifanyeje kwa huyu mke wangu maanake kama juhudi zote nimetumia huu mwaka wa 3 sijafanikiwa.

Nakaribisha mawazo yenu wadau.
 
Mkeo uyo bwana mbembeleze, mfariji mlishe pia.... atatulia tu
 
Muulize mapendekezo yake ni yapi kutatua hilo tatizo.
 
Acha kazi uone kazi kupata kazi,
yeye analalama kukaa nyumbani miaka 2 tu,wakati sisi tupo kitaa mwaka wa 8 huu na wala matumaini ya kuajiriwa hayapo angalau yeye mwenzetu anaweza pata option ya biashara!
 
Kwa taalamu, tyr kazi anayo, anataka nyingine ya nini? Ama humlipi?
 
There is smthng wrong

Nakushauri mchukue hue una atend nae semin za biashara na ujasiliamali

Akakutana na peopl wanaowez change fikra ya mtu na kupenda biashara..mtafaidika wote

Ishu akiwa motivated tu
 
Amechoka kukaa nyumbani akati profession yake ni 'leisure' and 'hospitality'...

Mwambie awe creative leisure na hospitality anaweza kuvi apply hapo hapo nyumbani...

Ki vipi mdau
 
Back
Top Bottom