Nimepima Hepatitis B niko positive

Nimepima Hepatitis B niko positive

Huu ndo ushauri,usimeze kidonge ata kimoja bila kupima viral load,ili uweze kumeza ARV Lazma kuna idad ambayo virus wanatakiwa wafike,angalau 20,000

SO USIMEZE DAWA KABLA YAKUPINA VIRAL LOAD NA JITAHID UONANE NA SPECIALIST,,,,

NENDA REGENCY HOSPITAL J4 AU ALH SPECIALIST ANAKUEPO KUANZIA SA 10 JION NADHAN.

KUHUS KUPONA KUNA WATU WAMAPONA BAADA YAKUTUMIA DAWA 6 MONTH AND SO,SO ITS TRUE UNAWEZA KUPONA

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimeku pm mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vidonge vya ARV vinakuhusu kama starting dose ...kwa asiyeelewa akikuuona navyo anajua umeungua kumbe huwa vinatumika kama tiba ya HAPITATISI B

sent from toyota Allex
 
Ili kujua kama acute infection or chronic wingi wa virusi (viral load) iwe ngapi? Mwenye kufahamu please share with us.
 
Ndio sababu, ARV zinatumika ..nakama ni acute nirahisi kupona kama utafuata Mashariti kwa muda huo wote .
Naomba kujua mashariti doctor.
Kuna mtu tulienda kuchangaia damu pale bank ya taifa ya damu akautwa na Hepatitis B kapewa dawa ila jamaa nahisi hafuati mashariti.
Alizidisha pombe n.k.

Kinachoniuma mimi ndiye nilie muomba tukamtolee mtu damu, sasa naona kama ndio nilimpeleka kwenda kujua matatizo yake nikamsababishia kupagawa.
Najifariji huenda nimemsaidia kupata tiba mapema labda atapona.
 
Barbarosa, Nenda Geita..Fanya Ngono zembe au kua na contact ya mate ,chuchu na wanawake tofauti 10 ..usipoondoka na HBV shukuru..... HBV kwa sasa inatishia Geita, Kahama, Sengerema.


Kwa habari ya HBV-

Ikiwa mgonjwa yupo kwa acute stage huyu akitumia Dawa vzuri ANAPONA
Geita ni hatari, HIV nayo inashika kasi sana mitaa hiyo.
Mambo ya machimbo ya dhahabu hayo yana ambatana laana na neema.
 
unajua tunaposema Hepatitis ni maambukizi ya Ini yanasosababishwa na Virus tofauti kama vile Flavivirus, Hepadna Virus , Calicivirus , Enterovirus n.k......kwa Hepatitis B ..maana yake unamaambukiz ya Hepadna Virus ..ARVs ni anti retroviral Dawa mahususi za kuzuia HIV .. Unajua kwann umepimwa na HIV?? Ni kwasababu ni Co-infenctions yaan Ni rahisi kumkuta mwenye HIV ana HBV lkn sio lazima mwenye HBV awe na HIV.


Sasa kwann unatumia ARV za HIV?? Kwa sababu HBV yeye kama yeye hana Dawa, Ila katika kufanya utafiti ikaonekana Dawa za ARVs mahususi kwa HIV zinauwezo wa kumzuia HBV asizidi kuzaliana nahatimaye kufutiliwa mbali na kinga ya mwili.



Ndio sababu, ARV zinatumika ..nakama ni acute nirahisi kupona kama utafuata Mashariti kwa muda huo wote .
Ila kama HBV anaweza kuisha kabisa kws dawa.. kwanini HIV haishi ? Au ana genetic stricture tofauti na Virus wengine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kufuatilia uzi hapa inayohusu Hepatitis B, leo nilienda kufanya vacination, wakasema hawawezi kutoa vacination bila kupima, wakapima nikiwa naona kwa sababu aliyenipima tunazoea naye.

Baada ya kupima, ikatiki (ikareact), akabadilisha kipimo ya kampuni nyingine.

Ikatiki tena (ikareact) hapo nikaprove am Hepatitis B positive, akaniomba nakapime na HIV ili ajue jinsi ya kunikacounsel kwa kuwa sikuwa na wasi wasi kwenye HIV coz najijua na najitahidi sana kujikinga pamoja na kupima HIV mara kwa mara vipimo viwili tofauti ikaonyesha Negative (Non reactive).

Hapa nimeshauriwa nitatumia ARV kwa miezi sita alafu narudia kupima tena, wakanitia moto nitapona bila shida.

Nawauliza kuna aliyewahi kutumia ARV (TLD) kutibu Hepatitis B disease anipe mwongozo, alipoenda kupima baada ya kutumia dawa alipata majibu aina gani?

Unapona kweli? Au nikusubiri kifo mapema? Cha ajabu sijawahi kusikia tatizo lolote kubwa ya kiafya.

Naomba msaada kwa mwenye uelewa na cha kufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari,
Katika mazingira halisi hutakiwi kuanza dawa mara tu unapojulikana una homa ya ini.

Kitu kinachotakiwa ni kwenda hatua ya pili ambayo ni kujua ugonjwa kama ni wa muda mrefu (chronic) au muda mfupi (acute).

Pia vipimo hufanywa zaidi ili kutambua kama mgonjwa amefikia hatua ya kuanza dawa, ambapo vitu vitatu hupimwa:
1: Kiasi cha virus ( viral load)
2: Uwezo wa ini kufanya kazi kwa kuangalia vichocheo vinavyotolrwa na inn
3: Kuangalia maumbile ya ini kwa ultrasound
na pia huweza kufanywa biopsy (kinyama) ili kuhakiki hali ya ini.

Kwa magonjwa ya virusi kama Homa ya ini na HIV, unaweza kupona kwa kuchukua dawa mara tu inapotokea umejikuta kwenye hatari au nafasi ya kugusana na chanzo cha maambukizi na kuchukua dawa (PEP) ndani ya masaa 72 na si pale ugonjwa unapokuwa umesajiliwa mwilini tayari.

Mengine hubaki kuwa miujiza na nafasi zake.
 
Dah sawa itabidi siku nikipata nafasi niende kujikinga.
Kiukweli nilikuwa siujui huu ugonjwa ndio nimeujulia hapa.
Miaka ya nyuma nilikuwa naona tu umeandikwa kwenye makaratasi ila sikuuchukulia maanani nikajua labda ni Kama maralia tu.
Kumbe ni kitu hatari hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
...vipimo unaweza pata hata temeke hosp or mnaz mmoja ila chanjo n ocean road unaenda na kadi tu maana majibu yanawekwa n database na sindano n 3 kila moja elfu 10..binafs nlifanya vipimo tmk hosp then chanjo nkaenda direct ocean road nkakuta majibu yapo kule...ocean road kuna folen kubwa ya wanahitaj vipimo ya huo ugonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom