Habari wakuu,
Mwaka juzi baada ya kumaliza chuo na kukosa kazi ya nilichosomea, nikaanza kufanya kazi ya receptionist ktk hoteli ya wahindi. Sijawahi fanya kazi ngumu km ile kwanza hamna off kilasiku kazini afu ni night shift tu ila nilivumilia sababu ya shida zangu, hawalipi vuzuri sn mshahara ni laki mbili tu kula na nauli juu yako. nimefanya mpaka mwaka jana mwezi wa 11, nikabahatika kupata kazi nyingine ni hizi tigo shop ndogo, kwakua nilikua nimechoka na ile kazi ya wahindi nikaona niondoke, ila najuta kukurupuka kwani ningefikiri kwanza maana hii ofisi niliyoiendea ni mpya kabisa ndo imeanza na mm km mfanyakazi wa 1. Boss mpya tulikubaliana atanilipa laki 3..sasa tatizo hii tigo shop ni mpya na imefunguliwa location mbaya hamna wateja kabisa, tokea nimeanza kazi sijawahi kulipwa mshahara boss anasema mpk duka lianze kuingiza hela, Mwezi wa 11 alinipa elfu 50 na wa 12 ni hivyovyo, kilasiku natumia 3000 toka mfukoni mwangu ya nauli na chakula.
Maisha ni magumu sn nahitaji pesa nimepanga, mama yng ananitegemea..sasa nilikua nauliza ni kweli mtu akifungua biashara ni mpk ianze kumlipa ndo mfanyakazi alipwe au anatakiwa akubali kuingia hasara miezi ya mwanzo anilipe mfukoni mwake? Na la pili nilikua nafikiria kuomba kurudi kule kwa wahindi japo nilikua nachoka lkn sina jinsi maana familia inaniangalia, nimejaribu kutafuta kazi nimekosa, je kurudi kule ni uamuzi sahihi? Naombeni ushauri ndugu zangu.