Ukifuatilia kwa makini siasa za mh Edward Lowassa utaona tofauti kubwa sana kati yake na wanasiasa wengine, lowassa amekuwa mhanga wa matusi, kebehi, kashfa na siasa za maji taka.
Lakini kinachonifurahisha kuhusu huyu bwana, hakuna hata siku utamamsikia akimjibu mtu, akimtupia dongo, akimuongelea mtu. Lakini wanasiasa wengine hasa wa ccm, wamesahau kunadi sera zao na kubaki wakimjadili yeye tu na kusahau sera ya vyama vyao. Mtego huo ameingia na magufuli, amebaki akitumia muda mwingi akimuongelea lowassa!! Wakati lowassa anaongelea wakulima wasikopwe, wazee wapewe pension nk.
Nimependa siasa za Lowassa, hasa kwa sababu hamjadili mtu anajadili issues.