Nimependa siasa za Lowassa

Nimependa siasa za Lowassa

Last emperor

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2015
Posts
10,346
Reaction score
9,881
Ukifuatilia kwa makini siasa za Edward Lowassa utaona tofauti kubwa sana kati yake na wanasiasa wengine, Lowassa amekuwa mhanga wa matusi, kebehi, kashfa na siasa za maji taka.

Lakini kinachonifurahisha kuhusu huyu bwana, hakuna hata siku utamamsikia akimjibu mtu, akimtupia dongo, akimuongelea mtu. Lakini wanasiasa wengine hasa wa CCM, wamesahau kunadi sera zao na kubaki wakimjadili yeye tu na kusahau sera ya vyama vyao.

Mtego huo ameingia na Magufuli, amebaki akitumia muda mwingi akimuongelea Lowassa!! Wakati Lowassa anaongelea wakulima wasikopwe, wazee wapewe pension nk.

Nimependa siasa za Lowassa, hasa kwa sababu hamjadili mtu anajadili issues.
 
hii ndo siasa kama marekanii vile si unakuta kiongozi mkubwa anapiga vijembe badala ya kueleza wananchi anataka kufanya nini na watu walivyo wajinga wanazani hiyo ndo siasa na kuona kama lowasa anaongea muda mfupi debe tupu kumbukeni hutoa sauti kuliko lenye kitu ndani
 
Great Minds Discuss Ideas; Average Minds Discuss Events; Small Minds Discuss People. safi sana
 
Lowassa ndo aliyemuweka jk madarakani,hii ishara tosha kuwa lowassa kwenye siasa za tanzania akina magufuli watasubiri sana,tulitegemea angerusha vijembe lakini jamaa anamwaga sera hana muda wa kutajataja au kuchafua watu,
 
Ukifuatilia kwa makini siasa za mh Edward Lowassa utaona tofauti kubwa sana kati yake na wanasiasa wengine, lowassa amekuwa mhanga wa matusi, kebehi, kashfa na siasa za maji taka. Lakini kinachonifurahisha kuhusu huyu bwana, hakuna hata siku utamamsikia akimjibu mtu, akimtupia dongo, akimuongelea mtu. Lakini wanasiasa wengine hasa wa ccm, wamesahau kunadi sera zao na kubaki wakimjadili yeye tu na kusahau sera ya vyama vyao. Mtego huo ameingia na magufuli, amebaki akitumia muda mwingi akimuongelea lowassa!! Wakati lowassa anaongelea wakulima wasikopwe, wazee wapewe pension nk. Nimependa siasa za Lowassa, hasa kwa sababu hamjadili mtu anajadili issues.

Ulichoongea ni ukweli kabisa mkuu..huyu jamaa japo watu wanamtukana kila tusi jamaa hamjibu mtu wala vijembe vijembe vya kijinga.....jamaa anaweza siasa sana...
 
Lowassa ni muungwana sana. Na hicho ndicho kinachomuumiza maana siasa za nchi hii wananchi wanataka kusikia blah blah
 
Watu wanasema ukweli halafu ninyi eti mnasema vijembe.

Huyu Lowassa ni fisadi na mgonjwa sana.

Unataka ajibu nini wakati anaambiwa ukweli.

 
Last edited by a moderator:
Ukifuatilia kwa makini siasa za mh Edward Lowassa utaona tofauti kubwa sana kati yake na wanasiasa wengine, lowassa amekuwa mhanga wa matusi, kebehi, kashfa na siasa za maji taka.Watanzania bwana we umesikia sera yoyote toka kwa lowasa?kumtoa babu seya ndio sera?hizo sera anazoongea kwa dakika kumi ndio sera?uchaguzi upi barani africa ulikuta mgombea ananadi sera dakika kumi?hata huko walikoendelea kama wakati wa obama uliona akiambia watu waende mitandaoni kusoma ilani ya chama chake?acheni ushabiki muwe realistic

Lakini kinachonifurahisha kuhusu huyu bwana, hakuna hata siku utamamsikia akimjibu mtu, akimtupia dongo, akimuongelea mtu. Lakini wanasiasa wengine hasa wa ccm, wamesahau kunadi sera zao na kubaki wakimjadili yeye tu na kusahau sera ya vyama vyao. Mtego huo ameingia na magufuli, amebaki akitumia muda mwingi akimuongelea lowassa!! Wakati lowassa anaongelea wakulima wasikopwe, wazee wapewe pension nk.

Nimependa siasa za Lowassa, hasa kwa sababu hamjadili mtu anajadili issues.
Watanzania bwana hizo sera anazozisema kwa dakika kumi ni zipi?ulishaona wapi katika chaguzi barani africa tu mgombea ananadi sera dakika kumi?na hata kwa nchi zilizoendelea ulishawahi ona mgombea anaongea dakika kumi kunadi sera?tuache ushabiki hata kama unahitaji mabadiliko angalia hayo mabadiliko yanapatikanaje sio alimradi mabadiliko.
 
Watu wanasema ukweli halafu ninyi eti mnasema vijembe.

Huyu Lowassa ni fisadi na mgonjwa sana.

Unataka ajibu nini wakati anaambiwa ukweli.



Kwani Magufuli ni mzima? (isome kwa sauti ya Sumaye). Kama mwezi ujao hataenda Ulaya labda siyo Mimi!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom