50thebe
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 4,139
- 4,124
Wanabodi
Nisiwachoshe na maneno lukuki.
Ni hivi, mboni ya viongozi wa UKAWA waliona kitambo namna mchakato wa Katiba mpya unavyopotoshwa na kundi la Wana CCM wenye malengo binafsi. Viongozi wa Ukawa wakaona sio sahihi kuendelea kushiriki vikao vya Bunge Maalum la Katiba. Wakasusa na kujiondoa huko Bungeni.
Kujiondoa huko Bungeni kuliibua mijadala ya kuwabeza na kuwashambulia UKAWA kwa kila namna ya kejeli. Wapo walosema UKAWA wapuuzwe. Kwa hali ilivyo sasa, inaonesha haiwezekani kuwapuuza UKAWA maana wanaonekana kuwa 'jiwe kuu la pembeni'.
Niwapongeze sana viongozi wa UKAWA na timu zao. Swali linabakia, UKAWA walifahamu aje kuwa kusimamia maoni ya Katiba ya Wananchi kunatosha kuibwaga vibaya CCM na serikali yake? Ama tunachoona ni kisehemu tu cha ishara ya nguvu ya umma?