Nimependa Mboni ya Viongozi wa UKAWA

Nimependa Mboni ya Viongozi wa UKAWA

Hoja ya msingi hapa ni kuwa kikundi kinachojiita UKAWA kimesema rasmi hakiendi bungeni tena hata kwa hoja yoyote ile.

Hoja inayofuatia ni kuwa, wanaweza kusimama katika maneno yao au ndiyo yaleyale ya siasa za kilaghai ambazo kesho au kesho kutwa tutawaona tena bungeni baada ya kula matapishi yao.

Imefahamika kuwa kilichokuwa kinawafanya wana kikundi kinachojiita UKAWA kuwepo bungeni ilikuwa ni Sura ya 1 & 6 ya Rasimu ya Katiba ambayo hoja zake ni Serikali moja, mbili au tatu.

Ikumbukwe kuwa hoja ya serikali moja, mbili au tatu iliyoko kwenye Rasimu ya Katiba katika sura ya 1 & 6 imeishafungwa kwa sasa kilichobaki ni upigaji wa kura baada ya sura zote 17 kujadiliwa kwa maana nyingine, UKAWA kwa sasa hawana hoja mpaka tena itakapofika siku ya upigaji wa kura.

Kinachojadiliwa kwa sasa ni Sura 15 zilizobaki ambazo ni muhimu zaidi ya madaraka ya viongozi yaliyoko kwenye idadi ya serikali zilizoko kwenye Sura ya 1 & 6 ya Rasimu ya Katiba ambazo UKAWA kwa uwezo wao mdogo wanadhani uwingi wa serikali ndiyo utawafanya wapate pia nafasi za uongozi.

Kwenye mambo ya kitaifa na mstakabali wake ndani ya demokrasia, jiwe kuu la pembeni ni sanduku la kura na siyo wanasiasa kama unavyotaka kutuaminisha.

Sitashangaa kuona au kusikia kama hawa wana kikundi cha UKAWA wanafuatilia sana yanayotokea kwenye Bunge la Katiba kwa sasa, hii ni sawa sawa na fisi kunyemelea kama mkono utadondoka. Mkono haudondoki na mtasubiri sana.

Bunge la Katiba linaendelea kama kawaida kama Mzee Sitta anavyobainisha hapa,

[video=youtube_share;EkEtBWIZ7Js]http://youtu.be/EkEtBWIZ7Js[/video]
Hakuna litakalowezekana bila sura ya 1 & 6 kupata muafaka kwani nyingine zote zitarahisishwa na sura hizi mbili e.g umiliki wa ardhi, tunu za taifa kujadiliwa na adhabu zake, muundo wa uongozi, haki za binadamu n.k na ndiyo maana zilijadiliwa za kwanza!
 
Wewe Bwana Diwani acha upotoshaji! usipotoshe kitu ambacho unajua unapotosha huo ni Uzezeta! Embu kwa akili hiyo kidogo uliokuwa nayo waondoe mawaziri wote wa Muungano halafu hao wanaobaki ni wa nchi gani! Gharama za kuendesha wizara zao zinachangiwa na nchi gani? halafu uje utuambie hapa kila tarehe 9 december kuna public holiday ya nchi gani na kwa nini mnatumia mabilioni ya kodi zetu kwa Taifa ambalo halipo! kama basi mtakuja na kusema ni kumbukumbu hivi kwa nini msikumbuke basi na mwaka 1918 walioondolewa wakoloni wajerumani ambao walikuwa hawasomeshi wazawa wakaja waingereza waliosomesha wazawa? Acheni kutudanganya
Ndugu, nadhani hujaelewa hoja ya msingi lakini ikumbukwe kuwa, maswali yako haya yatajibiwa wakati au baada ya bunge la Katiba linaloendelea kwa sasa.

Cha muhimu, stay tuned!
 
Hakuna litakalowezekana bila sura ya 1 & 6 kupata muafaka kwani nyingine zote zitarahisishwa na sura hizi mbili e.g umiliki wa ardhi, tunu za taifa kujadiliwa na adhabu zake, muundo wa uongozi, haki za binadamu n.k na ndiyo maana zilijadiliwa za kwanza!
Ndugu, Habari ndiyo hiyo!

By the way, wewe nadhani ulileta hoja hapa kuhusu bunge kusitishwa na Rais Kikwete. Imekuwa vipi tena?. Hoja yako bado inasimama?.

Kuishi kwa matamanio hakuwezi kufanya matamanio kuwa ni reality or truth.
 
Ndugu, nadhani hujaelewa hoja ya msingi lakini ikumbukwe kuwa, maswali yako haya yatajibiwa wakati au baada ya bunge la Katiba linaloendelea kwa sasa.

Cha muhimu, stay tuned!
sijaelewa kitu gani Mwana Diwani! Tambua kuwa huku UKAWA sipo kimakosa nilikuwa na Msimamo kama wa UKAWA tangu nipo kidato cha pili Lomwe Sekondari zaidi ya miaka 16 iliyopita! nimekuwa Mwanachama na kiongozi wa CCM ngazi ya Wilaya kwa kipindi cha Miaka mitano! so hila za CCM nazijua kindaki ndaki labda kwa kifupi tu nikueleze Msimamo wa serikali mbili ni wa Viongozi wa CCM tu tena Kamati kuu na sio msimamo wa wanaccm walioko huku vijijini! Muundo wa serikali Mbili haujawahi kuwasaidia Walalahoi hata siku moja zaidi ya kuzidi kuwatia umaskini! hakuna cha stay turned wala nini ndivyo maccm yalivyozoea kutupumbaza na kauli za matarajio feki Mwanadiwani Kauli za matarajio kama Uwazi na Ukweli ya Mkapa ikasaidia kuanzisha epa, na kwa mara ya kwanza nchi ikazalisha wakimbizi kutoka Pemba, Kukodi management za kuongoza makapuni yetu, kuiuzia viwanda vya umma na ile kali ya Maisha bora kwa kila mtanzania ambayo imetusababishia deni la laki sita kwa kile binadamu anaeishi within Tanzania Boundaries, huku kwa mara ya Kwanza Usalama wa taifa wakijidhihirisha kuwa ni Maisrael wa kienyeji kwa kutoa watu meno bila ganz
 
Ndugu, nani amekuambia kwenye Bunge la Katiba kuna serikali achilia mbali serikali ya CCM?

Ndani ya Bunge la Katiba kuna wajumbe pekee ambao wanafanya kazi kwa misingi ya kanuni na sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

kikwete alisimama kwenye bunge hilo na kuhamasisha maslahi ya CCM badala ya TZ na nyie mkafurahi kweeli.
leo mnaumbuka na tutawaumbua kweli kweli.
 

Mwanadiwani


Mkuu umehangaika kweli kutetea unachoamini kuwa ni sahihi.
Hata hivyo hujaweza kufifisha umadhubuti wa 'mboni ya viongozi wa ukawa'.

FYI, mambo yaliyofanywa na UKAWA mpaka sasa ni rasha rasha tu, masika yenyewe inakuja. Tarajia fisi ateleze kwenye kichuguu.
 
Back
Top Bottom