Nimepatwa na huzuni kuu baada ya kutangazwa majina ya walimu, nimekuwa nikijitolea bila mafanikio

Sikupi pole wala faraja yoyote huna akili kabisa wewe!!! Hivi unawezaje kujitolea kijana shupavu mwenye degree ya sayansi umeshindwa kujiajiri kazi na fursa Zipo nyingi nchi yetu Tanzania

Walimu hivi huwa mnarogwa au mnakufa mnakuwa misukule?? Kamshahara ambacho hakana hata posho, msoto wanaopata walimu na wewe unataka?? Ahsee nikushauri kitu bora ukafanya mambo yako hujachelewa maana kule wanaenda walokata Tamaa ya maisha, waliojawa laana hata shetani hawataki Wala Mungu hawataki na wananchi hatuwataki majizi ya kura siku za uchaguzi ndomaana hayaendelei
Kama una namna ya kumsaidia ili aweze kujiajiri msaidie.
 
KW hiyo shule zifutwe kama hutaki watu wawe waalimu?think greate Acha mihemko na chuki binafsi.
Ndio zifutwe kama serikali imeshindwa kuwalipa vzr walimu mbona IST, FEZA SCHOOLS, MOSHI NA IRINGA INTERNATIONAL SCHOOL zinawalipa na kuwahudumia walimu wao vzr tu inamaana serikali inazidiwa mkwanja na mtu binafsi mpaka walimu wapewe pesa za kisenge.

Kama wanaona ngoma ngumu wasiajiri Wala kuongeza shule maana wameshindwa kuwajali walimu
 
Ndio zifutwe kama serikali imeshindwa kuwalipa vzr walimu mbona IST, FEZA SCHOOLS, MOSHI NA IRINGA INTERNATIONAL SCHOOL zinawalipa na kuwahudumia walimu wao vzr tu inamaana serikali inazidiwa mkwanja na mtu binafsi mpaka walimu wapewe pesa za kisenge.

Kama wanaona ngoma ngumu wasiajiri Wala kuongeza shule maana wameshindwa kuwajali walimu
Sikweli, pale wanalipwa vizuri wazungu zaidi na zaidi, wanawalinzi house girls mshahara kima Cha chini Cha serikali, wanapewa nyumba,au watu wa nje, wazawa hawalipwi kivile, mi nakuambia, morogoro international pale Kama nyumbani.
 
Ajira sio ndo kutoboa maisha,hususani ualimu nikukimbilia matatizo zaidi ,,ebu badili mtazamo Fanya kama hujasoma nenda kapambane' utafanikiwa, ebu angalia miaka ulio jitolea ungekuwa ume kaza haswa mtaani naami ungekuwa sehemu Fulani Sasa!
𝐊𝐚𝐦𝐚 𝐤𝐰𝐞𝐥𝐢 𝐯𝐢𝐥𝐞
 
Pole sana ticha, baadhi ya halmashauri huwa zinawasaidia walimu wanaojitolea ili wapate ajira, kuna binti mmoja amemaliza chuo mwaka jana tu 2022 na ameajiriwa kwenye ajira hizi kwa misaada wa halmashauri.
𝐊𝐰𝐚 𝐦𝐚𝐬𝐨𝐦𝐨 𝐠𝐚𝐧𝐢?....
 
Mdogo wangu kachaguliwa kwenda some where anazingua,kazoea maisha yake na ana biashara kubwa mtaji zaidi ya 15,000,000,mama ake amesema asipoenda anamwachia laana
𝐦𝐡 𝐤𝐰𝐚 𝐡𝐢𝐲𝐨 𝐛𝐢𝐚𝐬𝐡𝐚𝐫𝐚 𝐢𝐭𝐚𝐤𝐮𝐟𝐚 𝐚𝐮
 
Nina biashara zangu na nimeajiri vijana kumi wote nawalipa mshahara Kwa wakati unaotunza Familia zao nawanasomesha shule za private, mchana wanakula kazini Kwa pesa yangu nawalipa na pesa ya nauli kila siku elfu tano Kwa mmoja mmoja na posho kila tarehe 15 huwa nawapa nusu ya mshahara wanaopokea. Una lakuongeza??
𝐒𝐚𝐰𝐚 𝐦𝐡𝐚𝐲𝐚
 
Sikupi pole wala faraja yoyote!!! Hivi unawezaje kujitolea kijana shupavu mwenye degree ya sayansi umeshindwa kujiajiri kazi na fursa Zipo nyingi nchi yetu Tanzania

Walimu hivi huwa mnarogwa au mnakufa mnakuwa misukule? Kamshahara ambacho hakana hata posho, msoto wanaopata walimu na wewe unataka? Ahsee nikushauri kitu bora ukafanya mambo yako hujachelewa maana kule wanaenda walokata Tamaa ya maisha, waliojawa laana hata shetani hawataki Wala Mungu hawataki na wananchi hatuwataki majizi ya kura siku za uchaguzi ndomaana hayaendelei
Mpe connection sasa, sio unaponda tu then unamuacha njia panda
 
Kichwa cha habari chahusika,

Nimejikuta nikapatwa na huzuni kuu mara baada ya jana kutangazwa majina ya waliochaguliwa kada ya ualimu na kutoona jina langu.

Mimi ni muhitimu wa shahada ya ualimu miaka sita iliyopita katika masomo ya sayansi.
Nilihitimu mwaka 2017. Tangu hapo nimekuwa nikijitolea huku nikiomba ajira zinazotangazwa lakini mpaka leo hii jina langu halipita.

Natamani kufahamu changamoto ni nini, Maana kama kigezo cha miaka ninacho, Kuhusu masomo ni sayansi nikiwa nimemeja kwenye somo la biolojia.

Nilijianza kujitolea kupitia mfumo wa TAHOSA mwaka mmoja na baada ya hapo niliendelea kujitolea kufundisha tangu 2019 mpaka leo.

Naomba msaada wa kuwasiliana na Mama Kairuki. Au kwa yeyote mwenye mchango niweze kupata ajira niondokane na msongo wa mawazo kwa kushindwa kusaidia wazazi wangu ambao ni wazee na wanahitaji msaada TOKA kwangu.

Natanguliza shukrani kwa wote

Haujui kwamba ajira ni utumwa?
 
Pole kijana, well and good kama huwa unaomba. Basi kijana wangu kuwa mtulivu na mwenye Subra, binafsi naamini kwa hakika bado kitambo kidogo mambo yako yatakaa sawa.

Kijana, tafadhali usipoteze consistency ongeza bidii zaidi unapoendelea kujitolea na kamwe usikatishwe tamaa na situation ya kutoliona jina lako awamu hii, ipo second selection I'm sure you will be shortlisted and placed somewhere kwa kazi na ninakutakia majukumu mema ktk ya ualimu in Advance, IN JESUS NAME, Amen. Asante sana

Second selection haipo kiongoz usimtie moyo
 
Karibu site kwangu nikufundishe kushona na kufunga mapazia kwenye hotel,nyumbani za watu maofisini nk.kwa mwezi hukosi laki sita kwa kazi za kufunga tu na milioni mbili hivi kwa kushona na kuuza.

Nina elimu pia Kama wweee.
 
Back
Top Bottom