Nimepata pigo naomba ushauri

Nimepata pigo naomba ushauri

Mimi ni kijana wa umri wa miaka 20 nilimaliza form four 2013 namshukuru mungu nilifaulu na kupata division one.
Nilipokuwa naanza form 5 quarter ya kwanza shuleni nilisumbuliwa na magonjwa fulani ambayo yaliniweka nje muda mrefu na ikabidi nipostpone mwaka wa masomo ili nipate matibabu kikamilifu hivyo mwezi huu wa saba ndio inabidi niaanze upya form 5...
Sasa tatizo langu ni kwamba napata depression kuona wenzangu wameniacha pia kwenda kusoma na watoto ambao nimewazidi miaka 2-3, pia napata mashaka kuona ntamaliza chuo na umri mkubwa wa miaka 25 ukilinganisha na wengine watamaliza na 22-23, naomba ushauri tafadhali!!!
Uliuona ule uzi mama mmpja huko Kenya anasoma na watoto wake shule ya msingi? Unajuwa anawazidi miaka mingapi?
 
kwanza kwa nini hupati depression wenzako wagonjwa walikufa wewe uko hai? , wenzako walomaliza f4 wana zero hawategemei kumaliza chuo maishani hata wawe na miaka 69? aliyekwambia miaka25 ni mingi kwakumaliza chuo nani?

mshukuru mungu ulifaulu &umepona na unaendelea na shule mdogo wangu mpendwa. soma kwa bidii huo umri usikutishe kwanu hao watoto kuna waloficha umri wai waliresit mara kibai hapo utakuta ni kaka zako na dada zako.

cha msingi piga kitabu ufaulu vizur hapo wewe ndo utakuwa babyy .

usipende kufanya mambo kwakuangalia watu hutakaa ufanikiwe, ukifika chuo utashangaa kukuta watu wana miaja 40 ndo kwanza wanasoma chuo mara ya kwanza.
kila la kheri usome kwa aman na ufaulu

Asante mummy!!!!
 
Da yaani bado utakuwa una mawazo ya kitoto nakumbuka wazee niliokuwa nao chuo tunasoma nao halafu mbaya zaidi wanatumia nondo hataree akina mama wanaandika vibuti ktk mapaja anatoa uku unamwangalia anakwambia tulia dogo. Ss ww unaona noma kusoma uku unatumia akili zako!
 
Muhimu nenda kakazane na masomo, sababu hao wakikupita kwa marks si ndio utakimbia shule.

Kuwa tayari kwa mapambano ya kusona na usijali kama hao wadogo kwako wakipata % kubwa zaidi yako. Wewe kasome kwa umri huo hamtaweza juana nani mkubwa kuliko nani labda ujitangaze au wakiona umemind uliowaacha ulipotoka wataviongea.

Kuwa mgumu umuhimu kupasi ndugu hao dogo wana akili pia. So wachukulie kama mko sawa and enjoy studying.
 
We dogo huna akili sawasawa. Basi usiende ili usije kumaliza chuo na umri mkubwa na usisome na watoto wadogo unaowazidi.
 
Back
Top Bottom