Duuh ni kweli kabisa.
. Ila ni kitu kinacho nishangaza sana. Kuwa binadamu anaweza kuwa manipulated kuona kuwa yeye ni hawezi Kamwe kujiwezesha kuwa tajiri kisa yuko mazingira ya kimaskini.
Nahisi hata kama hatuwezi kuumaliza umaskini ila tukiwapa awareness binadamu wataweza kufanikiwa
HAPANA,..NEVER,.....
Siku zote maisha yapo katika PYRAMID STRUCTURE katika kila angle ya maisha,....wanaofanikiwa ni wachache sana kuliko wanaofeli....
kwanzia shuleni walioanza darasa la kwanza sio watakaomaliza form four wala chuo,...
kwenye biashara walioanza biashara aina moja , kwa mitaji sawa sio watakaokuwepo kwenye biashara miaka mitano baadae, wengine watakuwa wameshafirisika, wengine wako palepale na wengine wamefanikiwa,...
kutokana na human nature,... binadamu ana wivu, tamaa, uvivu , pia negative energy visivyo na mipaka,(limitless)....
hivyo kutaka kusaidia wengine hakutamaliza tatizo hili, hata kidogo, bali kutaongeza (COMPLEXITY)...
mfano,..
katika kundi la watu watakaosaidiwa wataibuka watu watakaoona msaada ni haki yao, na hivyo wataraise hali ya utegemezi(uvivu).. tayari watakuwa mzigo kwa wengine,....waulize watu waliojitoa kuwapa mitaji ndugu zao, au kuwasaidia kwa namna yeyote ile ili kuwakwamua kutoka katika UMASIKINI,....
pili, tazama mifumo ya elimu na science and technology,...
miaka kadhaa nyuma Watu waliamini elimu kama njia sahihi ya kumfungua mtu ubongo na kumfanya aweze kuwa na fikra pana na yakinifu zitakozoweza kumfanya afanikiwe vyema zaidi kuliko mtu asie msomi,.. hivyo elimu ilitazamiwa kama msaada mkubwa sana wa kuwakomboa watu katika lindi la UMASIKINI na changamoto zao,...swali ni je?...unaamini elimu kama njia ya kutoa msaada dhidi ya UMASIKINI imefanikiwa, na je hatuna wasomi na waajiriwa masikini katika jamii zetu?,...
science and technology,..
miaka ya 1800 mpaka 1900 wakati wanasayansi wanafanya mambo makubwa kabisa yaliyoperekea mapinduzi ya viwanda, waliamini kuwa kufikia miaka ya 2000 tatizo la njaa, halitakuwepo kabisa , kwani sasa binadamu atalima kwa TREKTA, hivyo atalima eneo kubwa sana kwa nguvu kidogo, atatumia MBOLEA za kisasa na hivyo kupata mazao mengi sana, pia ataweza kupambana na uhaba wa mvua kwa kuwa ana nyenzo mbalimbali kama vile water pump n.k...hili liliwaaminisha kuwa binadamu ataweza kuwa chakula kingi sana, kiasi kwamba hataijua tena njaa,....
swali ni je, mpaka sasa ni watu wangapi wanaolala bila kupata chakula siku nzima , hata kwa nchi zilizo na amani kama tz,...
kwa kifupi zaidi, binadamu hasaidiki kwasababu ya COMPLEXITY and CURIOUSLY MINDSET aliyonayo,... "BINADAMU ANA SWALI KWA KILA JIBU"
waulize watu ambao wana mioyo ya kusaidia wengine bure bure ni nini hulipwa kama sio dhihaka, dharau, jeuri na maumivu,...
kuumaliza UMASIKINI miongoni mwa mwa masikini ni jambo gumu sana , kwani sio jambo la INDIVIDUALISM, bali ni la GOVERNING SYSTEM,...na maumivu makubwa ni lazima watu wayapitie, wayaishi , na wayakubali,...jambo ambalo si rahisi,...na hapo ndipo CAPITALISM INAZIDI KUKOMAA NA KUSHINDA,..