Nimeona nitumie njia hii kupata mtaji. Potelea mbali

yello masai

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
3,636
3,660
Natumaini mko salama wadau wa jukwaa.

Mwaka wa kwanza umepita, wa pili, wa tatu na sasa wa nne ndo huu. Hii ni tangu nihitimu na sina kazi ya maana. Nikiwaza kufanya biashara mtaji ni kikwazo.
Nimewaza kutangaza watanzania wanichangie mtaji nikaona hawawezi. Ila nikaona nitawachangisha kwa njia nyingine tu.

Hakuna asiyejua kuwa watanzania wamekuwa mabingwa wa kuchangia harusi. Nimeamua nimtafute mchumba atakayekubaliana na wazo langu then tutangaze ndoa. Kupitia kamati tutapanga bajet ya harusi hisiyopingua Milioni 25. Zitasambazwa kadi na watu watachanga michango. Kwa njia zozote nitahakikisha mpokea michango ni mtu anayejua lengo, au nitapokea mwenyewe (nitajipigia debe kwenye kamati).

Najua hela zitachangwa tu. Ikishafika milioni 10 tutaandaa tukio la kupoteza hiyo pesa (tukio bado nawaza jinsi ya kulipanga). Pesa ionekane imepotea au imeibiwa, then tufanye the lowest budget marriage na mchumba wangu(ikiwezekana bila hata sherehe).
Baada ya miezi mitatu tutafungua duka na kuanza biashara. Kutumia hiyo pesa.

Maisha yakiwa magumu unakuwa mgumu zaidi na akili zaidi.
 
Natumaini mko salama wadau wa jukwaa.

Mwaka wa kwanza umepita, wa pili, wa tatu na sasa wa nne ndo huu. Hii ni tangu nihitimu na sina kazi ya maana. Nikiwaza kufanya biashara mtaji ni kikwazo.
Nimewaza kutangaza watanzania wanichangie mtaji nikaona hawawezi. Ila nikaona nitawachangisha kwa njia nyingine tu.

Hakuna asiyejua kuwa watanzania wamekuwa mabingwa wa kuchangia harusi. Nimeamua nimtafute mchumba atakayekubaliana na wazo langu then tutangaze ndoa. Kupitia kamati tutapanga bajet ya harusi hisiyopingua Milioni 25. Zitasambazwa kadi na watu watachanga michango. Kwa njia zozote nitahakikisha mpokea michangu ni mtu anayejua lengo, au nitapokea mwenyewe (nitajipigia debe kwenye kamati).

Najua hela zitachangwa tu. Ikishafika milioni 10 tutaandaa tukio la kupiteza hiyo pesa (tukio bado nawaza jinsi ya kulipanga). Pesa ionekane imepotea au imeibiwa, then tufanye the lowest budget marriage na mchumba wangu(ikiwezekana bila hata sherehe).
Baada ya miezi mitatu tutafungua duka na kuanza biashara. Kutumia hiyo pesa.

Maisha yakiwa magumu unakuwa mgumu zaidi na akili zaidi.
Naskia wote Wanaokuchangia huwa wanawekeza tu kwako au wanalipa madeni ya jinsi ulivyowachangia wewe. Hawachangi tu kiholelaholela, sijui ni kweli.
 
Naskia wote Wanaokuchangia huwa wanawekeza tu kwako au wanalipa madeni ya jinsi ulivyowachangia wewe. Hawachangi tu kiholelaholela, sijui ni kweli.
Ni kweli. Na mimi nikishafanikiwa kwenye biashara zangu nitawachangiaga tu tena zaidi
 
Back
Top Bottom