Kuna rafiki yangu mmoja kaniomba ushauri. Nami nimeona si vibaya nikiwashirikisha wan JF ili kupata mawazo zaidi.Samahani nitatumia majina ambayo siyo halisi.
Lily ana mchumba wake anaitwa Julius, ambao wamekuwa wachumba kwa miaka 5. Wote walibahatika kugradute na kupata Barchelors degree japo walikuwa wanasoma vyuo tofauti. Kipindi wanasoma walikuwa wakitembelea na kuwasiliana maana vyuo vyao havikuwa mkoa mmoja.
Julius ndo aligraduate mapema maana degree yake ilikuwa ni miaka 3 na Lily ni 4. John alikaa mwaka mzima bila kubahatika kupata kazi. Lakini kipindi Julius anatafuta kazi ilifika kipindi akawa hana fedha na Lily akawa anatumia pesa zake za mkopo wa Bodi kumsaidia rafiki yake. Hatimae Julius alipata kazi lakini akapangiwa mkoa mwingine tofauti tena. Katika kipindi chote hicho cha uhusiaono wao walikuwa wakikutana na Lily alikuwa strictly sana hakutaka kufanya mapenzi bila mpira.
Lily aliamua kumwambia mpenzi wape huyo wapime lakini akamwambia hana nafasi hadi atakapoipta watapima ili waache kutumia mpira.
Uchumba uliendelea na Lily alipokuwa akipata likizo chuo anaenda kumuona japo ilikuwa safari ya cku mbili kufika alipokuwa anishi Julius. Lily naye baadae alimaliza na yeye alichelewa kupata kazi kama miezi minne, lakini katika kipindi hicho chote japo Julius alikuwa ameshapata kazi wala hakuwahi kumtumia hela yeyote ile imsaidie na Lily alikuwa akimuelezea hali halisi ilivyo.Baadae na lily alipata kazi mkoa tofauti na mchumba wake huyo. Baada ya Lily kupata kazi ,Julius naye alikuwa akipita kumsalimia wakati alipokuwa akienda kwao yani si kama kumtembea-alikuwa anapita,hivyo angeweza kufika leo na kesho yake au keshokutwa akaelekea kwao.
Lily alijitahidi kuwa anamnunulia zawadi mabali mbali mchumba wake-vikiwemo viatu, mashati, n.k-Ila kwa julius alikuwa c wa kumbebea mwenzake chochote kile labada akutane narafiki zake wamshawishi hasa wale waliokuwa wakimfahamu lily msimamo wake na upendo wake wa dhati kwa Julius.
Baada ya miezi sita Lily aanze kazi, Julius alimuamba hela kama 350,000 na lily alimpatia, sasa Julius akawa kila baada ya muda atamwambia mwenzake hana hela na lily baada ya kuona hivyo-akaamua kuwa anamwambia naye hana kwa wakati huo.
Lily akawa anashindwa kumuelewa mpenzi wake huyo hela anafanyia nini.Mara nyingi jioni au asubuhi Julius alikuwa akipiga sanza kutakaimu na ku kujua Lily anafanya nini ana nani ana yupo wapi.Tabia hii ilizidi hata Lily alipokuwa na Kaka zake,Julius aliomba akipiga simu Lily asiikate ili ajue wanaongea nini. Tabia hii ilimkera saana Lily.
Relationship yao ikawa na ugomvi usioisha, Lily alikonda saana na akawa anaumia jinsi anavyompenda Julius na japo hapati chochote kutoka kwa mchumba wake huyu na hata hakuna msaada wowote ule anaoweza kupata shida akamkimbilia kama rafiki na mchumba wake.
Kila walipokuwa wakikutana lily anaongelea suala la kupima lakini Julius alisikuwa akisema yupo bize na kazi hivyo hawezi kupata muda.
Mwaka 2007 Lily aliyopata short course kwenda nje ya nchi, alifunga safari kwenda kumuaga julius. Alikaa siku tatu lkn kataika siku hizo zote mpenzi wake hakumnunulia hata soda ,wala kusema wakanyooshe miguu kidogo jioni moja wapo. Akiwa kule alikumbushia suala la kupima na Julius akamwambia ina maana hamuamini toka waanze relationship? Akamwambia Lily lkuwa ikitokea wakaenda kupima akakuta Lily anavirusi yeye atamuoa tu bila kujali hali ya Lily, akamuuliza lily ina maana tukienda kupima ukakuta nina virusi utaniacha? Lily hakujibu bali aijawa na woga wa hali ya juu kutokana na maneno ya mchumba wake Julius. Lily alirudi akaendelea na mipango yake ya kwenda nje ya nchi.
Kabla ya kuondoka alipitia Dar ambapo alikuwa anaprocess document zote iliwepo visa, na baadhi ya nyaraka alizoambiwa aende nazo. Julius alimpigia simu na kumwambia aende tena waonane lakini Lily alimwambia cwei kuja maana siku zimeisha na naprocess doucument zangu. Julius alianza kupiga simu na kulalamika kuwa yupo kwa wanaume ndiyo maana anakataa kwenda kumuaga
Mda ulipo fika Lily aliondoka na akiwa kule kwa kweli mawasiliano hayakuwa mazuri kati yake yeye na mchumba wake. Aliporudi mambo yakaendelea hivyo hivyo lakini bila ya Julius kutaka kwenda kupima. Anachomwambia ni kwamba waoane tu. Mpaka sasa Lily hajui afanye nini!!
Ameniomba ushauri na mimi naomba kwenu wadau!!