Kwa niliyoyashuhudia katika mahusiano, naweza kusema kwa ujasiri kwamba, mahusiano ya kimapenzi ni ubatili mtupu chini ya jua. Yafuatayo ni aina za mahusiano na changamoto zake. Je wewe ulifanyaje ulipokumbana na changamoto za wanawake wa aina hizi?
- Wenye pesa: hawa ni pasua kichwa, atakuamrisha, no kubebishana yaani, yeye kazi kutoa maagizo tuu mwanaume unabaki kama mtumwa vile.
- Wasio na pesa: hawa ukiomba namba tu tayari umepigwa mzinga. Ukiingia kingi anahakikisha anakuchuna wewe na wakati huo huo ana wengine kadhaa. Akikuomba 50k, hiyo sms inaenda kwa watu kama nane hivi. Siku mkijijua mko wangapi ndo utaelewa somo. Hata ukisema ngoja utafute aliyetulia umuendeleze kimaisha yaani siku anajikwamua kidogo tu, tena siyo sana, kidogo tuu kafikia hatua flani baba utajuta kulifahamu jiji la makonda.
- Kuna kundi lingine huwa nashindwa pa kuwaweka: Labda niwaite strategists; Wanaweza kuwa na pesa au asiwe na pesa. Huwa nawafananisha na simba aliye kwenye mawindo. Unajua simba hakimbizi kila mnyama mbugani, huchagua mmoja na hula naye sahani moja mpaka amkamate. Akimaliza kula mawindo ndo hupanga mkakati wa kutafuta kitoweo kingine. Mwanamke wa kundi hili hamkubalii mwanaume mpaka awe na lengo lake flani, na siku likitimia lazima akulize. Na akishajua una hicho anachotaka kwako atatengeneza mazingira aonekane anakupenda sana. Siku akitimiza lengo lake maji utayaita mma. Akikumaliza anaenda kwa mwingine.
- Ukimpata wa kutoka bushi huko akaja mjini, yaani akishajanjaruka mjini unaanza kujuta kwa nini ulimleta mjini, bora angebaki kijijini.
- Wengine hawajajiendeleza kielimu, sasa wewe msaidie kujiendeleza. Baada ya kuvaa joho na ana kazi yake ndo utajua kilichomtoa nyoka pangoni.
- Wake za watu: Wanaweza kuwa ndani ya kundi mojawapo hapo juu, hususan namba 1 na 3. Wengi huamua kutoka nje ya ndoa kwa sababu kuu mbili. Tamaa ya pesa na wanaume zao kutowatosheleza kimwili. Wanaume wengine wana matatizo ya kusukari, wengine gap ya umri kati ya mwanaume na mwanamke ni kubwa sana. Kwa hiyo inafika hatua mwanaume anaanza kuchoka bado mwanamke anadai. Wengine safari nyingi hawakai nyumbani. Hakuna namna wanawake wanaanza kutafuta vibenten. Fanya tafiti, kuna lodge maarufu ambazo zinapata wateja wengi sana kati ya saa 4 asubuhi na saa tisa mchana. Huo muda wanaume tupo makazini tumewaacha wanawake majumbani mwetu au nao wapo makazini mwao na wameshajua ratiba ya baba anarudi jioni kama siyo usiku. Mke wa mtu akitaka kukutunuku wengi wao wako radhi amshushue na kumsema vibaya mumewe. Utasikia, oooh, yaani nina miezi sita sijawahi kufika kileleni. Sasa wewe nenda kamkojoze hata goli 6 usiku mmoja. Fine, atakusifia Ila ujue kuna siku atakutema kama big G akiona kuna hatari ndoa yake kuyumba.