Nimenusurika kuchezea kichapo arabuni kwa kudhaniwa ni mmarekani!

Tatizo lako umezidisha swaga, hata jamaa pale Savanna Lounge na RG wanajua wewe mmatumbi..lol
 

Mhhhhh sidhani kama hao ulosema ni waarabu ni wajinga kiasi hicho wasiweze tofautisha kati ya Muamerika na mtu toka Africa. Kwanza umesema ulikuwa na mwenyeji wako, ilikuwaje wakakuuliza wewe usojua lugha ya kiarabu badala ya mwenyeji wako??? Hapa nanusa harufu fulani ya ***************.
 
did you smell a rat?
 
Ni wapi huko i.e nchi gani?
 
Unalosema ni kweli tupu hata mie nilishawahi kuulizwa na hao jamaa Emirates je we dini gani? Sasa kwani kuulizwa dini na si kitu kingine- of course inaeleweka!
 

Hapo naona hiyo stori kidogo imechakachuliwa. Sasa wewe ulifahamu vipi kiarabu hicho kwa ghafla? Nao wamarekani huwafanyia hivyo hivyo waarabu wanaokwenda kwao.

Na hiyo pia sio ngeni kwani mimi mnamo mwaka 90 nilikwenda South Korea na kila nilipopita nilikuwa naitwa (kwa kejeli) ...... hey Americano!

Wanaamini Afrika ni nchi masikini sana na hawana uwezo wa kufika huko kwao.
 
Silu moja nilikaa katika hoteli mji mmoja mdogo ujerumani. Asubuhi wakati na check out, nikamwambia yule dada pale checkout counter kuwa nahitaji taxi. Alivyokuwa anapiga simu kuita taxi, nilimsikia akimweleza taxi driver kuwa abiria atakayembeba ni Mmarekani. Hata mimi nilipata mawazo kuwa picha waliyozoea ya watu wenye rangi kama zetu ambao wanaoweza kukaa kwenye hoteli kama ile ni Wamerakani weusi tu na sio Waafrika. Nikamuona amepitwa na wakati na anahitaji darasa. Bahati mbaya kwake sikuwa na muda wa kutoa hilo darasa.
 
Kijana ah kumbe ni mzee! Usiseme uongo weye. Mmarekani hapigwi hivyo. Huoni kwenye tv jinsi wamarekani wanavyopigwa iraq,afghanistan, palestina etc. Inavyooneka labda walikufananisha kua ukibaka unataka kuwaibia inaingia akilini. Maana nyie si mnajulikana banaa si ndio mulioniibia simu yangu ktk daladala? Halafu pale taifa mukamnyan'ganya brother simu na hela.
 
MOD hi Topic mimi kwa mawazo yangu naona bora uipeleke hapa ( Jokes/Utani + Udaku/Gossips) Kwa sababu hapa sipo mahali pake haingii akilini kuwa wewe uende Uarabuni kisha uwe na Mwenyeji wako kisha hao Waarabu waanze kukuliza Maswali uliwajibu kwa lugha gani Kiswahili au kiarabu? kwa sababu wewe hujuwi kiarabu uliwajibu kivipi? Hii ni Joke ingefaa MODERATOR Topic hii uihamishe iwe kule kwa ( Jokes/Utani + Udaku/Gossips) Samahani Mkuu MODERATOR sipendi kukuingilia kazi yako nakupa mawazo yangu asante.
 

Oyaa! Wewe ulichotakiwa kufanya Umangani ni kufuga madevu na kuvaa kanzu na bagharashia halafu ukiwa unavnjari mitaani unakuwa unajikuna kwenye pumbu na kuvuta ndevu kila baada ya kama dakika mbili hivi huku ukisema kwa sauti isiyo ndogo "Mashaallah! Allah Akbar!" utadhani huna akili nzuri vile. Nadhani kwa staili hii hakuna hata Mmanga mmoja angethubutu kukusumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…