Nimenusurika kuchezea kichapo arabuni kwa kudhaniwa ni mmarekani!

Bado Niponipo

JF-Expert Member
Aug 15, 2008
680
195
Tatizo lako umezidisha swaga, hata jamaa pale Savanna Lounge na RG wanajua wewe mmatumbi..lol
 
babayah67

JF-Expert Member
Mar 28, 2008
493
195
Leo hii nimerejea nyumbani baada ya kuwa nimesafiri kwa muda kikazi katika nchi mojawapo ya kiarabu! Nilipokuwa huko kwa wiki moja nilidhani kama ni mwaka! Watu ni wa ajabu sana! Kuna siku moja nilitoka na mwenyeji wangu kwenda kupata chakula. Muuza chakula (kitaa) akaniuliza wewe ni muislam? nikasema hapana! Akaniuliza wewe ni mmarekani? (aliuliza akichanganya kiarabu na kizungu). Nikawa najiuliza ni kwanini ananiuliza hivyo? Kabla sijamjibu nikasikia akipiga kelele 'amerikani' (huyu ni mmarekani). umati wa watu waliokuwa karibu wakakanizunguka huku wakibwatuka eti 'wamarekani ni watu wabaya sana kwani wamemnyonga saddam hussein pia wanamtaka na osama bin laden'. Mwenyeji wangu ikabidi afanye kazi ya ziada kuwaelewesha kwamba mimi sio mmarekani. Walikubali tu baada ya kuwatolea hati yangu ya kusafiria (pasipoti).

***(nawasilisha)

Mhhhhh sidhani kama hao ulosema ni waarabu ni wajinga kiasi hicho wasiweze tofautisha kati ya Muamerika na mtu toka Africa. Kwanza umesema ulikuwa na mwenyeji wako, ilikuwaje wakakuuliza wewe usojua lugha ya kiarabu badala ya mwenyeji wako??? Hapa nanusa harufu fulani ya ***************.
 
Pape

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
5,501
0

did you smell a rat?
 
Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,690
2,000
Leo hii nimerejea nyumbani baada ya kuwa nimesafiri kwa muda kikazi katika nchi mojawapo ya kiarabu! Nilipokuwa huko kwa wiki moja nilidhani kama ni mwaka! Watu ni wa ajabu sana! Kuna siku moja nilitoka na mwenyeji wangu kwenda kupata chakula. Muuza chakula (kitaa) akaniuliza wewe ni muislam? nikasema hapana! Akaniuliza wewe ni mmarekani? (aliuliza akichanganya kiarabu na kizungu). Nikawa najiuliza ni kwanini ananiuliza hivyo? Kabla sijamjibu nikasikia akipiga kelele 'amerikani' (huyu ni mmarekani). umati wa watu waliokuwa karibu wakakanizunguka huku wakibwatuka eti 'wamarekani ni watu wabaya sana kwani wamemnyonga saddam hussein pia wanamtaka na osama bin laden'. Mwenyeji wangu ikabidi afanye kazi ya ziada kuwaelewesha kwamba mimi sio mmarekani. Walikubali tu baada ya kuwatolea hati yangu ya kusafiria (pasipoti).

***(nawasilisha)
Ni wapi huko i.e nchi gani?
 
Newvision

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
446
0
Unalosema ni kweli tupu hata mie nilishawahi kuulizwa na hao jamaa Emirates je we dini gani? Sasa kwani kuulizwa dini na si kitu kingine- of course inaeleweka!
 
bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
3,896
2,000
Kuna siku moja nilitoka na mwenyeji wangu kwenda kupata chakula. Muuza chakula (kitaa) akaniuliza wewe ni muislam? nikasema hapana! Akaniuliza wewe ni mmarekani? (aliuliza akichanganya kiarabu na kizungu). Nikawa najiuliza ni kwanini ananiuliza hivyo? Kabla sijamjibu nikasikia akipiga kelele 'amerikani' (huyu ni mmarekani). umati wa watu waliokuwa karibu wakakanizunguka huku wakibwatuka eti 'wamarekani ni watu wabaya sana kwani wamemnyonga saddam hussein pia wanamtaka na osama bin laden'. Mwenyeji wangu ikabidi afanye kazi ya ziada kuwaelewesha kwamba mimi sio mmarekani. Walikubali tu baada ya kuwatolea hati yangu ya kusafiria (pasipoti).

***(nawasilisha)

Hapo naona hiyo stori kidogo imechakachuliwa. Sasa wewe ulifahamu vipi kiarabu hicho kwa ghafla? Nao wamarekani huwafanyia hivyo hivyo waarabu wanaokwenda kwao.

Na hiyo pia sio ngeni kwani mimi mnamo mwaka 90 nilikwenda South Korea na kila nilipopita nilikuwa naitwa (kwa kejeli) ...... hey Americano!

Wanaamini Afrika ni nchi masikini sana na hawana uwezo wa kufika huko kwao.
 
Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,024

Silu moja nilikaa katika hoteli mji mmoja mdogo ujerumani. Asubuhi wakati na check out, nikamwambia yule dada pale checkout counter kuwa nahitaji taxi. Alivyokuwa anapiga simu kuita taxi, nilimsikia akimweleza taxi driver kuwa abiria atakayembeba ni Mmarekani. Hata mimi nilipata mawazo kuwa picha waliyozoea ya watu wenye rangi kama zetu ambao wanaoweza kukaa kwenye hoteli kama ile ni Wamerakani weusi tu na sio Waafrika. Nikamuona amepitwa na wakati na anahitaji darasa. Bahati mbaya kwake sikuwa na muda wa kutoa hilo darasa.
 
Mtabe

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
675
0
Kijana ah kumbe ni mzee! Usiseme uongo weye. Mmarekani hapigwi hivyo. Huoni kwenye tv jinsi wamarekani wanavyopigwa iraq,afghanistan, palestina etc. Inavyooneka labda walikufananisha kua ukibaka unataka kuwaibia inaingia akilini. Maana nyie si mnajulikana banaa si ndio mulioniibia simu yangu ktk daladala? Halafu pale taifa mukamnyan'ganya brother simu na hela.
 
MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,608
2,000
MOD hi Topic mimi kwa mawazo yangu naona bora uipeleke hapa ( Jokes/Utani + Udaku/Gossips) Kwa sababu hapa sipo mahali pake haingii akilini kuwa wewe uende Uarabuni kisha uwe na Mwenyeji wako kisha hao Waarabu waanze kukuliza Maswali uliwajibu kwa lugha gani Kiswahili au kiarabu? kwa sababu wewe hujuwi kiarabu uliwajibu kivipi? Hii ni Joke ingefaa MODERATOR Topic hii uihamishe iwe kule kwa ( Jokes/Utani + Udaku/Gossips) Samahani Mkuu MODERATOR sipendi kukuingilia kazi yako nakupa mawazo yangu asante.
 
Schmidt

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
5,347
2,000
Leo hii nimerejea nyumbani baada ya kuwa nimesafiri kwa muda kikazi katika nchi mojawapo ya kiarabu! Nilipokuwa huko kwa wiki moja nilidhani kama ni mwaka! Watu ni wa ajabu sana! Kuna siku moja nilitoka na mwenyeji wangu kwenda kupata chakula. Muuza chakula (kitaa) akaniuliza wewe ni muislam? nikasema hapana! Akaniuliza wewe ni mmarekani? (aliuliza akichanganya kiarabu na kizungu). Nikawa najiuliza ni kwanini ananiuliza hivyo? Kabla sijamjibu nikasikia akipiga kelele 'amerikani' (huyu ni mmarekani). umati wa watu waliokuwa karibu wakakanizunguka huku wakibwatuka eti 'wamarekani ni watu wabaya sana kwani wamemnyonga saddam hussein pia wanamtaka na osama bin laden'. Mwenyeji wangu ikabidi afanye kazi ya ziada kuwaelewesha kwamba mimi sio mmarekani. Walikubali tu baada ya kuwatolea hati yangu ya kusafiria (pasipoti).

***(nawasilisha)

Oyaa! Wewe ulichotakiwa kufanya Umangani ni kufuga madevu na kuvaa kanzu na bagharashia halafu ukiwa unavnjari mitaani unakuwa unajikuna kwenye pumbu na kuvuta ndevu kila baada ya kama dakika mbili hivi huku ukisema kwa sauti isiyo ndogo "Mashaallah! Allah Akbar!" utadhani huna akili nzuri vile. Nadhani kwa staili hii hakuna hata Mmanga mmoja angethubutu kukusumbua.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom