Nimenusurika kubambikiwa kesi ya mauaji leo kituo kikuu cha Polisi Dodoma

Leo nikiwa katika mihangaiko yangu ya kila siku muda wa SAA saba mchana nilipigiwa simu na jamaa yangu tuliyesoma nae shule ya upili rafiki yangu Huyu yeye ni Boda Boda na alikuwa akinijulisha kwamba mama yake ni mgonjwa hivyo nikaona ni vizuri nipite kumjulia hali akanielekeza sehemu anayo tafutia riziki nikaenda baada ya kufika tukawa tunapiga soga kidogo kabla hatujaelekea kwao kumuona mama yake Mara ghafla bin vuu tukajikuta tuko chini tumepigwa mitama na polisi Mara makofi bakora kibao ukiuliza kosa unapigwa vibaya mno tukakamatwa na wenzetu kama nane tukatiwa ndani ya gari (ashoki)huku tukiendelea kukanyagwa virungu vingi vikiendelea kutembea tulipofika kituoni tukaambiwa kuna mauaji yametokea mtaa wa pili Jana usiku SAA sita kwahiyo tunahitajika tutoe ushirikiano wa kupatikana kwa mtuhumiwa mmoja aliyehusika ambae anasemekana anakaa mitaa hiyo tulipofika kituoni tukachukuliwa maelezo tukaswekwa rumande tumekaa masaa sita tukiugulia maumivu huku kunguni, chawa, papasi wakiendelea kututafuna tunashukuru nguvu za ndugu na majirani kuandamana mpaka kituoni kutetea haki zetu tumekuja kutoka SAA moja na nusu usiku kwa utaratibu huu kweli jeshi la polisi liko kwa ajili ya kulinda usalama wa raia au kukandamiza na kudhalilisha raia tunashukuru tumetoka japo kuna wenzetu wamebaki inasikitisha sana

acha kelele hio ni mbinu ya kiupelelezi ulitaka ukamatwe kwa kubembelezwa wakati umekutwa eneo la tukio ukikutwa huna hatia utaachiwa tuu polisi sio vichaa kama ulivotaka kutuamaminisha.
 
Leo nikiwa katika mihangaiko yangu ya kila siku muda wa SAA saba mchana nilipigiwa simu na jamaa yangu tuliyesoma nae shule ya upili rafiki yangu Huyu yeye ni Boda Boda na alikuwa akinijulisha kwamba mama yake ni mgonjwa hivyo nikaona ni vizuri nipite kumjulia hali.

Akanielekeza sehemu anayo tafutia riziki nikaenda baada ya kufika tukawa tunapiga soga kidogo kabla hatujaelekea kwao kumuona mama yake.

Mara ghafla bin vuu tukajikuta tuko chini tumepigwa mitama na polisi Mara makofi bakora kibao ukiuliza kosa unapigwa vibaya mno tukakamatwa na wenzetu kama nane tukatiwa ndani ya gari (ashoki)huku tukiendelea kukanyagwa virungu vingi vikiendelea kutembea.

Tulipofika kituoni tukaambiwa kuna mauaji yametokea mtaa wa pili Jana usiku SAA sita kwahiyo tunahitajika tutoe ushirikiano wa kupatikana kwa mtuhumiwa mmoja aliyehusika ambae anasemekana anakaa mitaa hiyo.

Tulipofika kituoni tukachukuliwa maelezo tukaswekwa rumande tumekaa masaa sita tukiugulia maumivu huku kunguni, chawa, papasi wakiendelea kututafuna tunashukuru nguvu za ndugu na majirani kuandamana mpaka kituoni kutetea haki zetu tumekuja kutoka SAA moja na nusu usiku.

Kwa utaratibu huu kweli jeshi la polisi liko kwa ajili ya kulinda usalama wa raia au kukandamiza na kudhalilisha raia tunashukuru tumetoka japo kuna wenzetu wamebaki inasikitisha sana
Kuna baadhi ya wajinga hubeza njia ya maandamano katika kudai haki
 
acha kelele hio ni mbinu ya kiupelelezi ulitaka ukamatwe kwa kubembelezwa wakati umekutwa eneo la tukio ukikutwa huna hatia utaachiwa tuu polisi sio vichaa kama ulivotaka kutuamaminisha.
unaelewa ulicho andika??gorm 4 ulipata ngapi kabla ya kwenda depo??
 
acha kelele hio ni mbinu ya kiupelelezi ulitaka ukamatwe kwa kubembelezwa wakati umekutwa eneo la tukio ukikutwa huna hatia utaachiwa tuu polisi sio vichaa kama ulivotaka kutuamaminisha.

Je wewe ni mpumbafu mmojawapo wa hao Police? wapi imeandikwa au kuuidhinishwa kuwa upelelezi unafanywa kwa kumpiga mtuhumiwa? usifikiri kuwa mbinu za upelelezi ulisoma peke yako mkuu!
 
Leo nikiwa katika mihangaiko yangu ya kila siku muda wa SAA saba mchana nilipigiwa simu na jamaa yangu tuliyesoma nae shule ya upili rafiki yangu Huyu yeye ni Boda Boda na alikuwa akinijulisha kwamba mama yake ni mgonjwa hivyo nikaona ni vizuri nipite kumjulia hali.

Akanielekeza sehemu anayo tafutia riziki nikaenda baada ya kufika tukawa tunapiga soga kidogo kabla hatujaelekea kwao kumuona mama yake.

Mara ghafla bin vuu tukajikuta tuko chini tumepigwa mitama na polisi Mara makofi bakora kibao ukiuliza kosa unapigwa vibaya mno tukakamatwa na wenzetu kama nane tukatiwa ndani ya gari (ashoki)huku tukiendelea kukanyagwa virungu vingi vikiendelea kutembea.

Tulipofika kituoni tukaambiwa kuna mauaji yametokea mtaa wa pili Jana usiku SAA sita kwahiyo tunahitajika tutoe ushirikiano wa kupatikana kwa mtuhumiwa mmoja aliyehusika ambae anasemekana anakaa mitaa hiyo.

Tulipofika kituoni tukachukuliwa maelezo tukaswekwa rumande tumekaa masaa sita tukiugulia maumivu huku kunguni, chawa, papasi wakiendelea kututafuna tunashukuru nguvu za ndugu na majirani kuandamana mpaka kituoni kutetea haki zetu tumekuja kutoka SAA moja na nusu usiku.

Kwa utaratibu huu kweli jeshi la polisi liko kwa ajili ya kulinda usalama wa raia au kukandamiza na kudhalilisha raia tunashukuru tumetoka japo kuna wenzetu wamebaki inasikitisha sana
Kwa utaratibu huu kweli jeshi la polisi liko kwa ajili ya kulinda usalama wa raia au kukandamiza na kudhalilisha raia tunashukuru tumetoka japo kuna wenzetu wamebaki inasikitisha sana
 
Sababu ya wewe kuachiwa wameona haujashiriki kutenda kosa,shukuru Mungu waliokuhoji ni watumishi wenye akili timamu.Jela ni mbaya,Jela maisha mabovu,Jela ni maradhi Jela za Tanzania kama ukitoka huna Afya mbovu shukuru sana Mungu wako jitaidi kadri uwezavyo usiingie Jela.

Kile walichofanya Polisi kama hatua za haraka tu katika upelelezi ili kupata hata anayejua chochote juu ya mauaji hayo.Unajua inauma sana unaposikia mtu ameuawa na vibaka wakati wanamkaba na wameiba simu Tekno ya Tsh 30,000/= R.I.P aliyeuawa poleni wafiwa wote.Pole member wa Jf kwa misukosuko ya Kiupelelezi iliyokufanya usote mahabusu

Siku moja ukiwa na uchumi wenye nafuu kumbuka kuna watu wako Jela kwenye chumba kichafu hakuna maji wala godoro na chakula ni shida ,wachangie hata kwa kuwapulizia dawa kwenye chumba hicho au kiboresha chumba hicho bila kusahau hata chakula cha siku moja.

Kuna watu hawana ndugu wa kuweza kuwawekea dhamana ila wamekamatwa kwenye mazingira kama ulivyokamatwa wewe kosa linadhaminika ila hawana wadhamini.

Mwisho nafunga kwa kusema kuwa, walioko kwenye Mahabusu na Jela ni Binadamu kama sisi tuwaangalie kwa jicho la tatu.
 
acha kelele hio ni mbinu ya kiupelelezi ulitaka ukamatwe kwa kubembelezwa wakati umekutwa eneo la tukio ukikutwa huna hatia utaachiwa tuu polisi sio vichaa kama ulivotaka kutuamaminisha.
Umesoma vizuri tukio limetokea mtaa wa pili na tulipokamatwa si eneo la tukio
 
Kuto zingatia taratibu na majukumu ya kazi ndio kuna wafanya hawa ndugu zetu kutumia nguvu.

Kwa wenzetu ilipaswa ufungue shtaka la fidia,ila kibongo bongo hapo utazua tatizo baada ya kutatua tatizo.

Ila pole ndugu ndio mzunguko wa dunia huo.
 
Back
Top Bottom