Nimenunua umeme wa elfu 5 nikapata unit 1

Nimenunua umeme wa elfu 5 nikapata unit 1

inawezekana un deni mkuu kwa kuwa wateja wa tarif one unit moja ni tsh 292 tariff four unit moja ni tsh 100 kuanzia ya kwanza mpaka ya 75 ikizidi hapo inakuwa 350.tunaomba mita yako tukupatir majibu sahihi
 
wa 9000 ukaata unit 73 upo tarif four kila unit sh 100 ukizidi hapo yaani 75 utanunua kila unit 350
 
Nilinunua wa elf 40 nikapata unit 9. Nilipoenda tanesco wakasema mita ilikuwa na deni la elf 66 hivyo wanaendelea kukata.

Yaani Tanzania hii ni wizi. Nenda Tanesco watasema wanakudai. Mimi ilibidi polisi ndo waje kunitoa pale maana kidogo nipige mtu
 
Kama VAT ni 18%...sasa embu piga 0.18×5000
Mkuu elewa hivi, ukitoa 5000 kila mwanzo wa mwezi ndo hayo makato yanafayika, haijalishi umenunua umeme wa shiling ngapi. Ukitaka kununua umeme wa 4000 muamala unakataa. Ukiweka 5000 ndo wanakata hizo 4505 na zinazobaki wanakupa unit hizo kidogo.
 
hakuna makato ya service charge toka tarehe 1 april 2016 hivyo ukinunua umeme unakatwa VAT REA 3%NA EWURA 1%VINGINEVYO LABDA KAMA UNADENI LA NYUMA LIWE KWENYE LUKU.TUMA NAMBA YA MITA UTAELEZWA
 
Uliza kwenye ofisi za Tanesco,yawezekana una deni.
 
Andika mita namba yako hapa nikusaidie
 
Weka mita namba sasA nikupe jibu la kuridhishaaa
 
Mkuu si waliacha hizo tozo za kila mwezi?
Mimi umeme wa 5000 uwa napewa unit 45 na sikatwi hayo makato toka walipositisha.
Mbona unabahati sana yani umeme wa elfu 5 unapata unit 45 wakati mwenzio napata unit 14.5 na wa elfu 10 napata unit 28.9
 
Back
Top Bottom