Nimemwona mtu anachomolewa simu, nimwambie?

Nimemwona mtu anachomolewa simu, nimwambie?

kuntaitunai

Senior Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
106
Reaction score
193
Habari za mchana huu wana jamvi, mida hii kama dakika 20 hv zilizopita nikiwanatokea maeneo ya mlimani city katika public transport, daladala imesimama pale mwenge kama dakika 10 hv. So Kuna mdada alikuwa anakuijongelea gari ili apande akiwa anajiuliza apande gari gani huku simu akiwa ameiweka katika mashavu ya mfuko wa begi lake la mgongoni akatokea kupishana na huyo baharia. Huyo baharia alikuwa akipiga debe pale na akawa fasta ameiona ile simu katika begi lile so akaichukua kiulaini sana akaitia mfuko wa nyuma.

Baada ya kuchukua hiyo simu akaendelea kupiga debe baharia huyo ila nimemwona vividly kabisa with my naked eyes, pia kuna mdada alikuwa anakuja katika gari akaona hilo tukio so nimejiuliza sana nimwambie yule mdada or what. Baada ya kuassess faster pale nikaona impact ya maisha ya huyo baharia yatakuwa matatani na pia yule mdada kwann akaweke simu open mazingira kama yale pale, na baada ya kumuona yule mdada aliyeshuhudia pia tukio hajasema chochote, nami ikabidi tu nikae kimya japo roho imeniuma kwekweli ndo maana nikaja kwa wanajamvi humu.

Tupeane ushauri kwa sabb najua wengi wame experience hii kitu je inatakiwa tureact vipi kiasi kwamba hatuwezi leta madhara kwa pande zote mbili.

Sent using Ubuntu
 
Kuna wakati nawachukia sana wale wenye msemo wa 'Wanaume wa Dar' ila kuna wakati naona wako sahihi.

Angekuwa dadako wa Damu ungekaa kimya? Angekuea mpenzi wako ungekaa kimya? Angekuwa mamako mzazi ingekuwaje?

Changes katika jamii huanza na wewe mwenyewe ili tukomeshe tabia hii kila jamii iwajibike.

Kesho hujui atamuibia nani tena, ulipaswa kusaidia ili wote wawili wajifunze aache wizi na mwingine awe makini.

Sent using Nokia ya tochi
 
Umenena vyema mkuu japo sidhani kama neno la mwanaume wa Dar limetumika kisahihi.
Anyways Asante kwa comment otherwise nimejifunza kwa namna moja ama nyingine.

Sent using Ubuntu
 
Bwanamdogo kapima MARINDA possibly ulibakwa ukiwa umepigwa Nusu Kaputi

Sent from my Huawei Mate X using Tapatalk
 
Kwann hujamsaidia huyo Dada hata Kama msaada sio sheria..
Et kwasabbu Yule mwanamke mwenzake alinyamaza na wewe ndo unyanmaze na wew Ni mwanamke mwenzake?? Kuibiwa kunauma Sana
Najifunza mkuu

Sent using Ubuntu
 
Hii dhambi imetendeka mbele ya macho yako (you saw vividly with your own eyes) yet hakuchukua hatua yoyote, wallahi Mungu atakuhukumu kwa hili... Adhabu ya kwanza wiki hii kabla haijaisha utaibiwa hiyo simu yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ungemuona dada yako anapigwa "makofi" kwenye miti na wahuni ungenyamaza?
Next time nikileta uzi wa kukabiliana na muhalifu wa aina hyo naomba usisite kuja mkuu. Naendelea kusisitiza najifunza mkuu.

Sent using Ubuntu
 
Hii dhambi imetendeka mbele ya macho yako (you saw vividly with your own eyes) yet hakuchukua hatua yoyote, wallahi Mungu atakuhukumu kwa hili... Adhabu ya kwanza wiki hii kabla haijaisha utaibiwa hiyo simu yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwakweli mkuu lakini I choose not to. Kwasbb maisha haya ni full of choices kwahvyo najifunza pia kupitia choice hii ambayo imeonekana ni mbovu kwa wengi.

Sent using Ubuntu
 
Next time nikileta uzi wa kukabiliana na muhalifu wa aina hyo naomba usisite kuja mkuu. Naendelea kusisitiza najifunza mkuu.
Sent using Ubuntu
Sijakuambia ukayatafute majanga na wahuni halafu wakukoyonge hadi wakuvunje mbavu.Kila jambo utumie akili zaidi.
 
Back
Top Bottom