Sinai
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 288
- 47
Habari wana JF! Mimi ni mwanaume, nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi (mchumba na mali nimetoa kwao) na mdada mmoja hivi kwa muda wa miaka mitatu sasa, yeye ni mwanachuo hapo UDSM na kwa sasa ndo anamalizia degree yake. Last weekend niliamua kumtembelea huko hostel kwake bila kumjulisha, ilikuwa jumamosi nikiwa na lengo la kwenda kumchukua ili tutoke kidogo! Cha ajabu huyo binti sikumkuta, nilipo jaribu kumuuliza mwenzake anaeishi nae chumba kimoja kasema aliondoka tangu jana yake jioni (ijumaa) na hakurudi hadi mida ya saa 10 jioni ambayo mimi nilipofika pale! Nikaamua kumpigia simu, kwavile yeye alikuwa hajui kama mimi nipo pale hostel, akawa ananidanganya eti yupo hostel na tena ameboreka sana, analalamika eti nimemtosa hata simu kutwa nzima sijampigia na mambo mengi! Mimi niliamua kuondoka huku nikiwa nimekasirika sana bila kumwambia kama mimi nimefika pale hostel! Jumapili aliporudi hostel akaambiwa kuwa mimi nilifika na nilimpigia simu nikiwa pale, binti amechanganyikiwa, analia hovyo na anaomba msamaha, tena amemwambia hadi mama yake na dada yake, leo jioni dada yake anataka kuonana na mimi, wadau mnanishaurije? Nimpotezee huyu dada? Kwani mimi nimesha amua kumwacha kabisaa huyo binti, na mali niliyotoa kwao nipo tayari kusamehe!