Nimemwaga mboga...lakini nafsi inanisuta.

Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,552
2,337
Jana nilifanya kitu kinacho ninyima raha sana, stori yenyewe ipo hivi.

Kuna msichana tuliwahi kuwa na uhusiano zamani kabla sijaoa na yeye kuolewa, kwa sasa anafanya kazi RITA. Kutokana na uhusiano mzuri tuliokuwa nao na pia tuliachana kwa roho safi kabisa kwa kuwa wote tulijua hatukua chaguo sahihi la kuishi hadi kifo kitakapo tutenganisha mimi na yeye bado tunawasiliana inapobidi. Mwezi uliopita nilikuwa nataka cheti cha kuzaliwa cha binti yangu kwa haraka nilipoenda pale RITA wakanizungusha wee hadi nikaamua kumtumia huyu dada ambaye ni X wangu.

Sasa nadhani wiki hizo mawasiliano yaliongezeka kidogo hasa kuhusu cheti cha binti yangu,mume wa huyu dada akaanza visa ikiwa ni pamoja na kumpigia simu mke wangu akimuambia anionye kuhusu mke wake. Mke wangu nili muelewesha lakini pia na yule dada nikamuambia aongee na mume wake. Yule mume wake akaona atumie nafasi hii kuniabisha, basi jana tukapanga tukae mimi mke wangu na yeye na mke wake tuweze ku clear hii issue. Tulipopanga kukutana kwa mstuko jamaa alikuja na mke wake lakini pia alikuja na jamaa zake ambao wengine mimi ninafanya nao kazi akilazimisha tuongee mbele yao. Kuona hivyo nikajua lengo lake lilikuwa kuniaibisha ndipo nikamstua wife aondoke.

Wife alipoondoka nikawaambia nipo tayari kwa mazungumzo ndipo jamaa kwa makeke akaniuliza kwa nini nawasiliana sana na mkewe, nilimuambia kuwa nilikuwa nimegundua nimeambukizwa ugonjwa wa zinaa na kwa kuwa pia nilikuwa nimetembea na mkewe basi tulikuwa tumeanza matibabu pamoja Marie stopes. Jamaa aliishiwa nguvu na kuondoka kwa hasira kubwa, mke wake naye aliishia kunimwagia maji na kuondoka. Sijui nini kimeendelea kwenye familia yao lakini sasa hivi najisikia vibaya mno. Hebu nisaidieni ni jinsi gani nitaweza kurudisha amani kwenye hii familia maana si kweli kama nimetembea na huyu msicha ila nilitaka ku get back kwa kutaka kunidhalilisha.
 
NYENJENKURU

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
1,036
247
Wewe ni mgombanishi.Ulitakiwa umweleze jaama maneno yalyale ya kwamba alikuwa nakusaidia kutafuta cheti cha mwanao cha kuzaliwa na si vinginevyo.Sasa umetoka nje ya mada na kumuonyesha kuwa umedu na mke wake ndo maana umepata gonjwa la zinaa
 
Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,351
11,577
nduka nduka nduka jamani una kichaa? aaah iyo sumu uliyomwaga kama ni kweli sijui
 
IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,375
6,996
Ingawa huyu bwana wa huyo ex-girl friend wako amefanya upuuzi-lakn wewe umefanya upuuzi zaidi,...samahani kwa kutumia lugha kali ni kama nimeghafirika na kitendo alichofanya huyu jamaa..uuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuh
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
45,218
95,800
Namuonea huruma huyo mwanamke
anaonesha hajui to pick the right guys for her..

Mumewe ni mshamba kwa kuita watu kuja kuongea hiyo ishu..

Na wewe nae umemfanya ajute kwa kukusaidia.....
 
IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,375
6,996
Namuonea huruma huyo mwanamke
anaonesha hajui to pick the right guys for her..

Mumewe ni mshamba kwa kuita watu kuja kuongea hiyo ishu..

Na wewe nae umemfanya ajute kwa kukusaidia.....

Naunga mkono hoja,...sijui kuleta watu ndio ilikua inamaanisha nini,..ona sasa kaondoka kaelemewa na mawazo....na hapo ndio wahenga wanaposema ndoa ndoano,...i will see siku nikioa
 
Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,552
2,337
Ingawa huyu bwana wa huyo ex-girl friend wako amefanya upuuzi-lakn wewe umefanya upuuzi zaidi,...samahani kwa kutumia lugha kali ni kama nimeghafirika na kitendo alichofanya huyu jamaa..uuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuh

Mkuu hakuna cha samahani, na mimi sasa baada ya kurudi kwenye sense naamini nilifanya upuuzi mkubwa sana, natamani kuyameza maneno yangu lakini hiyo damage sijui kama naweza kuiondoa.
 
IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,375
6,996
Mkuu hakuna cha samahani, na mimi sasa baada ya kurudi kwenye sense naamini nilifanya upuuzi mkubwa sana, natamani kuyameza maneno yangu lakini hiyo damage sijui kama naweza kuiondoa.

sawa sawa,...una roho ya kibinadamu haswa,...thats very good,..kukiri kosa ni dalili ya uungwana kiongozi wangu
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,772
23,076
maskini dada wa watu. . .

Anyway waweza mpigia mume wa x ukamwelewesha. . Cjui atakuelewa?
 
Nailyne

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
350
111
Naunga mkono hoja,...sijui kuleta watu ndio ilikua inamaanisha nini,..ona sasa kaondoka kaelemewa na mawazo....na hapo ndio wahenga wanaposema ndoa ndoano,...i will see siku nikioa

hapo kwenye bold hapo....kuwa uyaone
 
Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,552
2,337
maskini dada wa watu. . .

Anyway waweza mpigia mume wa x ukamwelewesha. . Cjui atakuelewa?

Mkuu huo ujasiri wa kuanza kumpigia ndio sina, na bora ningejua nini kiliendelea kwao ila hata wale jamaa aliokuja nao hawajamuona tangu jana wala mkewe hajaonekana kazini leo.

Ni vizuri always kuwa muungwana hata kama unashambuliwa na watu wa ajabu..

Mkuu, nipo kwenye darasa la anger management kwa mwezi wa nne hivi sasa, sijui kama ninafanya vizuri kwenye hii kitu.
 
Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,435
Jana nilifanya kitu kinacho ninyima raha sana, stori yenyewe ipo hivi.

Kuna msichana tuliwahi kuwa na uhusiano zamani kabla sijaoa na yeye kuolewa, kwa sasa anafanya kazi RITA. Kutokana na uhusiano mzuri tuliokuwa nao na pia tuliachana kwa roho safi kabisa kwa kuwa wote tulijua hatukua chaguo sahihi la kuishi hadi kifo kitakapo tutenganisha mimi na yeye bado tunawasiliana inapobidi. Mwezi uliopita nilikuwa nataka cheti cha kuzaliwa cha binti yangu kwa haraka nilipoenda pale RITA wakanizungusha wee hadi nikaamua kumtumia huyu dada ambaye ni X wangu.

Sasa nadhani wiki hizo mawasiliano yaliongezeka kidogo hasa kuhusu cheti cha binti yangu,mume wa huyu dada akaanza visa ikiwa ni pamoja na kumpigia simu mke wangu akimuambia anionye kuhusu mke wake. Mke wangu nili muelewesha lakini pia na yule dada nikamuambia aongee na mume wake. Yule mume wake akaona atumie nafasi hii kuniabisha, basi jana tukapanga tukae mimi mke wangu na yeye na mke wake tuweze ku clear hii issue. Tulipopanga kukutana kwa mstuko jamaa alikuja na mke wake lakini pia alikuja na jamaa zake ambao wengine mimi ninafanya nao kazi akilazimisha tuongee mbele yao. Kuona hivyo nikajua lengo lake lilikuwa kuniaibisha ndipo nikamstua wife aondoke.

Wife alipoondoka nikawaambia nipo tayari kwa mazungumzo ndipo jamaa kwa makeke akaniuliza kwa nini nawasiliana sana na mkewe, nilimuambia kuwa nilikuwa nimegundua nimeambukizwa ugonjwa wa zinaa na kwa kuwa pia nilikuwa nimetembea na mkewe basi tulikuwa tumeanza matibabu pamoja Marie stopes. Jamaa aliishiwa nguvu na kuondoka kwa hasira kubwa, mke wake naye aliishia kunimwagia maji na kuondoka. Sijui nini kimeendelea kwenye familia yao lakini sasa hivi najisikia vibaya mno. Hebu nisaidieni ni jinsi gani nitaweza kurudisha amani kwenye hii familia maana si kweli kama nimetembea na huyu msicha ila nilitaka ku get back kwa kutaka kunidhalilisha.
Kwa hiyo Nduka unataka kuniambia una mke na watoto?
 
dmaujanja1

JF-Expert Member
Nov 24, 2008
223
67
Ama kweli kuishi kwingi kuona na kusikia mengi. Ur animal ! Fanya liwalo uirudishe family ya mshikaji ktk amani la sivyo God will never 4gv u 4this.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom