Nduka
JF-Expert Member
- Dec 3, 2008
- 8,552
- 2,360
Jana nilifanya kitu kinacho ninyima raha sana, stori yenyewe ipo hivi.
Kuna msichana tuliwahi kuwa na uhusiano zamani kabla sijaoa na yeye kuolewa, kwa sasa anafanya kazi RITA. Kutokana na uhusiano mzuri tuliokuwa nao na pia tuliachana kwa roho safi kabisa kwa kuwa wote tulijua hatukua chaguo sahihi la kuishi hadi kifo kitakapo tutenganisha mimi na yeye bado tunawasiliana inapobidi. Mwezi uliopita nilikuwa nataka cheti cha kuzaliwa cha binti yangu kwa haraka nilipoenda pale RITA wakanizungusha wee hadi nikaamua kumtumia huyu dada ambaye ni X wangu.
Sasa nadhani wiki hizo mawasiliano yaliongezeka kidogo hasa kuhusu cheti cha binti yangu,mume wa huyu dada akaanza visa ikiwa ni pamoja na kumpigia simu mke wangu akimuambia anionye kuhusu mke wake. Mke wangu nili muelewesha lakini pia na yule dada nikamuambia aongee na mume wake. Yule mume wake akaona atumie nafasi hii kuniabisha, basi jana tukapanga tukae mimi mke wangu na yeye na mke wake tuweze ku clear hii issue. Tulipopanga kukutana kwa mstuko jamaa alikuja na mke wake lakini pia alikuja na jamaa zake ambao wengine mimi ninafanya nao kazi akilazimisha tuongee mbele yao. Kuona hivyo nikajua lengo lake lilikuwa kuniaibisha ndipo nikamstua wife aondoke.
Wife alipoondoka nikawaambia nipo tayari kwa mazungumzo ndipo jamaa kwa makeke akaniuliza kwa nini nawasiliana sana na mkewe, nilimuambia kuwa nilikuwa nimegundua nimeambukizwa ugonjwa wa zinaa na kwa kuwa pia nilikuwa nimetembea na mkewe basi tulikuwa tumeanza matibabu pamoja Marie stopes. Jamaa aliishiwa nguvu na kuondoka kwa hasira kubwa, mke wake naye aliishia kunimwagia maji na kuondoka. Sijui nini kimeendelea kwenye familia yao lakini sasa hivi najisikia vibaya mno. Hebu nisaidieni ni jinsi gani nitaweza kurudisha amani kwenye hii familia maana si kweli kama nimetembea na huyu msicha ila nilitaka ku get back kwa kutaka kunidhalilisha.