Nimemwadhibu dada wa kazi, majirani wanaingilia

jembelamkono

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
2,733
2,011
Habari zenu wakuu,

Kufwatia mwenendo mbovu wa dada yetu wa kazi jana nikiwa nimeshinda muda mwingi nyumbani nilijikuta nimepatwa na hasira nikaamua kumwadhibu.

Kwa siku za hivi karibuni amekua mvivu kupindukia,kazi hafanyi,usafi wa nyumba ndio kabisa,nguo anafua siku akitaka n.k.

Huyu dada nililetewa na mama mkwe wangu kutoka Mbeya,hata hivyo huyu mama mkwe aliwahi kumkanya sana abadilike hasa ukizingatia ametokea kwenye familia duni sana,hivyo hana budi kuwa mtii ili asiharibu future yake baadae.

Kwa muda mrefu nimekua nikimsikia wife anamgombeza na hata kumpiga na mwiko,tatizo ikiwa ni tabia yake ya uchafu na uvivu kupindukia.Just imagine tumeishi nae kwa kipindi cha miezi 6 lakini hata kupika wali au ugali hajui.

Sasa jana nilimpa kazi ya kufuta madirisha ya sebuleni mimi kama baba,baada ya kuona ni machafu sana vumbi na buibui vimetenda,japo nimekuwa nikilirudiarudia kuwaambia hilo swala lakini hawalitekelezi.

Ilimchukua zaidi ya nusu saa kutafuta maji na kitambaa ilikuanza kuyafuta,nikasema ninyanyuke nikamwangalie anafanya nini labda pengine kazi zimemzidi sisi hatujui (japo wapo wawili) kufika namkuta anachezea simu.

Nikamyang'anya simu ambayo hata hivyo niilimnunulia mimi,akawa hataki anaing'ang'ania,nilimpiga kibao kimoja akaiachia nikampa wife aikague,
balaa utitiri wa wanaume anaowasiliana nao,tena yeye ndie anawapigia au kuwa text.

Wife akampigia mmoja na ile simu ya binti wa kazi akajifanya ndie binti, jamaa likaanza kutiririka ukweli wote,basi tukagundua kumbe ni jamaa yake.

Nilikasirika,nilimpakichapo heavy,wife nae akamwongeza kisawasawa,huku tukimkanya tabia ile na madhara yake.

Leo nimerudi nyumbani mchana gafla bila ya wao kujua,nikasikia wanahadisiana issue ya jana huku wanamsema wife,yule mwingine anamwambia mwenzake "ningefurahi kama dada angechambwa na yule jamaa" anaendelea "ingekua ni jamaa yangu Amiri angemtukana kisawasawa".

Nikaingia ndani nikawauliza mnasemaje? Rudieni kusema yote mliyosema, wakasema baadhi na mengind wakamezea.Bahati mbaya nlikua naharaka nikaondoka zangu.

Sasa mchana huu wife kapigiwa simu na mwenyekiti serikalii za mitaa kwamba mimi na yeye jioni tunahitajika ofisini kwake.

Sijajua anachotaka kusema,lakini nilivyousoma mchezo kama majirani wanawapa kiburi wasichana wangu wa kazi,hasa pia ukizingatia ninapoishi kidogo Mungu kanijalia hali yangu iko vizuri ukilinganisha na majirani'zangu.

Pia ninapoishi nimezungukwa na waswahili kwelikweli,wengi hawana kazi,wanashinda vibarazani muda mwingi naona hii inachangia sana kupiga umbea na hawa dada wa kazi..i

Nimenuia kufanya mbaya hapo serikali za mtaa endapo wataniuliza na kuingilia uhuru wangu wa kuwaadhibu watoto wangu ninao ishi nao.

Naombeni mawazoyenu wenye uzoefu na mambo haya tafadhali.
 
Sina hakika kama unatumia busara sana katika maamuzi unayofanya, mimi nimewarudisha kwao wadada wa kaz watano had sasa lakin sijawah kuwapiga wala kujibizana nao. Kupiga kuna madhara mengi kuliko faida, mtu anayeishi na familia yako na anawaandalia chakula si vizur kuish naye kibabe utakula had mavi au sumu, nakushaur ukiwa na bint wa kazi akikosea muonye kama haelewi mrudishe kwao. Na kwa hali uliyonayo sasa ukimaliza ilo swala huko serikali za mitaa mrudishe huyo bint kwao.

Duc in Altum
 
Mbaba mtu mzima na madevu yako unampiga msichana wa kazi..... hizo nguvu si ungetumia kukima mchicha familia yako ikala mboga bora?

Huyo msichana kama hakuridhishi na utendaji wake si umrudishe kwao? Dhiki na umasikini wake sio sababu ya kumpiga. Kumbuka bila kuja umri huyo binti hapo ni kazini....aadhibiwe kikazi na sio kupiga.

Na mkeo kakusapoti kumpiga?

Hivi mkimpiga akaanguka na kuwafia mngesemaje? Hao majirani unaowaona waswahili kesho na keshokutwa ndio watakaotoa ushahidi wa "vipigo" juu ya msichana wako

Narudia binti haridhishi mrudishe kwao

Na mngekuwa na nia ya dhati kwa nini msingekaa chini na binti mkamwelezA madhara ya ngono na wanaume lukuki?

Keshona keshokutwa akiwadhuru wanao na kusepa mtafanyaje???? Msizoee kupiga piga watoto wa watu hovyo


Anyway.... nilidhani usafi na shughuli za nyumba husimamiwa na mke..........
 
....Huyu dada nililetewa na mama mkwe wangu kutoka mbeya,hata hivyo huyu mama mkwe aliwahi kumkanya sana abadilike hasa ukizingatia ametokea kwenye familia duni sana,hivyo hana budi kuwa mtii ili asiharibu future yake baadae.

....Nimenuia kufanya mbaya hapo serikali za mtaa endapo wataniuliza na kuingilia uhuru wangu wa kuwaadhibu watoto wangu ninao ishi nao

  • Hapo kwenye green sipasemei watakuja wenyewe sijui lengo lilikuwa nini kupataja...
  • ....ukizingatia ametokea kwenye familia duni sana..
    • Nadhani huo uduni wa familia aliyotoka hakujitakia yawezekana ni mwendelezo wa makosa waliyofanya watangulizi wake, maisha hubadilika ipo siku naye atakuwa wa aina tofauti mchukulie kwa upole...
  • ....Nimenuia kufanya mbaya hapo serikali za mtaa..
    • Nashauri usidhamirie kuwa na jazba ili majadiliano yawe yenye tija badala ya mifarakano jitahidi kuwa mtulivu ili nao wasipate sababu ya kuwa umeidharau serikali yao...
  • ....uhuru wangu wa kuwaadhibu watoto wangu ninao ishi nao
    • hapa umemwajiri mtoto, nadhani kisheria hupaswi kuajiri under 18s, anyway wataalamu watakuja na vifungu vyao...
 
J333 sijakuelewa,,umerudisha wadada wa tatu,,mimi nimelipa elf themanini,nauli kaja,,mwezi wa kwanza yuko vizuri,,nao kabadilika sana,,nguo za mtoto ziko nje chafu zimetupwa tupwa,, akiamka asbh anakaa tuu hafanyi kitu chochote,,,ndani kuchafu,,muda . mWingi simu ni text tuu,,unampa maagizo hayatekelezi,,hasiea kaka hakuna anaependa kupiga,,hata kupiga mke hakuna . ANaependa,,,
 
Unayofanya si sawa. Lazima utofautishe kati ya:- i. mtoto wako wa kuzaa (biological child), ii. mtoto wa ndugu unayemlea (non-bilogical child) na iii. mfanyakazi wako wa ndani. Usipovitenganisha jua kuwa utapata shida. Kumbuka kama mtoto sio biological child wako; ukimkanya na asikusikilize ACHANA NAYE kwani ana wazazi wake. Ushauri, nenda serikali za mitaa uombe msamaha kwa kosa ulotenda bila kukusudia.
 
J333 sijakuelewa,,umerudisha wadada wa tatu,,mimi nimelipa elf themanini,nauli kaja,,mwezi wa kwanza yuko vizuri,,nao kabadilika sana,,nguo za mtoto ziko nje chafu zimetupwa tupwa,, akiamka asbh anakaa tuu hafanyi kitu chochote,,,ndani kuchafu,,muda . mWingi simu ni text tuu,,unampa maagizo hayatekelezi,,hasiea kaka hakuna anaependa kupiga,,hata kupiga mke hakuna . ANaependa,,,
Acha hizo huyo si mtoto wako na hulazimishi kumwajiri. Tafuta mwingine. Aidha kumbuka yeye ni msaidizi tu. Kazi ya kulea, kusafisa nyumba etc ni za baba na mama wa nyumba wao ni wasaidizi.
 
umempa kichapo cha maana kama haitoshi mkeo nae akaja akamuongezea pia mkeo huwaga anampigaga had na mwiko. Duuuuh hv mshahara unamlipa shiling ngap?? ni kweli kakosea na kakuudhi ila kumshushia kichapo tena cha mbwamwizi sio vema Kama kakushinda mrejeshe kwao Maana kwa maelezo yako inaonekana huyo bint hajazoea mazingira ya kutumikishwa na hii ndio sababu hata kupika hawez
 
Mpige mtu ambaye angalau una historia yake ya kiafya.
Pili mtu kama huyo ambaye c ndugu yako ambaye anafanya kazi nyeti sana za ndan kwako unajiatarisha kuishi nae kibabe.
Kama una mtoto mchanga ipo cku utamkuta kwenye freezer au kamnyonga na kutoweka au achome nyumba na kutoweka.
Mtoto wa kazi hapigwi kama hajui mfundishe akishindwa atakuwa hakufai mrudishe kwao.
Hao majirani watamjaza ukatili atakaokuja kukufanyia ambao hutakaa umsahau.
 
Huoni hata aibu kabisaaa eti nikampa kichapo na wife nae kampa kichapo,ww na mkeo hamna roho ya ubinadam kabsaaa,kila mtu na mazingira alolelewa mlipaswa mkae nae chini kwanza mmweleze maisha n nn na anatakiwa aishije, na mkaongea nae km ndgu yako tu,unadhan kumpiga ndo kumrekebisha? Pia hata mkeo na yy n mvivu tu kwann kazi zingine asifanye yy km yy, hadi madirisha yanajaa vumbi na buibui ndani ina maana mkeo haangaliagi nyumba yake?
 
Hali yako nzuri,,,unaishi uswahilini,,,nasikitika hausi girl ulimwadhibu Kwa kushindwa kusafisha uchafu wa wigo wa buibui,,,Weka Madirisha ya aluminium na vioo,,,napita tyuu
 
Hawa wadada wa kazi ni jipu linaloishi majumbani mwetu...INAHITAJI Busara sana kulitumbua. Kwangu yupo mmoja kati ya wawili anahitaji kuondolewa. Ila pia kinachochangia ni umri...IMEFIKA Pahala mdada wa kazi chini ya 25yrs simuhitaji hata kidogo....PIA Ulimbukeni wa mambo ya mjini kwao unawasumbua kwelikweli....YANI Ni pasua kichwa.

Kupiga kwa kweli itokee pale unaposhindwa ku-control hasira kutokana na madhila yao ila sio jambo jema na la kuendekeza...NAONA Mleta mada ulipitiliza hasa ukichukulia kila siku unawapiga mpaka na wife anawapiga kwa miko.

Wazo zuri ni kila siku uwe unawasiliana na waleta wafanyakazi...HAKIKISHA Mwezi ukiisha na yeye anasepa..AKIONYESHA Ubora atakaa miezi miwili kila mwezi uwe ni assesment kwa utendaji wake...LA Sivyo anasepa unaagiza mwengine.
 
Hali yako nzuri,,,unaishi uswahilini,,,nasikitika hausi girl ulimwadhibu Kwa kushindwa kusafisha uchafu wa wigo wa buibui,,,Weka Madirisha ya aluminium na vioo,,,napita tyuu

Madirisha ya aluminum na vioo bado sio moja kati ya vigezo vya hali nzuri ya mleta mada....USWAHILINI Hali nzuri ni relative to majirani zako...UKILA Mboga mbili hadi tatu wewe uko vizuri, ukipiga rakaa 3 uko njema maana wenzako wote ni rakaa 1 au hata kupita kimya.

Na kwa laifu ya uswazi kwetu kuwa na beki 3 wawili nayo ni hali nzuri, hata nyumba yenye madirisha bado ni hali nzuri...HIYO Inamaanisha ni nyumba kubwa na madirisha yako wazi hewa ya kumwaga...SIO Kwetu na mie makabati yameziba madirisha utayasafisha na nini?

Kiufupi tuheshimu kuwa vizuri kwa mleta mada aishie uswahilini...
 
J333 sijakuelewa,,umerudisha wadada wa tatu,,mimi nimelipa elf themanini,nauli kaja,,mwezi wa kwanza yuko vizuri,,nao kabadilika sana,,nguo za mtoto ziko nje chafu zimetupwa tupwa,, akiamka asbh anakaa tuu hafanyi kitu chochote,,,ndani kuchafu,,muda . mWingi simu ni text tuu,,unampa maagizo hayatekelezi,,hasiea kaka hakuna anaependa kupiga,,hata kupiga mke hakuna . ANaependa,,,
Unaionea uchungu 80000 ila kama hutaki kusikiliza ushauri utapata hasara au matatizo mara 100 ya hiyo 80000. Mimi nililetewa bint kutoka Kyela baada ya week mbili nikagundua hampend mwanagu nikamrejesha kwao tena kwa kumpa tena nauli plus mshahara wa mwez mmoja.

Duc in Altum
 
Back
Top Bottom