Nimemtongoza jana, leo anataka nimtumie hela

Nimemtongoza jana, leo anataka nimtumie hela

kende

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2013
Posts
3,527
Reaction score
1,671
Kuna msichana niliwahi kuonana nae mara1 ni rafiki wa dadaangu, tulionana nilipoenda kumtembelea sista nikahisi kumpenda, jumapili kulikuwa na event ya kifamilia nikaonana naye, safari hii nikawa siriaz kumbana nimsomeshe hadi kieleweke.

Bahati nzuri tulipotoka kwenye event tulisafiri pamoja nikakaa naye kwenye siti zinazofatana, nilimtongoza though hakunipa jibu la moja kwa moja kunikubalia but alikuwa anaonyesha kuelekea kukubali, nilimwomba namba yake akanipa. Kesho yake ambayo ni jana akanichokoza kupitia msg, akanisalimia nami nikarespond.

Si nikahisi mtoto kashakolea, ile nataka nianze kumchokoza anipe jibu langu mara akatuma meseji 'Nasikia njaa', duh ile kuendelea kuchat nikagundua anamaanisha nimtumie hela. Eti ndugu wananchi, huyu ni wife material kweli au najiingiza kwenye majanga? Maana mtu mwenyewe hela za kuokoteza.
 
Sometimes wife material wanatengenezwa after marriage...
so kamaumempenda kweli muoe halafu anza kumpa dos and donts...

but kama ana njaa na hana pa kula....alikuwa anaishi vipi before you?
na waliokuwa wanamsaidia njaa yake aliwalipa nini?
 
Kwani kusema nasikia njaa manake nipe hela eeh? hii ndio style mpya yakuomba hela?
au unataka kujipendekeza kuanza kumpaa hela eeh?
 
Kwani kusema nasikia njaa manake nipe hela eeh? hii ndio style mpya yakuomba hela?
au unataka kujipendekeza kuanza kumpaa hela eeh?

Ndo kibomu hicho we unadhan mdada anakwambia anasikia njaa ndo utaenda kumsongea ugali na matembele?
Hahaha yaani unatakiwa kuingia mfukoni au mpesa/tigo pesa itakuhusu
 
Hahahaaaaa iyo ni money material....mpe pengine anakupima tuuu usijishauri kama kweli unampenda
 
Mambo mengine mnajiumiza kichwa tu, mtu kakwambia nasikia njaa, si umwambie akale.. kwani umemkataza...?

Mi mwenyewe ndo naona lilikua jibu la kumpa.hahha.kucomplicate tuu mambo.mtu unamwambia kale nakusubiri.kama kuna jingine atajiongeza.apo kavile naona kammisinterprete
 
Hapo ndio Mwanzo, anaanza na vibomu vidogodogo baadae utaombwa big money, kazi kwako
 
  • Thanks
Reactions: amu
Sio wewe tu mkuu hata mimi hao mie nimekutana nao sana ila mie wangu huwa hawasingizii njaa, nimetoka kumtongoza jana jioni amekubali kila kitu. Asubuhi unaamka una furaha kuwa nimepata kifaa kipya,

unajichanganya kumsalimia kwa msg eti unajifanya unajali sana, anakuja bby leo nimeamka vibaya naskia homa nahisi malaria nataka niende hospital, unamjibu poa nenda bby,

atakuambia sina hela kabisa nisaidie hata elfu 20 nikapime na kununua dawa. Nimekutana nao hawa kama 6 hivi mpka leo najiuliza ina maana nina mkosi kupata wa wagonjwa wa malaria wa gafla ?. mjini hapa unatakiwa uwe mjanja
 
Sometimes wife material wanatengenezwa after marriage...
so kamaumempenda kweli muoe halafu anza kumpa dos and donts...

but kama ana njaa na hana pa kula....alikuwa anaishi vipi before you?
na waliokuwa wanamsaidia njaa yake aliwalipa nini?

kaaz kwelkwel, sikutegemea vibomu kama vinaweza kuanza mapema hivi
 
Hahahahaha nasikia njaa nishakutana nao sana hao,.. Unamtongoza kakataa lakn anaomba hela

Halafu hapo mzee mzima huna kitu mwisho wa mwezi kama hivi unajihisi kukonda ghafla
 
Back
Top Bottom