Nimemtembelea Mjane Wa Daud Mwangosi...

Inatia huruma sana, na kwa kweli huwa sielewi hizi siasa za namna hii zinania ya kutuletea nini zaidi ya hizi huzuni kwa watu wasio na hatia.
 
Mungu akubariki Maggid kwa kuwa jirani mwema angalau huyu mama kwa kupitia wewe anaweza akawasogeza watoto ukienda tena mpe pole zetu
 
Ni muhimu sana Ndugu Mjengwa uisaidie hiyo familia kutafuta wakili wa kuwasaidia kufungua kesi ya madai dhidi ya Polisi na Serikali ya Tanzania. They should sue the state (whose agents the Police are,) for at least two billion shillings.

Sidhani watoto wao wataweza kufanya mitihani mwaka huu. Let us be realistic. Itabidi waombewe kuahirisha kwa mwaka mmoja, na wapewe counselling tu kwa sasa.

Naunga mkono ila naongozea kuwa hiyo kesi ikifunguliwa tuchangie gharama za wakili tofauti na mchango huu wa mjane
 
Maggid,
Msaidieni mjane wa Mwangosi afungue kesi ya madai dhidi ya serikali na jeshi la polisi.

Majid mjengwa;
Vii hakuna namna yeyote ya kuwafungulia kesi kamanda Michael Kamuhandaa(Iddi Amini) na vijana waliochangia kifo chake kwa kipigo na muuaji mwenyewe binafsi niko tayari kuchangia mfuko huo ili kuona haki inatendeka badala ya kuwaachia polisi wenyewe wahakikishe haki inatendeka wakati wao ndio waliosababisha kifo cha mhusika?

Ni muhimu sana Ndugu Mjengwa uisaidie hiyo familia kutafuta wakili wa kuwasaidia kufungua kesi ya madai dhidi ya Polisi na Serikali ya Tanzania.

Nyie mnamtaka Maggid asaidie kufungua kesi dhidi ya Serikali wakati Maggid yeye anasema CHADEMA ndiyo imemuua Mwangosi! Mkuu Matola emu njoo uchangie hapa!
 
TUMBIRI ninachokifikiria mimi sasa hivi for good ni kumuweka huyu Maggid kwenye ignore list yangu, huyu kwangu ni zaidi ya shetani na sitakaa tena nimuweke kwenye kundi la binadamu.
 
Last edited by a moderator:
At least huyo Majjid unayemuona hana hizo sifa ametoka zaidi a kilomita 300 kwenda kumjulia hali mjane wa marehemu na kumtafutia the way forward, tofauti na wewe uliyekaa nyuma ya skrini ya hiyo device yako ukiandika maneno yenye lengo la kumkatisha mtu tamaa.
Nadhani jukumu la kumsaidia mjane wa Mwangosi sio la Majjid pekee, ni la kila mmoja wetu. Na itakua hatumtendei haki Majjid kama tutabeza juhudi zake.
Na kama unaona Majjid sio mtu stahili kwa nini usichukue wewe hilo jukumu la kumsaidia mjane wa Mwangosi kutafuta haki yake Mahakamani?
Majjid Mjengwa nakuheshim na naomba Mungu akupe nguvu ili uzidi kumsaidia mjane na familia ya marehemu Mwangosi ambaye Kamuhanda aliamua amnyang'anye uhai wake.

Chilli,
Kwanza Majjid hajatoka km 300 kwenda kumjulia hali mjane wa marehemu, na mimi sina tatizo na yeye kukusanya michango ya kumsaidia mjane wa marehemu. Nilikwisha mpongeza kwenye thread aliyoanzisha hapo awali akitoa na majina ya waliokusanya michango. Ukitaka unaweza kutafuta.

Pamoja na jitihada za kukusanya michango, hiyo haiondoi ukweli kuwa Majjid hawezi kuisaidia familia ya marehemu kudai haki yao mahakamani. Ujasiri huo hana.
 
nimemuona leo kwenye gazeti la nipashe Dr. Asha Migiro akicheza ngoma nikashangaa sana aliyekuwa naibu katibu wa UN

ni cheo kikubwa sana Leo hii haki za binadamu zinavunjwa hata kutoa tamko hakuna jamani angalau hata kulaani hakuna.

utetezi wa haki za binadamu unaishia Newyork tu. ukitoka kuja Tanzania unakaa kimya kuhusu haki za binadamu wakati

raia wakiuawa bila hatia. waandishi jaribuni kutusaidia kupata maoni yake tukione hicho kigugumizi chake cha kukataa

kumuhudhi jk
Asante kwa mawazo yako ya kijasiri na yenye mantiki tele.Yaani huyu mama kaniudhi na kunikera to the maximum.NDIO HAWA AMBAO ETI ALIKUWA UMOJA WA MATAIFA KUFANYA NINI?Hivi mpaka tunavyoongea hajatimuliwa kweli kule?na hii UWT si wing ya nyinyiemu mbona hawajaongea lolote kuhusu huyu mjane?jamani i suggest uanzishwe mfuko maalumu wa kusaidia kesi ifunguliwe.
 
Ni muhimu sana Ndugu Mjengwa uisaidie hiyo familia kutafuta wakili wa kuwasaidia kufungua kesi ya madai dhidi ya Polisi na Serikali ya Tanzania. They should sue the state (whose agents the Police are,) for at least two billion shillings.

Sidhani watoto wao wataweza kufanya mitihani mwaka huu. Let us be realistic. Itabidi waombewe kuahirisha kwa mwaka mmoja, na wapewe counselling tu kwa sasa
.

Nakuunga Mkono sana katika hili la Watoto wa Mwangosi kufanya mtihani katika kipindi hiki. Jamani, hawa watoto watakuwa wameadhirika mno kisaikolojia kwa kifo kibaya kilichompata baba yao. Naamini kwamba hawako katika hali ya kufanya mtihani wowote ule.
Tunaomba JF wenzetu walio karibu na Idara za Elimu zinazohusika, watuwakilishie maombi yetu haya ya kuomba Watoto wa Mwangosi waahirishiwe kufanya mitihani angalau kwa Mwaka huu. Inasikitisha.

 
TUMBIRI ninachokifikiria mimi sasa hivi for good ni kumuweka huyu Maggid kwenye ignore list yangu, huyu kwangu ni zaidi ya shetani na sitakaa tena nimuweke kwenye kundi la binadamu.

...Mkuu Matola, mbona umechukia hivyo? Nini chanzo cha hasira yako na Mkuu Majjid?

 
Last edited by a moderator:
LHRC wameingia mitini, nyie mtaweza? Madaktari wenyewe wamejichanganya wengi wanaomba radhi kwa kile walichokifanya. Huyu mama hana sababu ya kuanzisha kesi za kijinga za kumpotezea muda hata wa kulisha kuku au kujifunza kupiga picha. Akishitaki ndiyo anamrudisha mumewe?

Kikubwa ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo na kushukuru wadau wote ambao wanamchangia fedha za kujikimu huku akitafakari safari yake na wanae. Hizo kesi kufungua ni pesa, badala umpe pesa apeleke shule, unashauri aende kupotezea kwa walengwa wenyewe waliofanya hayo yaliyotokea.

Tuwe wabunifu wa kufikiri!
 
kuhusu kufanya mitihani, bora tu wajitahidi wafanye, Mungu atawasaidia. kuhusu kufungua mashtaka mimi binafsi nawashauri hapana, hata watuhumiwa wakihukumiwa haitabadilisha yaliyotokea- kwa kifupi hamna replacement ya mume, baba kipenzi aliyeuawa kikatili. hayo nawashauri wamshukuru Mungu wayaache yameshatokeaa, kwa wakati wake Mungu kama ni hukumu atahukumu kwa haki, hatapendelea.
mnaweza mkaamini katika kushitaki, mkaja kubaki midomo wazi jinsi hukumu itakavyotolewa,msiamini masikio na macho yenu. Mungu awape faraja yake na maisha yaendelee, japokuwa hamuwezi kusahau haraka hilo tukio-Mungu awasaidie sana.
 
Mmmh MAREHEMU NAYE ALIKUWA JEMBE yaani alikuwa hajafikisha miaka 40 tayari ana mtoto yuko form 4. haya marehemu huwa hana kasoro. R.I.P JEMBE.......
 
Inatia hasira kuona idadi ya watoto yatima ikiongezeka kwa upumbavu wa polisi. kamuhanda walishe na kuwasomesha hao watoto au laa wakwako pia watabaki yatima kwani maombi ya Watanzania hayaendi bure. Hivi umepata nini kwa kumuua Mwangosi, damu isiyo na hatia ni laaana kubwa kwako na kizazi chako chote. Unajisikiaje watoto wako wanaposema baba tunaomba mkate, baba wa watoto wa mwenzio umemuua. Natamani kuuona mwisho wako maana lazima uwe mbaya tu.
 
nimemuona leo kwenye gazeti la nipashe Dr. Asha Migiro akicheza ngoma nikashangaa sana aliyekuwa naibu katibu wa UN

ni cheo kikubwa sana Leo hii haki za binadamu zinavunjwa hata kutoa tamko hakuna jamani angalau hata kulaani hakuna.

utetezi wa haki za binadamu unaishia Newyork tu. ukitoka kuja Tanzania unakaa kimya kuhusu haki za binadamu wakati

raia wakiuawa bila hatia. waandishi jaribuni kutusaidia kupata maoni yake tukione hicho kigugumizi chake cha kukataa

kumuhudhi jk
the last tym I checked, the woman is a gamba...so a gamba shud behave like one...sijaona gamba lolote kwa nafasi yake kwenye chama hicho akizungumzia chochote kuhusu suala la the late Mwangosi...
 
naona uchungu kwasababu nikwaangalia watoto na mama yao, I imagine the trauma they r going through ila Mungu ni MWAMINIFU SANA yaani saaaaana.

mama Mwangosi asidanganywe na mtu akapoteza muda wake ati kufungua kesi dhidi ya hao jamaa. awaache, though inauma ila awaache na kukabidhi maisha ya kwake na wanae kwa Mungu. she needs to move on with life and I believe the family will lead a successful life as long as Mungu yuko pamoja nao.

our life right here on planet earth gives us a partial flavour of both heaven and hell as much as each one of us deserves. I'm one of those people who believe in the existence of karma (what goes around, comes around). so, the Almighty will provide unimaginable hell taste of life slaps to these vampires (also known as Mwangosi's murderers) one after another, kuanzia waliopanga unyama ule mpaka walioitekeleza na wale wote wataohusika kuinyanyasa familia ya marehemu, kila mmoja kwa stahiki yake, Mungu hakosei hata mara moja!
 
LHRC wameingia mitini, nyie mtaweza? Madaktari wenyewe wamejichanganya wengi wanaomba radhi kwa kile walichokifanya. Huyu mama hana sababu ya kuanzisha kesi za kijinga za kumpotezea muda hata wa kulisha kuku au kujifunza kupiga picha. Akishitaki ndiyo anamrudisha mumewe?

Kikubwa ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo na kushukuru wadau wote ambao wanamchangia fedha za kujikimu huku akitafakari safari yake na wanae. Hizo kesi kufungua ni pesa, badala umpe pesa apeleke shule, unashauri aende kupotezea kwa walengwa wenyewe waliofanya hayo yaliyotokea.

Tuwe wabunifu wa kufikiri!
Tumeona miaka michache iliyopita kulikuwa na kesi kama hii. Ni ya Imran Kombe ambaye alipigwa risasi "kwa makosa" na polisi. Mjane wake alifungua kesi ya madai, na kama kumbukumbu zangu ni sawa basi alilipwa kwenye milioni 600.

Nadhani sio lazima kuwa na fedha kwanza. Ukiacha mawakili wa msaada, kwani haiwezekani kukubaliana na wakili sehemu gani ya fidia atachukua na akafanya kazi yote kwanza? Wakili wa mjane wa Kombe nadhani alikuwa Eric Ngmaryo wa Moshi. Labda ingekuwa vema Majid awasiliane naye kwa ushauri zaidi.
 
kuhusu kufanya mitihani, bora tu wajitahidi wafanye, Mungu atawasaidia. kuhusu kufungua mashtaka mimi binafsi nawashauri hapana, hata watuhumiwa wakihukumiwa haitabadilisha yaliyotokea- kwa kifupi hamna replacement ya mume, baba kipenzi aliyeuawa kikatili. hayo nawashauri wamshukuru Mungu wayaache yameshatokeaa, kwa wakati wake Mungu kama ni hukumu atahukumu kwa haki, hatapendelea.mnaweza mkaamini katika kushitaki, mkaja kubaki midomo wazi jinsi hukumu itakavyotolewa,msiamini masikio na macho yenu. Mungu awape faraja yake na maisha yaendelee, japokuwa hamuwezi kusahau haraka hilo tukio-Mungu awasaidie sana.
Tuacheni kukata tamaa tunapoonewa. We must learn to fight evil. There is need for the family to sue the government. Ni lazima baba aliyekufa matunzo ya familia yake yatoke kwa serikali iliyomuua. Kesi ya madai ni muafaka, ni muhimu kwa ajili ya wanae.
 
Back
Top Bottom