Nimemsomesha, nimegharamika, leo kaniacha anaolewa na mtu mwingine

Kwanza pole sana kakaangu.Jizuie kufanya maamuz kwa kukurupuka, pili haina haja kulipiza kisasi kwani haitakua final solution ya tatizo, you just move on jifunze kutokana na makosa yako na utambue kwamba hiyo ni sehemu ya maisha ambayo ilikua ni lazima uipitie. Na usiweke the general rule kwamba wanawake wote wapi hivyo wanapendwa hawapendeki 'No' yupo mwanamke wa kwel atakaekuja kukupenda kwa dhati huyo hakya wako na ndio maana kaenda zake. Move on kaka, and keep in your mind life is always unfair so accept the consequences.
 
Tatizo wanaonyesha kiburi hata mahakamani hawakanyagi. Na barua walipelekewa.Kusamehe nashindwa mkuu wangu.

Asante pia
mkuu tatizo mahakamani wanataka vivid documents with vivid amounts she owes you.....bila hiyo document, kumshtaki ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. maandishi mliyoandikiana yako PLAIN.....hayataji kiasi unachodai na huna RISITI ya madai hayo. hata ikitokea akakubali kukulipa hili "DENI" atakulipa kulingana na uwezo wake (e.g sh 100 kwa mwezi) na sheria inamlinda....kumbuka DENI halifungi mtu ila mhusika hutakiwa kutaja kiasi anachoweza kukulipa (mfano tsh 50 kwa mwezi) hadi deni unalomdai la sh milion 15 litakapoisha. hapa ndipo penye ugumu. mkuu, hawa wazazi njaa wakati mwingine sio wa kuwaamini sana. na inawezekana alishapata wajanja wamemfundisha namna deni linapolipwa kwa amri ya mahakama. kumbuka jinsi chenge alivyowagonga watu kwa gari na kuwaua kwa makusudi na aliposhitakiwa akatakiwa kulipa tsh 70,000 (35,000 per person kwa mujibu wa sheria). inawazekana hao wazazi wamechungulia adhabu ya kisheria watakayopewa endapo utawashinda mahakamani ndio maana wanakuwa na jeuri iliyopitiliza. pole sana mkuu, ndio ukubwa huo.
 
du pale zake. mkuu nakuambia hawa nyumbu (wanawake) sio wa kuwaamini hata kidogo.
 
KAMA KUNA KOSA ULIFANYA NI KUANDIKISHANA, TENA MBELE YA MASHAHIDI! MAPENZI NI YA WATU WAWILI NA NI KAFARA! KWENYE MAHUSIANO HUWA TUNACHEZA KAMALI TU NA KUMUACHIA MUNGU ATUONGOZE!
SASA NA WEWE SUBIRI WALIYESOMESHA WENZIO!
 
du pale zake. mkuu nakuambia hawa nyumbu (wanawake) sio wa kuwaamini hata kidogo.
Usiite wanawake nyumbu na mama yako naye nyumbu? Kuwa mstaraabu basi na maneno yako, huyo mwenzenu zawezekana hakupendwa bali zilipendwa pesa zake , mshauri cha maana si kuongea utumbo, hapo mwenyewe hujaoa subiri utaona mke wako atakupigisha na deki chooni.
 
Pole sana, Muwe mnasoma post humu aisee, maana kila siku tunasema MCHUMBA HASOMESHWI . Ushapoteza mkuu, achana na madai samehe na songa mbele.
 

Huo ndo ulikuwa mpango wa Mungu kwa huyo mtoto wa kike. Labda watoto wake watasaidia watoto wako. Haihitaji hasira.
 
Daaa na mm nina kamojaaa nakaacha chuo sitadhubutuu kuinvest pesaa zanguu kwa ajili nampendaa ndio ilaa kujitiaa kitanzii acha anione bahili ila huo upuuzi sitofanyaa of coz nilishaliaa kwenye mapenzi na nilishaapaa apa kutokuliaaa tenaa...pole mkuu najuaa inaumaa jikazee kiume atakujaa kukumbukaa mbelen.narudiaaa polee sanaaaa this chicks aren't loyal.
 
safi kabisa yaani safi kabisa....kila siku tunasema MWANAMKE ASOMESHWI yule hakuwa ndugu yako bila hiyo pesa ungefungua biashara sasa hivi uko mbali kabisa kiuchumi..

Yaani umenikera kweli kweli kama hiyo hela nilichangia aaaaarg
 
Hatuwekezi kabla ya mimba...ili.mtoto.asiteseke...na ndio.gavana yenyewe...mwenzetu sijui ilikuwaje....pole.lakini ndo umejifunza hivo
 
Tusimuhukumu kwa historia
Nachokushauri tu ni kwamba achana na ikiwezekana kufuatilia hata hiyi pesa, kwani hujui mtaka shari kajipanga nini, cha msibgi chukulia kama fundisho na mshukuru Mungu kakuonyesha kabla ni mapema. Mwombe Mungu akupe wepesi na kamwe usijechukua maamuzi ya hasira ukaingia kwenye mitego yao kwani wanajua fika kabisaaaa kua utaumia na wanasubiru waone utafanya nini, cha msingi bora ukae kimya na uendelee na maisha, muda utaongea huenda umeepushwa na mengi mkuu.

Hili liwe fundisho kwako na kwa wengine pia
Acha kufanya maamuzi ya hadira tulia usipoteze na kipato kilichobski kwa kumuadhibu mtu, mwache Mungu atafanya kazi yake
 
Ulifanya kwa upendo muachie Mungu. Utapata tu atakayekupenda. Amini nakuambia baada ya miaka kumi penye uhai utakuja kumbuka haya maneno yangi. It is not about yeye kuolewa na mwanaume mwingine kwani kwa kuwa moyo ulikwishapenda kwingine hamna jinsi. Tatizo ninamna alivyokuacha. Mkataa pema pabaya panamuita. Most probably alimuelezahuyo mwanaumeuliyomfanyia na huyo mwanaume akamconvince akuache. Unadhani mwanaume anamuonaje huyo mwanamke? Itakuja kumgeukia. Achana nayo hiyo kesi, concentrate na kazi yako. Ukitaka kumkomesha usionyeshe kujali endelea na maisha yako!
 
mkuu, sasa kama nyie wanawake sio NYUMBU kwanini mnawapa wanaume shida kama hii?
 
Muwe mnapitia huku jamiii forums kabla hamjaanza kulipia ada. Sasa mambo yameharibika ndio mnatuletea lawama na masikitiko, haya mambo yameshajadiliwa sana humu na majibu yapo.
 
Ameshindwa olewa nawe akijua wewe ni babake mzazi maana hujui kaongea nini na mama'ke
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…