Nimemsikiliza Ridhiwan, Bado

Nimemsikiliza Ridhiwan, Bado

Imma Saro

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
394
Reaction score
197
Nimemsikiliza Ridhiwan Kiukweli bado anashindwa kujenga hoja anajikita kwenye kejili kwa wapizani,
Eti angechangia bila kutaja upizani asingesikika
Unataja mataifa yanayo onyesha vifa vyao vya jeshi,
Sisi tunahoji mabilioni yanayotumika kufanya maonyesho wakati jimboni wanafunzi wanakaa chini,
Wakati jimboni hakuna kituo cha Afya,
Tunajiuliza fedha hizo zote zingetumika katika kuzuia maambukizi ya Dengue
10173634_650551901695474_7079847669657270732_n.jpg
 
Ndiyo anajifunza hivyo, kidogo kidogo anasonga. Mwaka 2025 utasikia amekwishaiva na kuchaguliwa kama mgombea wa kiti cha urais.
 
Nimepita kariakoo leo, mtaa wa uhuru kuna libwawa likuuuuubwa la maji yenye vinyesi, makamasi, makohozi na kila aina ya uchafu. Nikasogea mbele pale jirani na Benjamin Mkapa Sekondari na yenyewe ni madimbwi na barabara mbovu kupita kawaida. Nikasogea hadi Akiba, ni hivyo hivyo. Dah! Serikali ya CCM imeamua kukomesha watanzania
 
Angeweza kutumia dakika zake vyema katika kujenga hoja ambayo ingeweza kulisaidia taifa na kuondoa ile dhana ya kwamba kapewa kwa kuwa mtoto wa mkubwa,
Pili unaposema kuonyesha sila ni kawaida ni sawa ila kila sherehe zinamaandalizi yake kwani tunasiku ya mashuja hivyo tungetumia siku hiyo kuonyesha hizo zana za kivita, na sio sherehe za Muungano,

Give the devil its credit where it is due.Amejitahidi, juzi tu ameapishwa na leo ameweza kuongea bungeni JAPO NI UTUMBO.Kuna wabunge wengine tangu wachaguliwe leo mwaka wa 4 hawajawahi kuthubutu kuongea bungeni. Wabunge hao ni kama ;-)
1. Lameck Airo (CCM, Rorya)
2. Mohammed Dewji (CCM, Singida)
3. ....................
4. ..............................
5. ...............................
 
Angeendelea na sheria aachane na siasa, bongo wengi wetu sio creative tunapenda kurithi mpaka ajira za wazee wetu kama vile ni ufalme
HUSSEIN MWINYI
MAKONGONGORO NY
A.MALIMA
RIDHIWANI
MGIMWA'S
 
nipe muuuudaaaa makali ya jembe yanaonekana baada ya kujua udongo ukoje
 
Hayo yangetoka kwa Tundu ungemwita jembe. Vilaza bwana wala usiwalike kwenye sherehe
 
Ndiyo anajifunza hivyo, kidogo kidogo anasonga. Mwaka 2025 utasikia amekwishaiva na kuchaguliwa kama mgombea wa kiti cha urais.

Kwa hiyo tumekubali kuwa bunge letu ni la kujifunzia................!! Mwakani usije kuta akina Black Widow na Nshoza wamo kwenye hilo darasa!!
 
Angeweza kutumia dakika zake vyema katika kujenga hoja ambayo ingeweza kulisaidia taifa na kuondoa ile dhana ya kwamba kapewa kwa kuwa mtoto wa mkubwa,
Pili unaposema kuonyesha sila ni kawaida ni sawa ila kila sherehe zinamaandalizi yake kwani tunasiku ya mashuja hivyo tungetumia siku hiyo kuonyesha hizo zana za kivita, na sio sherehe za Muungano,

Hata utoe saa nzima mtu kama huyu hawezi kujenga hoja. Thinking is veru difficulty. Kuna watu unaweza ukadhani wanafikiria lakini siyo kweli. Biolojia inasema baadhi ya wale unaodhani wanafikiri, ukweli ni kwamba kichwani wanaona maluweluwe tu! Hakuna fikra na hapo ndo utamuona mtu anatoa hoja zisizoungana.

Hakuna kitu hapo hata kwa miaka 20 ijayo. It's a product of brain architecture.
 
Mnafikiri kuna chamaana atakachoongea, Kwani Komba alishawahi ongea kitu cha maana Bungeni kwa manufaa ya Taifa?.
 
Nimepita kariakoo leo, mtaa wa uhuru kuna libwawa likuuuuubwa la maji yenye vinyesi, makamasi, makohozi na kila aina ya uchafu. Nikasogea mbele pale jirani na Benjamin Mkapa Sekondari na yenyewe ni madimbwi na barabara mbovu kupita kawaida. Nikasogea hadi Akiba, ni hivyo hivyo. Dah! Serikali ya CCM imeamua kukomesha watanzania
Mkuu..nje ya mada kidogo...hivi ulikuwa unafanya utafiti gani hadi ukagundua/ukaona makohozi, kinyesi,
Makamasi n.k? Samahani lakini...maanake huo mchangayiko hata mzoga wa paka una afadhali..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom