Wanajamvi nashukuru kwa comment zenu mchanganyiko. Kwa muhutasari nimefarijika na kupata jibu muafaka. Njia pekee ya kuwa salama ni kuacha mahusiano nje ya ndoa, mbinu rahisi ni kuacha fikra na mawazo ya kutamani tamani. Pili, ni kuacha kuanzisha mahusiano mapya. Inawezekana kabisa kati yetu tunatumikia kifungo kama changu, njia pekee ya kuwa huru ni kuacha kuanzisha mahusiano mapya, pindi mahusiano yaliyopo yatakapoisha na iwapo dhamira yetu si kuanzisha mengine mapya basi hiyo itakuwa ndio tamati.
Mwisho kabisa UKIMWI ni kweli unaua njia pekee ya kupambana na gonjwa hili ni kuacha kufanya ngono kabisa, kuwa mwaminifu kwa mpenzi mmoja na yote hayo yakishindikana tusisahau kutumia kondom na tuzitumie ipasavyo.
Tanzania bila unyanyapaa, maambukizo mapya na vifo vitokanavyo na UKIMWI inawezekana.