ni kwamba, majini na mashetani wanao uwezo kuzaa na wanadamu, ilishawahi kutokea hivyo hata enzi za zamani malaika waliotupwa chini kuvamia wanadamu wakazaa nao wakatokea watoto walioitwa majiti (the giants) kina Goliath wa kule Gaza ya palestina na wengine. hao walikuwa majitu yenye miili mikubwa kuliko hii na yalitumiwa na shetani kufanya kila lililo kinyume na watu wa Mungu.
hapahapa bongo, wachawi wanaelewa hili, mara nyingi tu wanawake wanaamkaga asubuhi wanakuta wamelowa, wamefanywa kichawi na wachawi bila wao kujua, pia majini yanalala na yanaoa wanawake na wanaume wengi tu, watu wa Tanga na watu wa pwani wanajua hili, na hata humu yawezekana wapo walioolewa na majini. yapo pia yale wengi wanayajua kama pepo mahaba/jini mahaba ambalo linakujia kwenye ndoto usiku na unahisi uhalisia kufanya tendo la ndoa. kwa ufupi, majini na mashetani na wachawi, wanao uwezo kukufanya chochote kama hauna Yesu Kristo moyoni. ninyi nyote msio na Yesu moyoni, mnaweza kuingiliwa na majini any time, unakumbuka kipindi cha popobawa?
majini ya aina hiyo sasa, wakati mwingine huwa yanavaa mwili wa mwanadamu na yanazurura mitaani, na yana nguvu ya mvuto kwa yeyote asiye na Mungu. na majini hujivika mwili wa sura nzuri, ila kiuhalisia yana sura mbaya kuliko chochote. kule kariakoo yamejaaa na njia panda ya magomeni mataa pale. mara nyingi tu watu huwa wanakutana na watu, na wale wenye macho ya kiroho huwa wanayaona, ila yakiona mlokole huwa yanabadilisha njia yanakimbia.