Nimemkumbuka Dr. Slaa

Nimemkumbuka Dr. Slaa

kt the irreplaceable

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2017
Posts
2,387
Reaction score
4,932
"Nitakapo apishwa kuwa rais wa JMT, mwakipesile ukatafute nchi ya kwenda" maneno ya ukali na gadhabu ya Dr wilbrod Slaa wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010 pale jijini mbeya. Itakumbukwa kuwa mkuu wa mkoa wa mbeya kwa wakati huo John mwakipesile, alifanya kila aina ya figisu kuhakikisha Dr slaa hafanyi mkutano mbeya, kwanza umeme ulikatika jiji zima na pia polisi walikua wanachelewesha kuanza kwa mkutano ilihali mwisho wa kampeni ulikua saa kumi na mbili jioni. CCM walimuogopa Dr slaa, alikua na ufuasi mkubwa wa vijana waliokua wakitaka new regime

Nakumbuka nilikua kidato cha tano wilayani Rungwe mkoani mbeya, hivyo niliruka ukuta na masela na kusafiri mpaka mbeya mjini kumsikiliza Dr. Slaa was a presidential material, alikua anajua kuhutubia, anajua kujenga hoja, na msimamo mkali kwa vile anavyoamini. "Nikiwa rais elimu Bure toka chekechea mpaka chuo kikuu, nikiwa rais sitaki kumuona mtanzania anaishi nyumba ya tembe..." Rafiki yangu mmoja alikua afande pale mjini alininon'goneza "hakika hili jamaa hata mie natamani lichukue nchi".Hakika Dr slaa aliijua siasa.

Hata baada ya kuukosa uraisi dr slaa alipania kukijenga chama mpaka kwenye ngazi ya shina, CHADEMA ilipata uungwaji mkono mkubwa sana kipindi hiki. Kila ukivaa kombati za kaki mtaani ulionekana kuwa shujaa tena kamanda kweli kweli.
Kwa wakati huo kua chadema ilikua ni sifa tosha, spirit ya Dr slaa ilienea kwa vijana wengi wadogo nchini. Ilikua ni nadra kumkuta kijana ccm, wazazi wangu wote ni CCM ila walishangaa jinsi mtoto wao nilipokua nawapa shule ya upinzani. Nakumbuka mama alinambia... " mwanangu siasa haitakiwi uwaamini watu kiasi hicho, hyo ni kazi ya kutafuta kula kama kazi nyingine tu". Wala sikua na habari.

2015 mwenyekiti alifanya kosa kubwa sana ambalo litakitafuna chama kwa mda mrefu sana. Ile gia alioibadilisha hewani ilifungua vichwa vya vijana wengi ikiwepo mimi na kuamini kuwa siasa ya upinzani ya Tanzania ilikua ni ya viongozi wenye njaa, wasio na misimamo, na wenye uchu wa madaraka, eti mtu aliye ndani ya chama kwa mda mrefu, mtu aliyeshiriki kueneza Sera, hoja na propaganda ashindwe kuaminiwa na badala yake aje mtu tuliemtusi na kumpa kila aina ya tuhuma!!!. Lahaula ilikua kituko. Hakuna kampeni ziliojaza watu za upinzani, kama kampeni za kukemea ufisadi!! Kumbuka oparesheni sangara, Ile list of shame ya Dr slaa ilifungua milango ya fahamu ya watanzania kuhusu nchi yao. Lakini mambo yote haya yalibadiliswa ndani ya wiki mbili tu baada ya mwenyekiti kubadili gia angani na kumchukua kamanda dhaifu ambaye hakuwahi hata kuvaa kaki, ilionyesha dhahiri alikuja kimwili tu ila kiroho alikua kule aliporudi saizi. makamanda hawakuongelea tena kuhusu ufisadi badala yake tulizungushwa mikono kuimba mabadiliko.. Walio jikoni wana siri nzito juu ya nani alifaidika na uzungushwaji mikono huu.

Leo hii CHADEMA hujui kama wana katibu mkuu, jamaa yupo yupo tu. Vijana wao na wabunge wao wanaendesha siasa kiujanja ujanja tu. Wanadandia kila hoja mitandaoni, hawana zile amsha amsha za Dr wengi wamekaa kipigaji pigaji tu kusubiri kuunga juhudi. Eti wanashabikia kiongozi wa ccm kumchallenge magufuri 2020, inaonekana hata adui yao saizi hawamjui.
Binafsi niliistaafu siasa za Tanzania 2015 nikijikita zaidi na kutafuta namna ya kulea kizazi changu kijacho, sasa nimeamua kuwa mtizamaji tu... Upinzani una safari ndefu kwenda kuishika dola, huu ni ukweli mchungu kuumeza.

The irreplaceable.
 
Nliacha kushabikia siasa mwaka 2015 sina chama mpaka sasa ila sifurahishwi na haya yanayofanywa na ccm

Nliona wanasiasa ni wale wale hasa baada ya kumpitisha lowasa agombee uraisi

Siwezi elezea ghadhabu nlyopata ya ule unafiki

Ila nkaapa siwezi shabikia ccm maisha

Ila neutral mind
 
Nliacha kushabikia siasa mwaka 2015 sina chama mpaka sasa ila sifurahishwi na haya yanayofanywa na ccm

Nliona wanasiasa ni wale wale hasa baada ya kumpitisha lowasa agombee uraisi

Siwezi elezea ghadhabu nlyopata ya ule unafiki

Ila nkaapa siwezi shabikia ccm maisha

Ila neutral mind
kwanini watu wanalalamikia awamu hii?
 
Hungeweza kuona Dr. Slaa akiokoteza maneno ya kihuni ya humu mitandaoni kama vile "jiwe, mshamba, chatle" nk kisha unaenda kuyaandikia hoja kama afanyavyo Lisu na wafuasi wengine wa chadema!

Slaa alikuwa anaibua hoja mpaka system inatetemeka.
 
Slaa kaondoka chadema kwa ustadi mkubwa sana, lengo ni kulinda reputation yake atakapukuwa nje ya chadema, na sasa anakula matunda ya kazi aliyoifanya.
Nliacha kushabikia siasa mwaka 2015 sina chama mpaka sasa ila sifurahishwi na haya yanayofanywa na ccm

Nliona wanasiasa ni wale wale hasa baada ya kumpitisha lowasa agombee uraisi

Siwezi elezea ghadhabu nlyopata ya ule unafiki

Ila nkaapa siwezi shabikia ccm maisha

Ila neutral mind
 
Yupo CCM anakula bata kule Stockholm!!
Alinyimwa kugombea ubunge akiwa CCM akahamia CDM,kanyimwa kugombea uraisi akiwa CDM akahamia CCM. Kwa hiyo yeye haoni wengine kufaa kugombea bali yeye tu!?
Shida yake kubwa hana maamuzi, maamzi hutoka kitchen.
 
Alinyimwa kugombea ubunge akiwa CCM akahamia CDM,kanyimwa kugombea uraisi akiwa CDM akahamia CCM. Kwa hiyo yeye haoni wengine kufaa kugombea bali yeye tu!?
Shida yake kubwa hana maamuzi, maamzi hutoka kitchen.

Ndo mana mnaonekana wa Ajabu. Hamjui hata kamanda Wa kweli ni Yupi. 2014 nilikuwa tz. Slaa alikuwa Tishio nakwambia. Sasa Hivi wote wqshamba.
 
Hheri waliobaki kwa sisi tunaomjua Toka miaka ya 1994 wakati yunampokea Krt hadi anarudi ccm hiiii any way tuyaache once msaliti . always msaliti
 
Back
Top Bottom