Zee Korofi
JF-Expert Member
- Oct 5, 2021
- 1,604
- 1,440
Natanguliza samahani mno ikiwa kuna watu nitawakwaza. Huyu ni msichana mzuri na nadhifu na tuna mazoea kidogo, nilichukua namba nikamwambia namuhitaji, hakuwa na hiyana. Muda wote huu nilijua anaitwa Faith (nahisi nilisikia vibaya).
Tukakubaliana tukutane juzi Pub fulani, sasa kabla ya kukutana akanitafuta kwa namba ngeni, nikauliza jina akaniambia Fadhila, sikuamini nikazama TigoPesa nihakikishe, nakuta ngoma 'Fadhila' imevimba pale.
Nikapiga ile namba akapokea manzi wangu, sikuonesha mshtuko kwake ila nikauliza kama ni kweli anaitwa Fadhila, akakubali. Tangu muda huo mpaka sasa nimemchunia, na hatukukutana.
Msichana mzuri ila sijapenda jina lake, limekaa kienyeji mno (samahanini sana kama nitawakwaza). Hapana aisee!