Nimemchoka sana mama yangu

nilifanyiwa kitendo hicho Mara moja nikawa silali tena labda tuwe wengi chumban.na form one nikaanza kukaa kwa mama..kazi natafta na mimi siyo legelege
 
Mpendwa lady Jay.., Hebu acha kuwa mwizi wa fadhila, huyo ni mama yako alikubeba miezi 9 na akakusomesha hadi kufikia hapo !! Wewe hujui madhila na shida alizopambana nazo huko nyuma !!

Yaani hata ufanyejee huwezi mlipa au kulinganisha fadhila zake !!! So be polite na umtii na kuhakikisha apate mwisho mwema..... !!!
(kama kukaripiwa /kutukanwa/kusimangwa wingi mbona wamepitia)
 
You nailed it Mrs ake.

Cha kwanza lady hana budi kumsamehe mama ake Kwa yote. Anapitia na atapitia magumu mengi na mama yake, but hana budi kumsamehe kama anataka aishi kwa amani. Hatujui nini kilitokea, but inawezekana mama yake ni mtu aliyeweka uchungu mkubwa moyoni, unfortunately uchungu huo anaumalizia kwa mtoto. Kuna kitu possibly kinachomuumiza kwenye yale mahusiano na baba mtoto, na hajawahi kukiachilia moyoni mwake wala kumove on. Maumivu yote anayahamishia kwa mtoto, siku akija kuyaachilia utashangaa atakavyoumia na kujuta juu ya yote anayokufanyia. Muombee mama ako, possibly anachokifanya ni out of her control, muombe Mungu aingilie kati.

Inaumiza mnoo, but mchukulie mama ako kama udhaifu wako, kama jaribu lako ambalo huwezi kumtupia mtu mwingine. Muombe Mungu akupe hekima ya kuishi na mama ako, na kila siku muombee mama ako akauachilie huo uchungu

Above all, kemea roho ya kukataliwa, kama alivyosema mrsleo. Muombe Mungu akupe kibali mbele zake na mbele ya wanadamu. Hutokataliwa tena, hutochukiwa tena, utakubalika popote pale utakapokuwa na utakapoingia. Mungu akutie nguvu na akutetee katika hili
 
nilifanyiwa kitendo hicho Mara moja nikawa silali tena labda tuwe wengi chumban.na form one nikaanza kukaa kwa mama..kazi natafta na mimi siyo legelege
Sawa, basi endelea kutafuta kazi umuepuke huyo mama yako anayekuchukia. Watu wanasema huyo ni mama yako huna jinsi.....mimi nakwambia usipoteze muda kwa mtu asiyekupenda.....hata kama ni mzazi. Haijalishi alifanya nini kikubwa angali ukiwa mdogo.....kwani wewe uliomba uje duniani? Kwahiyo kukulea kwa upendo jukumu lake.

Jambo lingine, usikae nyumbani unasema unatafuta kazi, toka nenda kafanye kazi kwenye mashirika kwa kujitolea, nenda kaongee na watu.....tena umesema wewe si legelege? Ukiwa smart utapata sehemu ya kufanya kazi hata week haitaisha.
 
asante
 
Pole sana, jitahidi kutafuta kazi kwa bidii kubwa nadhani hata humu kuna kazi huwa zinawekwa humu jaribu kuapply usichoke na ukifanikiwa kaa mbali kabisa na mama yako kwa kuhakikisha mnakutana mara chache sana hasa kukiwa na ulazima wa kufanya hivyo. Inawezekana mama yako mdogo labda hakuwa mkweli kwako labda huyu si mama yako mzazi au alikupata katika njia ambayo hakuipenda hivyo chuki na hasira zake ya kitendo alichofanyiwa imehamia kwako. Pole sana.
 


Pole sana Lady J.
Vumilia umalize masomo yako. Jitunze, uwe Mcha Mungu na baadae utafanikiwa na kuwa nguzo ya kutegemewa katika familia yako. Hakuna lisilokuwa na mwisho. Mtegemee Mwenyezi Mungu utafanikiwa.
Amin.
 
Pole sana Lady J.
Vumilia umalize masomo yako. Jitunze, uwe Mcha Mungu na baadae utafanikiwa na kuwa nguzo ya kutegemewa katika familia yako. Hakuna lisilokuwa na mwisho. Mtegemee Mwenyezi Mungu utafanikiwa.
Amin.
Asante
 
sio wazazi badilikeni wewe ndo ubadilike km ulikua unalala na wanaume bila kinga siku za htr uache yaan kwakifupi ujitambue mambo yanayotokea kati yako ww na mama ako ni matokeo ya mama yako kupewa mimba bila plan yeyote matokeo yake katelekezwa na baba yako usikute na ww unfanana na baba yako bas mihasira yote unapewa...aliyekuambia huyo sio baba ako nae mpuuzi tu ulipaswa kujua badae sn mnk baba ako hakujali uwepo wako...matokeo yake ht ukifeli unataka uchekewe kisa mama yako...ni ujinga huo....mama kutokukupenda ni mihasira yake ya mistakes zake za ujana ambzo ww inabidi ujifunze zisikutokee...si mara zote mara nyingine ht ww unakosea kwahy lzm uzinguliwe kwan wewe nani usisemwe?tafuta kazi kaa nae mbali mpe nfs heshima irudi khs kumchukia ni upuuzi wako mwenywe wa kutojua binadamu si mkamilifu....sikushangai ukikua utaacha...mama ako akikosea jifunze kutokana na makosa yake othrwise ni ngumu
 
sawa nimekuelewa ila sijawahi kufeli.pili silalamiki kusemwa nikoseapo tena nakiri kosa na kuomba msamaha na simchukii mamangu ni upendo tu hupungua kwasababu hana upendo kwangu kabisa na naona hivi tangu udogoni
 
Kuna jambo alilotendwa na Baba yako likamuumiza sasa wewe ndio umekuwa pa kulipia kisasi.
Msamehe ila kama kuna watu wazima anaowaheshimu jaribu kuongea nao ili wamwite na kumuonya! Ingawa hatofurahishwa na wewe kutoa siri yake lakini itakuwa dawa na ataacha kukunyanyasa kwa Uwezo wa Mungu.
 
Mm, kweli mama ni mama tu. Pole sana, ila huyo mama yako kama kuna siku itafika mungu angemfunulia na kukumbuka kwamba wewe ni mtoto, tena na kwamba wewe hukutuma application ili akuzae. Ni wajibu wake kama mzazi kukupa mapenzi. Ni excuse ipi huyo mama atakuwa nayo yakutokukupenda. Mama yako anahitaji msaada wa kisakologia!! Jipige moyo konde na wewe utakuwa na maisha yako. Mwenyezi mungu atakusimamia na kukuguta machozi. Ninarudia tena: mama yako anapashwa kusaidiwa. And girl, you are a brave one, you have made it up to now. Stop crying, just pull up your socks as you have done: maisha mazuri yanakusubiri. Things pass: remember that. Sure, you will make it. Ku share hili tatizo lako na sisi: iwe therapy kwako. Afadhari umefunguka, tangu sasa just look forward, umuangalie mama yako kwenye miwani ya mbao. Na tena usitafute mume kama ndiyo solution ya maisha yako (wanaume nao ni kazi) NO. Rafiki sawa wa kupeana naye mawazo, TIME WILL TELL. Wishing you, all the best!!
 
asante sana
 
Sasa bi mdashi kama huyo wa kazi gani????

Huyo dawa yake ni kumlia timing kwenye kona ya ukuta na kumkwida Nondo ya bichwa! Aendee akaanzishe ubabe wake huko kuzimu!!
 
Pole sana, Inahuzunisha sana.
Ni bora hata angekuwa ameshafariki ujue moja, Kinachouma zaidi ni kufanyia yote hayo na mama yako mzazi, Mtu ambaye ulipaswa uwe karibu katika nyakati zote maishani.

Kama mama anakufanyia hivyo ni nani zaidi unayeweza kumdekea na akakufariji unapopata matatizo dunia hii.

Inahuzunisha sana,
Inatia hasira sana,

Nini Ufanye?
Mtii kuanzia sasa bila manung'uniko, Fanya kile anachokihitaji kwa ubora au Mara mbili zaidi ya matarajio yake.


Ni kitu kigumu lakini jitahidi kufanya bila kulalamika, Wakati unafanya yote jitahidi kujenga mazoea mazuri na watu hasa was mtaani kwenu huku ukimuomba Mungu.

Naamini baada ya muda, mabadiliko utayaona, Mabadiliko hayo yaweza kuwa ni kwa wewe kupata kazi au mama yako kukuhurumia.

Every Problem has a solution.
 
usijali dada jikaze ndo maisha hayo ipo siku yataisha tu cha muhimu komaa katika kitabu na Mungu pia basi.
 

WW LAZIMA UWE WIFE MATERIAL UKIINGIA KWENYE NDOA SIO SIRI NATAFUTA WATU WA HIVI, WALIOPITIA CHANGAMOTO, HAKUNA LINALOSABABISHWA WASUMBUA SIO WABINYA SAUTI WENGINE HUKO MTAANI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…