Nimemchana Ukweli Mke mtarajiwa

Sasa kwani kakosea nini hapo?
Mbona tena kawa mstaarabu kabisa kakupa taarifa mapema!
Labda sema tu kuwa uwezo wa kuwahudumia ndio huna lakini hata hivyo sidhani kama huo uwezo wa kula nao kwa hiyo siku moja huna. Nahisi ni roho mbaya tu!

Kama ni mkeo mtarajiwa atakuwa anaijua hali yako kiuchumi labda kama huwa unamdanganya hali yako. Kwa hiyo hata akija akashindia maandazi hatashangaa kama anaijua hali yako na pengine amejipanga kukusaidia wawapo hapo kulingana na hali yako ilivyo!

Kiujumla huna upendo hilo haliwezi kuishia kwa huyo tu, hata kwa ndugu zako inaonekana huwezi kuwasaidia kwa roho hiyo!
Mi ninavyompenda mchumba wangu lazima niwapende na ndugu zake na ndivyo ninavyofanya na ndiyo furaha na amani yangu ilipo!
Hakuna kitu nafurahi kusikia mchumba wangu akinieleza jambo kutaka msaada kwangu maana yake ananiamini(hapa nasemea mambo ya msingi) na huwa sina hiyana kabisa kumsaidia.

Umeniangusha sana brother. Bado hujakomaa kifikra kufikia hatua ya kutaka kuoa maana hujajipanga kimajukumu!

Najua hii ni story tu ila una mawazo ya ovyo!
 
Huyu cjui kama ako serious na
Alichoandika hapo au alikua
Amekunywa kidogo akachanganya
Na bangi

[Color= yellow]Triple A[/color]
Hata mie nahisi changamsha genge tu
 
Vuzuri sana Mungu akubariki. BARAKA zinaanzia nyumbani kwetu. Kristo mwenyewe alianza kuchagua mitume ambao walikuwa ni nduguze.

Hakuna kitu kizuri kama kuyoa msaada kwa mujitaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii hali ngumu ya maisha hakika haiwaachi watu salama. Maamuzi mabovu sana, aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…