Nimemaliza chuo kikuu cha JF

Milale

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
494
189
Habari wanajf wote..
Ikiwa leo nimetimiza miaka 6 nikiwa mwanachama wa JF tangu nijiunge rasmi, nina mengi sana ya kusema ila kwa leo acha niseme haya machache.

Sikubahatika kupata elimu kubwa ya darasani ila elimu kubwa nimeipata hapa hapa JF mpaka leo hii kuna wanaoamini kuwa mimi ni mhitimu wa chuo kikuu tena ngazi za juu.
Kwa elimu hii niliyoipata hapa JF sina budi kusema asante kwa wanachama wote walionipa maarifa haya ambayo najivunia kuwa nayo leo hii.
Mara nyingi huwa napenda sana kusoma machapisho yangu ya miaka ya nyuma kuangalia jinsi nilivyokuwa nahangaika kutafuta ajira humu JF maana hunifanya nikumbuke nilipotoka nilipo na kujua niendako.Na niliweza kufanikiwa hapa hapa na leo hii watu tena wenye elimu kubwa na ambayo niliitamani sana kuipata wanaomba ajira kwangu. ASANTE MUNGU.
Kikubwa nilichojifunza kwa maisha ya sasa vijana tunakosa uaminifu na muda mwingi tunautumia katika masuala yasiyoweza kubadili maisha yetu.

Weka nia, juhudi, nidhamu na malengo huku ukimtanguliza MUNGU, hakika maisha yako lazima yabadilike.
Asanteni sana wanachama wote mlionisaidia kwa njia moja ama nyingine sina cha kuwalipa zaidi ya kusema asanteni na MUNGU awabariki.
 
Broo Milale nakubaliana na wewe sana, elimu inayotolewa humu ni kubwa, na sina shaka umejiajiri kaka. Humu muna shuhuda za waliofanikiwa na wale ambao walikumbana na challenges mbali mbali. Kama upo kwa nia ya kujifunza basi hapa ni Zaidi ya chou kikuu
 
Mwenyezi Mungu aendelee kukubariki.
kwa hapa JF ni wengi tumejifunza mengi nikiwemo na mimi pia.
 
Broo Milale nakubaliana na wewe sana, elimu inayotolewa humu ni kubwa, na sina shaka umejiajiri kaka. Humu muna shuhuda za waliofanikiwa na wale ambao walikumbana na challenges mbali mbali. Kama upo kwa nia ya kujifunza basi hapa ni Zaidi ya chou kikuu
Kabsa hapa mimi pamekuwa msaada mkubwa
 
JF kama kata, streets zenye tabia zote zimo bila kusahau watu wa kila kariba. Ukiona haikuendelezi bhasi ujue wewe ndio umeamua kujidumaza. Hongera mkuu
 
Back
Top Bottom