Samahani ndugu wana jf...niliwahi kufanya kazi ya ku-supply vifaa Halmashauri ya wilaya moja hivi. Kwanza malipo yangu yalichelewa sana mpaka ikabidi nianze kutishia kwenda mahakamani. Baada ya kuwa mkali walinilipa. Nilipopeleka cheque benki baada ya benki kuzipokea siku moja baadae niliangalia balance nikakuta kwamba walikua hawajaipost fedha hio kwenye acount yangu. Nilirudi benki kuuliza kulikoni mbona hela siioni ya cheque nilizoingiza jana yake! NILIJIBIWA KUA HAWA WATU WAMEKULIPA KWENYE ACOUNT AMBAYO HAINA FEDHA....hivyo warudishie cheque zao. Nilipokwenda kuonana nao ikiwa ni mweka hazina wa halmashauri hio niliambulia jibu kua nivumilie mpaka baada ya wiki mbili ndio akaunti hio itakua na fedha. saasa wadau naomba ushauri wenu...hundi ninazo je ninaweza kushtaki ili nilipwe?
Asante sana kwa kunipa mwanga ndugu...nadhani unaelewa hizi kazi za uzabuni ukiwa mchanga mara nyingi unakimbilia kazi tu bila kuangalia namna malipo yatakuaje..nashukuru ssana nazidi kujifunza.Serikali huwa wasumbufu kulipa ingawa watakulipa lakini utakuwa umesumbuka,nilishaifanyia kazi halmashauri moja nikawa nawadai mill 42,hadi kulipwa it took a year tena baada ya kusumbuana,kuna jamaa yangu huu ni mwaka wa tatu mpaka wamepelekana mahakamani,kama capital yako ni ndogo usijaribu kufanya nao coz watakuweka juu ya mawe,kuna ambazo ni nzuri kufanya na watu hao kama za kukusanya ushuru wa mahotel,masoko,stand etc ambapo pesa yako unaikata juu kwa juu