Nimelima mazao yameota mvua hakuna, nakaribia kuchanganyikiwa

Tandam4

JF-Expert Member
Jan 23, 2017
379
824
Wakuu mtu anaweza rukwa akili hivihivi. Katika kupambana na hali ya kiuchumi, mwaka huu niliamua kujilipua shambani na kulima takriban ekari 40 za maharage.

Nikitumia gharama kubwa ktk mbegu na kulima. Sasa maharage yameota tena vizuri sana ila sioni dalili ya mvua kwa siku za karibuni, hivyo kupelekea kukauka kwa zao hilo.

Nasikia kuna wataalam wa asili wanaoweza saidia kunyesha mvua kama si tunguri{Afrika}, basi nuclear[ulaya] nishaurini niende wapi
cc.mshana jr
" mamvi
 
Pole sana.. ume bet ukapoteza, unaweza kunyanyuka ukaendelea na maisha ukiwa umejifunza tayari, au ukaaka na kuendelea kutumaini miujiza
God knows It could be a lot worse Tandam4
"unaweza ukanyanyuka na kuendelea na maisha" "very strong courage. Kunyauka kwa msimu mmoja wa mazao yako sio mwisho wa ww kufanikiwa ndugu bali changamoto hzo zichukulie kuwa ndio mwanzo wa mafanikio yko.
 
Wakuu mtu anaweza rukwa akili hivihivi.Katika kupambana na hali ya kiuchumi,mwaka huu niliamua kujilipua shambani nakulima takriban ekari 40 za maharage.Nikitumia gharama kubwa ktk mbegu na kulima.Sasa maharage yameota tena vizuri sana ila sioni dalili ya mvua kwa siku za karibuni, hivyo kupelekea kukauka kwa zao hilo.nasikia kuna wataalam wa asili wanaoweza saidia kunyesha mvua kama si tunguri{Afrika},basi nuclear[ulaya]nishaurini niende wapi
cc.mshana jr
" mamvi
pole mimi nimelima heka 10 za mahindi kila nikiamka napiga simu kuuliza kama kuna mvua kumbe hamna kitu ila kwa mtaalamu wa singida plz help me hata jinsi ya kutumia umwagiliaji maana kuna siku mtaona uzi kuwa pressure yangu imepanda kisa hamna mvua
 
Kuna uzi huku nilikuwa ninapinga kwa nguvu zote kwamba kilimo hakimsaidii mtu,laiti ungeuona kabla....
Tulishapitamo.
 
Wakuu mtu anaweza rukwa akili hivihivi.Katika kupambana na hali ya kiuchumi,mwaka huu niliamua kujilipua shambani nakulima takriban ekari 40 za maharage.Nikitumia gharama kubwa ktk mbegu na kulima.Sasa maharage yameota tena vizuri sana ila sioni dalili ya mvua kwa siku za karibuni, hivyo kupelekea kukauka kwa zao hilo.nasikia kuna wataalam wa asili wanaoweza saidia kunyesha mvua kama si tunguri{Afrika},basi nuclear[ulaya]nishaurini niende wapi
cc.mshana jr
" mamvi
Pole mdau kama uliweza kulima ekari 40 funga macho chimba kisima ufanye kilimo cha umwagiliaji japo ni gharama lakini hutajutia

Sent from my SGH-T999 using JamiiForums mobile app
 
Usichanganyikiwe omba kudra tu za mwenyezi MUNGU.
CCM wameshasema eti ukame haukuwemo kwenye ilani yao ya uchaguzi, hivyo basi sio wao waliouwepo
 
It's always too risky kufanya kilimo at large scale bila kuwa na reliable back-up ya umwagiliaji.

40 acres kwa kutegemea mvua?!!! mkuu hapo ulikosea sana. Pole sana.

Ktk harakati za utafutaji kimaisha... there is nothing risk-free.

Lose and Learn. Keep the hustling burning.

-Kaveli-
 
Tandam4 usiwe na shaka au kuchanganyikiwa. Mtafutaji huwa hakati tamaa kama siyo msimu huu hata msimu ujao utainuka tena. Kutokupata msimu huu siyo kwamba msimu.mwingine hutafanikiwa. Mafanikio yapo tele kama Mungu akikuacha hai na kama utaendelea kupambana na kujifunza kutokana na makosa.

Hata kama hutapata kabisa chukulia tu hiyo ni changamoto ya kujifunza kuelekea katika mafanikio.

Kumbuka " a smooth sea never makes an experienced sailor"
 
Yaani mijitu mingine sijui inafikiria ikiwa chooni maana maandishi yanakuwa yanayoandikwa hayatofauti kinachokuwa kinatoka kwa ile sehemu.

Tandam4 usiwe na shaka au kuchanganyikiwa. Mtafutaji huwa hakati tamaa kama siyo msimu huu hata msimu ujao utainuka tena. Kutokupata msimu huu siyo kwamba msimu.mwingine hutafanikiwa. Mafanikio yapo tele kama Mungu akikuacha hai na kama utaendelea kupambana na kujifunza kutokana na makosa.

Hata kama hutapata kabisa chukulia tu hiyo ni changamoto ya kujifunza kuelekea katika mafanikio.

Kumbuka " a smooth sea never makes an experienced sailor"
nimependa hapo mwishoni ulivyomalizia
 
Wakuu nawashukuruni sana kwa kunitia moyo japo wachache wanakatisha tamaa tuendelee kuomba
 
Wakuu mtu anaweza rukwa akili hivihivi.Katika kupambana na hali ya kiuchumi,mwaka huu niliamua kujilipua shambani nakulima takriban ekari 40 za maharage.Nikitumia gharama kubwa ktk mbegu na kulima.Sasa maharage yameota tena vizuri sana ila sioni dalili ya mvua kwa siku za karibuni, hivyo kupelekea kukauka kwa zao hilo.nasikia kuna wataalam wa asili wanaoweza saidia kunyesha mvua kama si tunguri{Afrika},basi nuclear[ulaya]nishaurini niende wapi
cc.mshana jr
" mamvi
Itabidi hapo ufanye mpango wakuyamwagilia lasivyo utakula sana hasara
 
pole mimi nimelima heka 10 za mahindi kila nikiamka napiga simu kuuliza kama kuna mvua kumbe hamna kitu ila kwa mtaalamu wa singida plz help me hata jinsi ya kutumia umwagiliaji maana kuna siku mtaona uzi kuwa pressure yangu imepanda kisa hamna mvua
Singida sehemu gani mbona maeneo ya iramba nasikia inanyesha
 
Hao wanaokukatisha tamaa ni wale ambao kamwe hawatakaa waendelee. Maneno wanayoandika ni reflection ya wivu wanaokuonea kwa sababu wewe umejaribu wao hawawezi. Mimi nililima eka tano za vitunguu kwa kilimo cha umwagiliaji. Lakini ule mto unapotoka mfereji naomwagilia nao umekauka. Jirani yangu alikuwa amechimba kisima cha mita 30 lakini nacho kimekauka. Tutaendelea. Kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi. Samora Machel aliyekomboa Msumbiji kwa mapambano dhidi ya mabeberu wa kikoloni alikuwa anasema: Aluta continua (vita vinaendelea) japo nchi yake ilishapata uhuru. No retreat no surrender!
 
Wakuu mtu anaweza rukwa akili hivihivi.Katika kupambana na hali ya kiuchumi,mwaka huu niliamua kujilipua shambani nakulima takriban ekari 40 za maharage.Nikitumia gharama kubwa ktk mbegu na kulima.Sasa maharage yameota tena vizuri sana ila sioni dalili ya mvua kwa siku za karibuni, hivyo kupelekea kukauka kwa zao hilo.nasikia kuna wataalam wa asili wanaoweza saidia kunyesha mvua kama si tunguri{Afrika},basi nuclear[ulaya]nishaurini niende wapi
cc.mshana jr
" mamvi
Kilimo cha kufa Na kupona! Hapa Ni kazi tu
 
Hao wanaokukatisha tamaa ni wale ambao kamwe hawatakaa waendelee. Maneno wanayoandika ni reflection ya wivu wanaokuonea kwa sababu wewe umejaribu wao hawawezi. Mimi nililima eka tano za vitunguu kwa kilimo cha umwagiliaji. Lakini ule mto unapotoka mfereji naomwagilia nao umekauka. Jirani yangu alikuwa amechimba kisima cha mita 30 lakini nacho kimekauka. Tutaendelea. Kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi. Samora Machel aliyekomboa Msumbiji kwa mapambano dhidi ya mabeberu wa kikoloni alikuwa anasema: Aluta continua (vita vinaendelea) japo nchi yake ilishapata uhuru. No retreat no surrender!
Mapambano ya kilimo Ni kutafuta blood pressure
 
Wakuu hali ya Nchi na unyeshaji wa mvua ni mzuri na hakuna njaa kama baadhi ya watu wanavyo wahadaa watanzania.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom