Nimelikosea Wapi? Naomba Mawazo Yenu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimelikosea Wapi? Naomba Mawazo Yenu.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kipeperushi, Dec 10, 2011.

 1. Kipeperushi

  Kipeperushi Senior Member

  #1
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wakuu wa janvi... Kimsingi bado sijapata picha kuhusu mrembo huyu. Kama ni member wa jf nitafurahi kama na yeye ata-coment, naamini nitamsoma tu kulingana na coment yake. Stori nzima iko hivi:- Niliwahi kupewa contact ya mrembo moja na rafiki yangu kwa ajili ya kujenga urafiki na binti huyu ambaye by that time alikuwa ni mkazi wa Mjini Magharibi, huko Zenj. Kwa kweli nia ya kujenga urafiki nae ilikuwa ni kwamba hatimae aje kuwa mke wangu. Idea hii niliipata toka kwa huyo rafiki yangu kwa sababu huyo mrembo alikuwa rafiki wa mke wa huyo rafiki yangu. Rafiki yangu alishawishika kuniunganisha na mrembo huyo kutokana na mapenzi ya binti huyo kutaka kuwa na mume ambae ni rafiki wa karibu na yeye (rafiki yangu). Baada ya kuanza mahusiano ya simu, mahusiano ambayo yalichukua takribani mwaka mmoja na zaidi kidogo kabla hatujaonana na huyo mrembo, hatimae huyo mrembo alinialika nimtembelee Zenj. Ki msingi wakati huo hali yangu ya kiuchumi haikuwa nzuri sana kwa sababu nilikuwa nje ya kazi kwa muda mrefu kidogo. Lakini kutokana na kampani ya marafiki zangu nilifanikiwa kudondoka Mjini Magharibi. Bahati nzuri wakati haya yote yanaendelea nilijitahidi kumwekea wazi mrembo huyo kuhusu hali halisi ya maisha yangu ilivyo. Mrembo huyo ambae kiasili ni mzaliwa wa Tanzania Bara, alikuwa anaishi Zenji kikazi. Jambo la ajabu ni kwamba wakati naelekea Zenji kwa mwaliko wake huyo bibie, nikiwa najua kama yeye ndie mwenyeji wangu, mrembo huyo alikataa kata kata nisifikie nyumbani kwake. Hivyo nililazimika kufikia hoteli, ambapo kutokana na gharama za kimaisha za huko Zenji nililazimika pia kufupisha muda wa ziara yangu toka wiki moja hadi 24hrs. Kwa kusema kweli nilitokea kumpenda sana huyu bibie, hasa kwa sababu hata yeye pia alionyesha kunipenda sana hata kabla hatujaonana. Baada ya muda kupita tukiwa tunaendelea na mawasiliano yetu kama kawaida tulipanga kukutana tena Dar es Salaam mimi nikiwa natokea Mbeya na yeye akiwa anatokea Zenji, ili tujadiliane mpango wa awali wa ndoa yetu, ikiwa ni pamoja na mimi kwenda kutambulika rasmi kwa wazazi wake Dodoma, nilichelewa kumlaki airport Dar. Kwa kweli sababu ya msingi ilikuwa ni mipango ya kipesa tu, ndio ilinichelewesha, kwakuwa katika ujio wake safari hii yeye ndiye alikuwa mwalikwa na mimi ndiye mwenyeji wake, na bahati mbaya kutokana na kuchelewa kwangu kufika Dar toka safari yangu ya Mbeya, mipango ya kipesa ilikuwa haijakaa sawa mpaka muda ambao ndege aliyosafiria huyo bibie ilipowasili Dar. Hata hivyo niliwasiliana nae na bahati nzuri baadae tulikutana nae baada ya yeye kuja mwenyewe kwa daladala. Baada ya tukio hilo mawasiliano yetu yamedhoofika kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba hata dalili za maendeleo ya mipango yetu ya ndoa zimepotea kabisa...! Ndugu zangu wanaJf, nimeuleta uzi huu hapa jamvini kwa sababu naamini kwamba hiki ni kiwanja cha watu wenye fikra pevu. Naomba mawazo yenu, lengo langu ni kurudisha uhusiano wangu na huyo bibie, tatizo langu ni kwamba nahisi mrembo amenidharau.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  katafute pesa kwanza....

  no finance no romance......

  no money no honey.....

  get it?
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  too much details, cant u cut it short.
   
 4. h

  hayaka JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hapendwi mtu yapendwa pochi!
   
 5. Kipeperushi

  Kipeperushi Senior Member

  #5
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pesa iko mbaya sana mkuu. Tatizo sio pesa, tatizo ni vipi narudisha uhusiano wetu kwenye nguvu yake ya awali. Mwanzoni alijua sina pesa na alinielewa, na sasahivi anjua nina pesa lkn kapoa kabisa, unanisoma vizuri the boss?
   
 6. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  tulia tafuta kazi, ukisha pata kibarua ndo mtafute, kwa sasa huwezi kumwelewa kwakuwa una mambo mengi kichwani. lakini kwanini usiongee na huyo aliyekuunganishia huyo mchumba? wao wanafahamiana hivyo aweza saidia zaidi , kuliko hapa JF
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  He he he he, mrembo kajilipia ndege afu unampandisha daladala?
  Ni sawa na kula msosi saafi afu unakula desert ya nhundwa, the ugliest fruit huko nakotoka.
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mkuu Nakushauri tafuta ajira kwanza! Maisha ni pamoja na pesa, hawa wenzetu wanaangalia sana security yao hasa mshiko wako.
  Ukpata kazi nzuri mtafute utasikia visingizio mia kidogo
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kiti cha basi..kishakaliwa na mwinginewe..
   
 10. CtVKiLaZA

  CtVKiLaZA JF-Expert Member

  #10
  Dec 10, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  fukara hana haki ya kupenda??
   
 11. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2011
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ...'they say woman never goes back financially, while man never goes back romantically'....land job/b'ness earn some dough, take her out...atleast she'll feel secure and jet to your strip for good...
   
 12. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #12
  Dec 10, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mkuu huyo atakuwa ameweka hela mbele kuliko kitu chochote kile so kuwa makini sana na ikiwezekana haraka sana iwezekavyo mpotezee sio lazima umuowe yeye,out there kuna wanawake wengi sana tena sana wanatafute waume wa kuwaowa jaribu ku play nao vizuri tu,achana na huyo atakuumiza kichwa tu hapo,.....
   
 13. Poriposha

  Poriposha JF-Expert Member

  #13
  Dec 10, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Otherwise its pain or tyt life!!!
   
 14. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #14
  Dec 10, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  he he he pole ndugu ila punguza jazba,kumbuka mtu asiyeweza kukuvumilia wakati una matatizo hakufai.....anyway,man up andf call her umuulize imekuwaje amebadilika gafla.inawezekana ana mwengine tayari
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Dec 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kama ishu yako ya kifedha haikumsumbua tangu mwanzo, (maana aliamua mwenyewe kujisafirisha kuja kukuona pamoja na kwamba alijua hujakaa vizuri kwenye maswala ya pesa) jua hajaridhika na kile alichokiona.
  Kwa kiasi fulani watu wanaokua wameingia kwenye mahusiano kabla ya kuonana hua hawaendelee kama walivyokua mwanzo baada ya kuonana uso kwa uso.Sijui kama mlishatumiana picha au la, ila jua kwamba kama hamkua mmetumiana basi ile picha aloyojijengea kichwani mwake haifanani kabisa na wewe ulivyo.Na kama mlishatumiana basi picha yako ilimpa picha ambayo ni tofauti kidogo na ulivyo. Kwa ufupi ni kwamba muonekano wako sio sawa na vile alivyotarajia.

  Na kama hiyo ndio hali halisi hamna unachoweza kufanya, labda kama unaweza kubadili muonekano wako ili umpe furaha ya macho kama ulivyompa ya moyo mpaka akaja kukuona.
   
 16. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #16
  Dec 10, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Tatizo lako nadhani ni kutokuwa responsible.Kwanza huwezi kung'ang'aniza kukutana na demu kwake wakati hamjuani na ndiyo kwanza mnakutana uso kwa uso.Inaelekea ulishawahi kumuonyesha vitabia vingine kama hivi kabla.Kama mlipanga muda mrefu umpokee airport halafu wewe unachelewa mpaka bibiye akapanda daladala,huoni kwamba umeshindwa kuonyesha tabia ya ukomavu?Inawezekana demu anapenda ku keep time na siyo kuwekana wekana mahala bila mpango.Kwako inaweza kuwa sababu ndogo lakini kuna watu hiki ni kigezo tosha cha kukuona hufai kuwa naye katika mahusiano.
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  yaani mtu kaja na ndege we ukamuacha apande daladala
  na unasema pesa unayo?
  ama sielewi au we muongo au huyo mdada ndo aliona humjali kabisa
   
 18. Poriposha

  Poriposha JF-Expert Member

  #18
  Dec 10, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kawaida kama ulianza uhusiano na mwanamke/mwanaume mapema may be tokea primary ila zinakuwa zile za kitoto toto lakini urafiki wenu unaendelea kudumu mwishowe mnapozidi kukua ndivyo na uhusiano/urafiki wenu unazidi kukua pia then mnakuja kujikuta mmekuwa wapenzi, hapa huwa kuna asilimia kubwa ya penzi lenu kuwa la dhati hata kama mmoja wapo hana standard nzuri ya maisha coz mlifahamiana mapema LAKINI ndugu yangu KIPEPERUSHI huyo binti ulimtamani kwanza kwasababu si rahisi kupenda kitu 100% kabla ya kukiona na inapelekea kushirikisha moja kati ya milango ya fahamu...so mwanzoni wewe haikuwa hivyo, pengine mwenzio alisha kujengea picha flani huyu mtu yuko hivi na vile so alivyo kuta haviko kama ile Imagination yake ni rahisi sana wewe kuwekwa pending..Kumbuka dimbwi la maji halipimwi kwa kuzamisha mguu... Umesha dumbukia sasa inakuwa tabu kwako kujiokoa ila Usikatee tamaa itajipa tu pengine si chaguo lako.

  "Is Not Easy by Lucky Dube"
   
 19. AMINATA 9

  AMINATA 9 JF-Expert Member

  #19
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 2,132
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  una akili sana ww
  hakuna haja ya ushauri mwingine zaidi ya huu mkuu alokupa ...mengine ni kuongezea tu ila la msingi ni hili
   
 20. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #20
  Dec 10, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  Mmh, umenitisha kwa hiyo statement maana mi pia inanihusu, but kwa upande wangu we do exchange pichaz na kila siku we skype everyday
   
Loading...