Nimekuwa mnyonge ghafla na akili imesimama, msaada tafadhali

muhitaji

Member
Mar 10, 2022
8
4
Habari ya muda huu wakuu....

Kuna huu upele ninao mikononi na sehemu kadhaa za mwili, ni mkavu hauwashi wala hautumbuki yaani umekuwa ni kama sehemu tuu ya ngozi yangu nikiamini kuna siku utaondoka kama ulivokuja japo ni miaka zaidi ya 10 sasa bado upo hivyo hivyo.

Nikizungumzia jinsi ulivyo anza ni kipindi nipo miaka 14 mitaa hyo ya balehe, mwili ulikuwa unawasha na vipele vidogo vibich vilitoka mikonon pia ni kama vilikua ukipasua hiki kinakuja kingine, nilienda hospitali wakati huo lakini hakuna majibu sahihi nilipata, nilishaogeaga sana detol na hata maalovela nilishapakaa sana lakini wapi. Mwisho vilipotea vyenyew ila ndo likabaki hilo balaa la hvyo vipele vikavu karibia sehemu kadhaa za mwili. Nikiwa mkubwa hivi nilivyo nilishawahi endaga hospitali moja ya rufaa kwa madaktari wa ngozi lakini bado sikupata jibu sahihi zaidi zaidi walinicheki magonjwa ya zinaa tu na kunipa dawa za kupakaa ila hakuna kilichobadilika.

Sababu ya kuja kwenu ndugu zangu ni jinsi ya upele huu sasa umeanza kumtoka huyu mdogo angu wa mwisho, yaani ukiangalia kuanzia dalili mpaka umri unaomuanza nao ni kama ilivyokuwa kwangu, sitaki kuimanisha na upande wa pili la hasha! Ila natamani kujua kama ni ishu ya kawaida ya kigenetic na pia kama dogo anaweza pata dawa ila walau yeye asifike nilipo mimi. Sahivi mama anamlaumu kwanini akikaa anajikuna ovyo, anaona dogo kama anajifanyisha lakini mimi kwakua nilishapitia hii hali naelewa ni ugumu gani anaupitia. Kifupi hana raha na sijajua kama atakuja kuwa nayo endapo akifikia hatua yangu, nahofia sana saikolojia yake kuvurugika kupitia hili. Mwenye msaada au ushauri tafadhali anisaidie.

Natanguliza shukrani wakuu..

#picha nne za mwanzo ni mkono wa dogo jinsi vinaanza na hyo picha ya mwisho(mkono mkubwa) ni mkono wangu.

IMG_20220310_181852.jpg
 
Mi naona ungempeleka kwa daktr mapema iki kama mnaweza kuuwahi ugonjwa itakua sahh
 
Mi naona ungempeleka kwa daktr mapema iki kama mnaweza kuuwahi ugonjwa itakua sahh
Tatizo mimi pia nilishaendaga hospitali enzi vinaanza nikiwa mdogo na hakuna kilichotokea, pia hata ukubwani nishawahi enda.

Lakini kama kuna hospitali unaifahamu au mtu yeyote anaifahamu anaweza nisaidia jina tukajaribu huko.
 
Tatizo mimi pia nilishaendaga hospitali enzi vinaanza nikiwa mdogo na hakuna kilichotokea, pia hata ukubwani nishawahi enda.

Lakini kama kuna hospitali unaifahamu au mtu yeyote anaifahamu anaweza nisaidia jina tukajaribu huko.
Duu polen mkuu ila mi sina nnapopajua nadhani wanaofahamu watakuja kukupa maelezo
 
Ulishawahi kutumia dawa gani

Kama ulishawahi nitajie kama bado nitakupa dawa mi vilinitesa mwaka dawa nimepata juzi
 
Wakuu nashukuru jumatatu kuna dawa tulibahatika kupata ni vidonge dogo anakunywa na walau matumaini yapo... Ndo nipo naendelea kumtazamia..
 
Pole sana, mimi naona usiende hospitali za mtaani, nenda hospitali kubwa kama Muhimbili umuone mtaalamu wa ngozi
 
Back
Top Bottom