Nimekutana na mwanamke, kanitoroka

Nimekutana na mwanamke, kanitoroka

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,931
Reaction score
4,549
Habari zenu wakuu,

Usiku wa kuamkia leo sitakaa niusahau katika maisha yangu,yaani tarehe 2/8/2015 saa 5:40 usiku katika hotel moja Mwanza ambayo naihifadhi jina kwa sababu za kibiashara,ni siku nyingi sana yapata miezi miwili nyuma nilikuwa nachat na mrembo mmoja.

Kwa kweli kama ni urembo Mungu alimjalia si mchezo,nikamtumia nauli akawa amekuja jana kutoka Dar,nilifurahi sana kumuona nikamchukua hadi katika hotel ambayo nilikuwa tayari nime book,kipato changu ni cha kuunga na super glue,ila nilikuwa na pesa ya kutosha maana nilibahatika kupata pesa nyingi hivi karibuni katika mazingira ya ajabu.

Nikiwa na mrembo wangu katika hotel lobby nikinywa bia na yeye Redbull tu alidai hatumii kilevi,ilipofika saa 5:40 nikamwambia tukalale,tulifanya mapenzi kama kawaida tukasinzia,nimekuja kushtuka saa 11 alfajiri hayupo kitandani,chooni hayupo,mlango wa chumba umefungwa,walinzi na wahudumu hawakumuona akitoka,hakuiba chochote,katoweka na mkoba wake tu hajaacha alama yoyote.

Kwa kweli nimechanganyikiwa
 
Hahaha acha uhuni fanya toba kwa Mungu wako.
 
mr Eric

shukuru mungu ulifanikiwa kumbomoa Bure bila kumlipa chake.je angepotea kablà hujajilia vyako ungejickiaje?
 
Last edited by a moderator:
poa tu, tafuta mwingine achana na huyo katoweka mwenyewe
 
Sasa baada ya kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha vip ulimtumia tena pm??
 
Back
Top Bottom