Nimekutana na Jini?

Mkuu kuhusu paka ni uwoga wako tu. Katika mazingira ya kawaida paka anayevuka barabara asubiri nini wakati mmeshapishana? Hivyo, wakati unamwangalia kwa kioo cha nyuma alikuwa ameshatokomea.
 
Dah... ajabu sana, eti mtu hadi unajua kuendesha gari lakini paka mweupe na mwanamke blonde aliyevaa nguo nyeusi hujawahi kuwaona live. Hii nchi ya ajabu sana
 
Ukiwa mitaa ya Kigoma na Shinyanga unaweza ukadata ukitembea usiku na gari! Unaweza kukutana na debe ktkt ya barabara linabingirika lenyewe ukilikwepa unalo
 
Kawaida tu kwenye dunia yenye Mungu na mashetani yapo tunashukuru hukudhurika poł sana punguza muda wa kurudi uciku km saa10
 
Hayo mambo yapo asee, siku moja nilikuwa natoka tunduma kwenda sumbawanga ilikuwa kama saa tisa usiku looh ghafla niliona fuso linageuza mbele yangu but Ile kukwepa sikuliona.... Kumbe niliokuwa nao hawakuona lolote
 
Ha ha haaaa.. Unaijua nauli ya kutoka dar hadi katavi? Half Katavi ni mlisha mifugo nyumbani kwa Pinda kule Mpanda so ticket ya ndege kwa duu kama wewe haezi gharamikia. Unless ujitolee kwa kila kitu


Mie hata kwa ngondi nitaenda tu nimekufa kwa huyo bwana
 
Wakati flan nikiwa kilwa masoko, usiku saa 3 mzee mmoja aliniomba lift nikamnyima, ndani ya sekunde 3 mguu wa kulia ukafa ganzi nikaanza kutumia mguu wa kushoto hadi nikafika nyumbani.
Nilijiuliza maswali mengi sana sikupata majibu
 
Kaa huamini sema "siamini kama majini yapo" period......... usielezee hapa kama wewe ndo msemaji wa mwisho! Majini yapo na yanafanya Yao kama kawaida, Mimi Ni mkristu nilikua siamini hizi mambo, but nilikutana na jini la kike Ana Ana, mpaka Leo linasumbua! Imani kama yako imepelekea shida kwangu coz ilichukua miaka 6 Kuja kuamini na hiyo Ni baada ya uaribifu mkubwa kutokea.....usipotoshe watu hapa, Leo watu wengi wanaishi na majini bila kujua yanaleta shida kubwa but vile wana Mawazo kama yako inawachukua muda kupambana nayo!
 
1. ... "Kuangalia nyuma kwa kutumia vioo sikumuona yule paka!"

Mida ya SAA 10 usiku, sidhani kama inawezekana uone kitu kilichopo nyuma eti kwa kutumia site-mirror or driver-mirror, it is never easy kwenye barabara ya giza! Unless barabara ina mataa au kuna gari lingine nyuma yako linakufuata.

2. Majini ni viumbe. Kama unaamini kuwa SHETANI yupo, basi amini pia kwamba majini yapo.

Haijawahi kunitokea, ila binafsi naamini mambo hayo yapo.

Mkuu nadhania ungekuwa ushapiga 'vyombo' + akili za usiku, walahi huyo blonde ungempa lift. Teh teh

-Kaveli-
 
Ukiwa mitaa ya Kigoma na Shinyanga unaweza ukadata ukitembea usiku na gari! Unaweza kukutana na debe ktkt ya barabara linabingirika lenyewe ukilikwepa unalo


Mkuu nimewahi kuisikia hiyo 'kanuni' mara nyingi sana, kwamba unapokuta kitu cha ajabu (au mtu) katikati ya barabara usiku mwingi, USIKWEPE! Nyosha tu ata kama unaenda kukigonga. Eti ukikikwepa tu ni kosa kubwa, inakula kwako, lazima upate bonge la ajari ama ufe.

Kumbe ina ukweli eeh?
 
Mh hii kitu ilishawahi mtokea mama yangu kipindi nikiwa mdogo, alikutana na nguruwe kama 80 hivi usiku na vimuri muri akapotea njia
 

Yes
Hata mchana
Kuna basi moja 3yrs back I think lilipata ajali maeneo ya singida baada ya kumkwepa bibi kizee
 
Nasikia jini huwa haonekani kwa reflected light eg mirror hata ukimpiga picha haitoki.
 
Ilitokea km 4yr ILIYOPITA tulipanda daladala Posta to GOMS majira ya mchana alipanda dada mmoja kakaaa seat ya nyuma kabisa pafyumu tamu, kuaribia darajani tutasikia shusha, kweli gari ikasimama hakuna aliyeshuka konda katukana kosa HATUA 2 tu anashika mfukoni Hana hata Mia na dada hatukkujua kashukia wapi, abiria wote seat ya nyuma walilala.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…