Nimekumbuka zamani

Nimeanza kusoma kwa shauku kweli, lakini nilipofika pale "eti kwa bibi tukawa tunavunja TV......" mudi wote wa kusoma ukaisha! Zamani tunayoijua sie sio hiyo!!!
 
Wewe hujafaidi kitu asee kama Kwa bibi yenu kulikuwa na geti na Tv huko sio vijijini ni mjini huko.


Raha ya kufaidi mwe huru sio kufungiwa kwenye geti. Hizo movie hata kwenu unaweza kuzitafta ukapata tu.



Sisi tulikuwa tunaenda Kwa bibi kijijini Tena miaka hiyo hata CD hazikuwepo

Kwanza wajukuu maximum ni 25 Hivi
Kwa bibi kulikuwa ng'ombe wengi zaidi ya 100!!

Babu alikuwa mkarimu mno na bibi pia.....tukifika tu tunachinja wenyewe mbuzi kubwa la kuchoma tu yaani linaishia juujuu tu kwenye shikome😂

Muda huo Kuna nyama za kubanika zimeshakauka mpaka basi zinaitwa ng'homele kisukuma ni mwendo wa kukata na kuloweka kwenye maji ya chumvi Kisha unakula...

Maziwa sio ya kuuliza ni muda wowote tu unajipimia ....basi wajomba kesho yake mnaenda nao kuchunga pamoja na kuwinda huko mnakutana Watoto shazi mnawinda sungura,digidigi na ndege kama kware ama kanga kama ni masika pamoja na kuchoma uyoga mnakula!!!(Hivi vitu vyote mjini huwezi pata hata ukiwa milionea)


Mkirudi kutoka machungani kulikuwa na bwawa mnaenda kuogelea weee acha tu hapa sio wanawake au wanaume mnaoga mtakavyo maana tulikuwa wadogo wakubwa ndo walikuwa hawaogi...


Mkirudi mtakula mpaka mnakula Tena. Siku ya sikukuu tulikuwa tunaenda kununulia juice cola zile zinaweka kwenye chupa za soda tulikuwa tuna nunua shilingi5 Hadi kumi!!

Michezo ilikuwa mingi sana kuumizwa ilikuwa sehemu ya michezo pia.

Kuna siku hamuendi kuwinda ni Tour ya kusaka matunda pori na kumletea bibi na Babu imagine tulikuwa tunaanza saa3 Hadi saa8 ndo tunarudi na mizigo ya matunda tumechoka mbaya😹😹

Sisi video kipindi chetu huwezi kuikuta Kijiji kiza hata Kwa diwani huikuti wewe ulichoelezea ni miaka ya 2007 hapa tu Kuna CD/DVD!!

Ukweli na miss sana enzi hizo Kuna mto maji tulikuwa tuna yaziba Kisha tunakamata samaki na vidagaa mkimaliza ni kuchoma hapohapo pilipili tulizia huko kula acha kabisa

Kuna matunda mizizi Yale uking'oa linakuwa kama muhoga ila Lina maji tupu matunda Yale hata nyani wanayapenda sana..

Ni vingi vya kuelezea hii ni miaka ya 1995-2002 Hivi acha kabisa
 
Umesimulia hadi nimejikuta natabasamu pekeyangu,. Ila maisha haya raha sana aisee ukiwa kwa wazee
 
Sisi tulikuwa wadogo sana tatizo, Tusingeweza vyote hivyo😃😄
 
Sisi kwetu likizo ilikua kama camp ya mateso ni mwendo kwenda shamba hapo kulima, kuchimba mashimo ya kupanda migomba, kutifua & kupalilia pia kusomba majani hapo mpaka likizo iishe ushakua mweusi mweusi hivi
Eti ushakuwa mweusi mweusi hivi,.
Ila we jamaa😂😂
 
Nyie mlikuwa wajukuu wa kishua. Mambo ya CD na snacks.

Sisi michezo yetu ilikuwa kombolela, na kuiba kamba za bibi tunafunga bembea zile za kwenye mti . Halafu kuna kwenda kuogelea mtoni huko na kula vimatunda pori.
Nimeshtuka aliposema zamani Kisha akataja vitu vya kisasa imagine tv,deki,CD hadi snack itakuwa mi nimeishi zama za mawe maana kwa bibi ilikuwa Raha unaenda nae shambani we unalima kidogo kidogo ukila mihogo
Ukirudi unasifiwa unajua kulima
 
Hivi Hawa nyonya damu ni kina nani??, ni watu au wadudu ?? Maana tulikuwa tunatishiwa sana hadi mtu unaogopa kutoka njee😆😂😂,.

Simu zilikuwa za wazazi mkuu,. Labda anapiga uncle anawapa binamu na mzee atanipa Mimi au labda dada angu tunaongea nao hivyo . Ni miaka ya 2014 kurudi huko nyuma ndiyo nilikuwa shule ya msingi enzi hizo
 
Nimeshtuka aliposema zamani Kisha akataja vitu vya kisasa imagine tv,deki,CD hadi snack itakuwa mi nimeishi zama za mawe maana kwa bibi ilikuwa Raha unaenda nae shambani we unalima kidogo kidogo ukila mihogo
Ukirudi unasifiwa unajua kulima
Eti zama za mawe😂😂😂,.
Maneno Huwa mnayatoaga wapi ?? ..

Ila sijui kwanini ukiwa unaishi kwa bibi Kuna Ile feeling ya comfortability hadi raha
 
Mkuu una miaka mingapi? Maana haya mazingira ni ya juzi hapo enzi za kikwete na unasema ulikuwa bado mtoto.
 
Hivi Hawa nyonya damu ni kina nani??, ni watu au wadudu ?? Maana tulikuwa tunatishiwa sana hadi mtu unaogopa kutoka njee😆😂😂,.

Wakubwa walikuwa wanasema ni watu...

Simu zilikuwa za wazazi mkuu,. Labda anapiga uncle anawapa binamu na mzee atanipa Mimi au labda dada angu tunaongea nao hivyo . Ni miaka ya 2014 kurudi huko nyuma ndiyo nilikuwa shule ya msingi enzi hizo

Kama ni 2014 kwenda nyuma basi ndio maana sijaona ni zamani ya ambayo mimi naiona zamani...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…