Nimekumbuka zamani

Nimekumbuka zamani

Leejay49

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2023
Posts
19,295
Reaction score
60,915
Habari za siku nyingi wanajukwaa….

Leo nimekaa nimejiwazia nikajikuta tu naona watoto wa sikuizi hawaenjoy kama ambavyo sisi zamani tulikuwa tunaenjoy,. Watoto wa saizi hawajui hata raha za kwenda likizo kwa bibi

Kwanza niseme tu kuwa bibi yetu kama wajukuu kabarikiwa nao ,. Mpaka sasa nadhani tunaweza kuwa hata tuko 50 na wengine ambao hatuwajui wanaweza kuwa hata 60 tumefika,. Imagine watoto 13 naa wote wana watoto sio chini ya wanne😄😄 ( ila hiii sio lengo la uzi ) ila mtaelewa kwanini nimesema hivi.

Kipindi kile ilikuwa likizo zote za sikukuu yaani December na ile likizo ya pasaka bibi yangu alikuwa anasisitiza wajukuu wotee tuende kumwona,. Yaani tulikuwa tunakuwa wengii kwa bibi ( kila kona unayopita ina mtu😅😅😅) ,. Na kwa vile tulikuwa wengi uharibifu kila siku kuanzia kwenye vyombo watu wanavunja,. mafundi TV sasa ndio kabisa mpaka bibi alikuwa anafungia ndani Tv zake zote hakuna kuangalia mpaka tuondoke,.

Sasa hapo ndio ile mikakati ilikuwa inaanza,. Ikikaribia likizo simu zinaanza kipigwa basi kila watu tunapangiana vitu vya kubeba,. Mie na dada angu tulikuwa tunabeba zetu TV ,. Binamu zetu wengine wa mwanza walikuwa wanabeba deki,. Wa arusha walikuwa wanabeba CD ( baasi hapo kila mtu ataagiza movie anazozitaka wao kazi yao kuzifatuta zilizotafsiriwa wanakuja na CDs Kibao ),. Wengine wa Dar ilikuwa kazi yao kubeba snacks ,.Wengine mipira midoli yaani Ili mradi tu kila mtu awe na chakubeba ….. Yaani ilikuwa tukifika kwa bibi ni kuangalia tu movie kuanzia asubuhi hadi usiku maana ilikua marufuku mtu kutoka nje ya geti😁😁😁

Usiku sasa kila watu wakishaingia chumbani kwao ni muda wa mastori hadi mida mibovu asubuhi hata hakunaa anayekumbuka alilala saa ngapi,. Kila watu wanasimulia stori za nyumbani shuleni yaani ilikuwa raha kipindi kile….

Bibi kwanza alikuwa ananunua sahani nyingi na vikombe vya plastiki kila mtu anamwandika jina kwenye sahani yake ( maana hataki kero mda wa kula zilikuwaga kelele sio za nchi hii watu wanachagua sahani maara vikombe mwisho wa siku kuvunja ),. Baaasi nguo zetu zote zilikuwa zinaandikwa majina ili akija mtu wa kufua kila mtu kambani anaenda kuanua nguo zilizoandikwa jina lake,. Ila bibi😂😂😂

Bibi alikuwa anatuambia yaani babu yenu wakati anajenga hii nyumba aliweka vyumba vikubwa kwajili yenu,. Yaani dream yake ilikuwa muwe mnakuja mnajaa kama hivi mnacheza mnampigia kelele,. Lakini kwa bahati mbaya alifariki bila kumwona mjuu wake hata mmoja ,. Yaani wote tumezaliwa akiwa kashakufa🥹🥹🥹

Kipindi kile ilikuwa hata kama likizo imekukuta mgonjwa utang’a ng’ania usafiri tu hivyo hivyo maana utajisi unyonge wenzio wote wako kwa bibi,.
Sema ndio hivyo sasa watu wenyewe wotee saizi washakuwa watu wazima ,. Wakuoa wameoa na wakuolewa wameshaolewa wengine toka waliendaga nje kusoma haawajarudi wenginee ndio hivyo yaani kwenda kwa bibi sikuizi laabda litokee tukio na hata mkienda hamui wengi na hata hao wachache kila mtu yuko busy na mambo yake yaani nyumba imepoozaaa😔😔 sio kama zamani…
 
Nyie mlikuwa wajukuu wa kishua. Mambo ya CD na snacks.

Sisi michezo yetu ilikuwa kombolela, na kuiba kamba za bibi tunafunga bembea zile za kwenye mti . Halafu kuna kwenda kuogelea mtoni huko na kula vimatunda pori.
 
Nyie mlikuwa wajukuu wa kishua. Mambo ya CD na snacks.

Sisi mizecho yetu ilikuwa kombolela, na kuiba kamba za bibi tunafunga benbea zile za kwenye mti . Halafu kuna. Kwenda kuogelea mtoni huko na kula vimatunda pori.
Lakini mlikuwa mnaaenjoy sanaa,. Ile tu mnakuwa wengi mnafurahia ila sikuizi hamna hii kitu
 
Lakini mlikuwa mnaaenjoy sanaa,. Ile tu mnakuwa wengi mnafurahia ila sikuizi hamna hii kitu
Eeeh ilikuwa raha sana . Ukiambiwa uondoke kabla ya wenzako unaona umekatiliwa sana yaani. Halafu kama ni december unakuta ni kipindi cha masherehe sijui kipaimara alooo😂😂😂tulikuwa tunavamia kila nyumba unakunywa nyumba hii fanta nyingine coka nyingine mirinda. Mkirudi nyumbani mmevimbiwa😂😂😂😂
 
Bibi alikuwa anatuambia yaani babu yenu wakati anajenga hii nyumba aliweka vyumba vikubwa kwajili yenu,. Yaani dream yake ilikuwa muwe mnakuja mnajaa kama hivi mnacheza mnampigia kelele,. Lakini kwa bahati mbaya alifariki bila kumwona mjuu wake hata mmoja ,. Yaani wote tumezaliwa akiwa kashakufa🥹🥹🥹
Life is so unfair 👆
Ni kweli, hata kwangu, hakukuwa na furaha kama ile ya kuwa around Bibi na babu na cousins, tulienjoy sana!
 
Eeeh ilikuwa raha sana . Ukiambiwa uondoke kabla ya wenzako unaona umekatiliwa sana yaani. Halafu kama ni december unakuta ni kipindi cha masherehe sijui kipaimara alooo😂😂😂tulikuwa tunavamia kila nyumba unakunywa nyumba hii fanta nyingine coka nyingine mirinda. Mkirudi nyumbani mmevimbiwa😂😂😂😂
Hahahh,. Yaani ni full burudani
Watoto wa sikuizi hawajui haya
 
Back
Top Bottom