Nimekumbuka miaka ya zamani!

Nimekumbuka miaka ya zamani!

Nguvu moja

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2017
Posts
3,371
Reaction score
2,715
Enzi ya Mwalimu kulikuwa na majengo kumbi maarufu jijini dar... Tukianzia pale Morogoro road na Msimbazi kulikuwa na kumbi maarufu ya wazee waliopigana vita na mkoroni jina la ukumbi ulikuwa unaitwa Tanzania Legion..

Ukitoka hapo mbele yake kidogo kama unalekea Akiba hiyo hiyo Morogoro road mkono wa kushoto, kulikuwa na Jengo kubwa la Umoja wa Vijana. Ukienda kati kati ya jiji kule posta mtaa kaluta na Zanaki miaka ya 80 kulikuwa na Club ya Washirika na hapo ndio ilipoanzishwa Washirika band mwaka 87 ukitoka hapo ukienda mbele hatua chache kidogo unaenda pale mtaa wa makunganya kulikuwa na jengo lililokuwa chini ya wizara ya afya lililokuwa linajishughulisha na Vizazi na Vifo lilikuwa linaenda kwa jina Kabidhi wasii wa serikali inayoshughulikia vizazi na vifo, sasa hivi hao ndio wanaitwa Rita

Ukitoka jengo hilo lililopo hapo mtaa wa makunganya kwa nyuma yake posta street kulikuwa na Mbowe Club miaka ya 80 ilivuma sana hii Mbowe club baadae mwishoni mwa miaka ya 90 ikaja kubadilishwa jina na kuitwa Club Bilicanas.

Bado tukiwa hapo hapo kati kati ya jiji ukienda pale Mtaa wa Maktaba na Upanga street karibu na kanisa la Wangrikana mbele kidogo utakutana na ukumbi maarufu uliokuwa unavuma sana miaka ya 80 ulioenda kwa jina la YMCA

Yapo mengi sana ya kukumbuka ikiwemo ukumbi wa Wapi wapis bar uliopo chang'ombe maduka mawili ilikuwa kila siku za weekend miaka ya 86 wanapiga Maquis band wana kamanyola bila jasho.

Mimi yangu kwa machache ninayoyakumbuka ni hayo kama muhenga mwingine mwenzetu anae kumbuka zaidi mambo kadhaa ya wakati huo enzi ya miaka 80 mpaka mwishoni mwa miaka 90 aendelee....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Threads ya wazee ngoja nibaki hapa nijue vitu adhimu
 
Back
Top Bottom