Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 374,171
- 866,429
Nimezila sana ila sijashiba sijavimbiwa wala sijanenepa... Unajua ni kwanini.. Bado sijapata ile yenyewe.... Jahazi la kaya linasukwasukwa.. Mapori yanafuka moshi... Mawimbi yanatamalaki... Sijatoka kitambi... Ngoja niendelee kula story....!!!
Tunakaribia kung'oa magugu yote ili tuanze kupanda, palizi haiko mbali... Hatutaki msimu wa mavuno ugubikwe na mavune kwasababu ya magugu yaliyokomaa pamoja na mavuno..... Lakini usitumie sumu kuua magugu... Yatafisha na vingine...
Natamani kula story nishibishe nafsi... Hivi kike tunachokitumia vibandani mwetu ni dawa ama ni sumu? Dawa inaponesha... Sumu inaangamiza....
Muangamize mmbu msumbufu kwa kofi, usitumie rungu utaharibu na vingine... Muangamize mmbu mkorofi kwa kofi usimpulizie dawa ya sumu ama sumu ya dawa... Hutamwangamiza yeye tu... Utawangamiza na wengine wenye faida kwako...
Buibui na utando wake atamnasa mmmbu mkorofi au nzi msumbufu.. Atanasa na wengine pia japo si papasi na kupe... Lakini atawanasa na kujifanyia chakula.... Huyu hafai kuangamizwa kwa dawa ya sumu ya mmmbu...
Usiposafisha nyumba yako na kuiweka kwenye mpangilio makini.... Hutokaa acha kutumia sumu kuangamiza wavamizi wapendao uchafu na kibanda kisichopangiliwa... Utamwangamiza kiroboto papasi yupo... Utamwangamiza kunguni.... Mmbu yuko... Utamwangamiza mbu wa dengu na mabusha mchana... Usiku mmbu wa malaria na homa kali yuko akikusubiri kwa hamu
Kofi moja hukomesha jeuri ya mmbu ila chunga alisilikwepe wala usitumie nguvu nyingi, usije ukaangamiza huku ukibaki na jeraha.... Dawa ya sumu haifai.... Inaangamiza na wasiohusika lakini ukikutana na mmbujanja atajibanza pahala salama usimuone katu wala dawa ya sumu isimpate barabara.....
Ni pale utakapodhani kuwa dawa ya sumu imefanya kazi yake barabara na kujiachia ukikenua usingizini na madenda juu... Mmbu janja toka kwenye maficho huibuka na kukupa michomo ya kibabe... Atakufaudu huku akikuachia virusi vyake vyote....!!!
Una mbadala wa kumuangamiza papasi
Una mbadala wa kumuangamiza kunguni
Una mbadala wa kumuangamiza inzi
Una mandala wa kumuangamiza mmbu....
Tumia mbadala kutomdhuru buibui na utando wake... Ana faida kwako huyu... Hana madhara nawe
Tumia mbadala huo kutomuangamiza sisimizi tena kwa rungu.... Hana shida nawe wala hana kelele zile za mmbu wala usumbufu wa nzi... After all hata akikuona hawezi kukukimbia kwakuwa hana mawaa...
Wenye dhambi ndio wakimbiao bila kukimbizwa... Na wajifichao bila kutafutwa....
Tukisafishe kibanda kwa tafakuri hekima, upendo na hofu ya Mungu.... Bila chuki, bila fadhaa bila kisasi bila kujikweza ili kikitakata tuserebuke kwa pamoja juu ya kaya yenye furaha na si kaya inayopendeza machoni lakini imesimama kwenye mafuvu na mifupa..... Ya wasio na hatia
Natamani kula story lakini kumepambazuka. ....!!!!