Nimekuja kwenu kuomba ushauri

Nimekuja kwenu kuomba ushauri

Hivi Kim Kardashian na Kanye West mahali yao anapokea nani?

Kuna ulazima sasa wa kuachana na tamaduni za kijinga kama hizi.
 
kweli 4m mahari? wazee wengine bana kujidharaulisha tu..we tafuta mzee mtu mzima ikibidi wawili waambie mahari mwisho laki 5 ndio uwezo wako..kama hawataki basi wamchukue binti yao na wakuachie watoto wako..uone kama watasubutu..khaa wazazi wengine nuksi kweli
sisi nyumbani kwetu mahari anataja mtoto wa kike mwenyewe mahari yake na anapewa mwenyewe muolewaji na wala mzazi hachukui senti, binti akiamua ndio anampa/anawagawia wazazi kidogo lkn sio lazima.. wazazi wao wanapewa sijui blangeti, shuka, jembe n.k ambayo hata haifiki elf 40

Ndiyo sababu hata kuachika ni rahisi sana kwa wino na karatasi yenye maneno matatu tuu!
 
Usiumize kichwa kaka. Hata kama ni 2M bado ni nyingi sana, wewe fanya vitu vya muhimu ambavyo vina muhusu mkeo, mama na baba tu. Kwenye mahali ya mke unatoa hata kilo 5 unakuwa umemaliza. Mahali haimalizwagi uliza wazee wetu wenye busara watakuambia.

Tulia na mkeo kulea watoto kwani ndicho muhimu kushinda vyote. Usimwogope baba mkwe wala nani, fanya kutokana na uwezo wako tu. Pole sana kwa kashikashi hizo.
 
Sisi wanawake bwana anapata fursa anajishauwa wkt ana watoto wake yy ndo muolewaji ana kukomoa jikaushe watashuka hd laki
 
Huyu mkeo hana huruma kabisa anakukomoa, hiyo mahali nikubwa sana na swala kama ni faini ya kumzalisha huwa ni ela kidogo tu unaweka kwenye bahasha, mpige binti mwambie nikitoa 4m ya mahali basi hakuna sherehe yoyote itakuwa kimnya kimnya uone jibu lake
 
Unaelimu ya chuo, hujui tofauti ya mzazi mwenzako na mke? Kweli Elimu yetu mchuzi juu. Turudi kwenye mada, zama za kuwaogopa baba/mama mkwe zimekwishapita, kinachotakiwa ni kuwaheshimu tu, waambie uwezo wako wa kutoa mahari, wakigoma achana nao, kuku umemfungia ndani na funguo unazo mwenyewe na mpaka sasa kakutagia mayai mawili. Wasi wasi wa nini? Wakikataa ofa yako ishi na huyo binti mtabariki ndoa hata uzeeni.
 
Back
Top Bottom