Nimekuja kwenu kuomba ushauri

Nimekuja kwenu kuomba ushauri

Uncle nlivo ona hata huyo mkeo hakufai make majibu anayo kupa hayaridhishi hata kidogo!!, lamsingi fungeni safari kama mwanzo nenda uwaambie kiasi hicho huna wala kukipata ni issue wao wataamua lakufanya! tena usizidishe laki 3!!..
 
Yaani ningekua wewe,namrudishaje hapo nyumbani nakuwa namtumia fedha za matumizi namwambia bado nafikiria kama nitamwoa au la!
Kwa kukusaidia mkuu, embu mrudishe kwao halafu usimwambie kama mmeachana uone Mambo yatakavyokuwa ila mbona mahari inapangwa kienyeji enyeji hivyo? Hawa hawajui maisha eeh?
 
4mill?kwa mahali tu!acha ujinga au anatoa madini hyo demu?ana uzuri gani;nenda katoe laki mbili tu kaka;mil hyo biashara?
 
Mahali siyo lazima ulipe yote kwa wakati mmoja! Wapoze na laki 5 weka kitu ndani then nitolee hiyo mpaka kifo. Yaani uwape 4M na still bado tu wataendelea kukupiga mizinga ukishaoa huyo mwanao.
 
kweli 4m mahari? wazee wengine bana kujidharaulisha tu..we tafuta mzee mtu mzima ikibidi wawili waambie mahari mwisho laki 5 ndio uwezo wako..kama hawataki basi wamchukue binti yao na wakuachie watoto wako..uone kama watasubutu..khaa wazazi wengine nuksi kweli
sisi nyumbani kwetu mahari anataja mtoto wa kike mwenyewe mahari yake na anapewa mwenyewe muolewaji na wala mzazi hachukui senti, binti akiamua ndio anampa/anawagawia wazazi kidogo lkn sio lazima.. wazazi wao wanapewa sijui blangeti, shuka, jembe n.k ambayo hata haifiki elf 40
 
4m hiyo mkomoeni wape laki 5 kaka zaidi ya hapo akupe risiti yenye VAT muulize huyo mkwe yeye alitoa sh gapi pengine anadaiwa anataka umlipie du! Hatari sana au ndio umeme umepanda
 
Habari wana MMU!
Pamoja na kwamba ni member jf na msomaji wa maoni yanayotolewa hapa MMU lakini sikuwahi kupost chochote hapa MMU,lakini leo nimekuja kwenu kuomba ushauri.

Mimi ni kijana niliye na mke na watoto wawili mapacha ingawa bado sijafunga ndoa.Huyu mke alikuwa ni mpenzi wangu wa siku nyingi. Baada ya mimi kumaliza chuo nikawa nimepata kazi mkoa tofauti na aliko mpenzi wangu,sasa katika kuondoa upweke nikawa namtumia nauli anakuja kunitembelea.Baada ya muda akiwa amerudi kwao akaniambia ana ujauzito, kwa kweli sikubisha ingawa kuoa nilikuwa bado hii inatokana na kuwa nilikuwa bado sijajipanga kabisa.

Baada ya kama wiki moja hivi akaniambia anataka atoe ule ujauzito mimi nilimkatalia na bahati nzuri certificate yake aliyokuwa anasomea alikuwa ametoka kufanya mtihani wa mwisho,ikabidi nimwambie aje kwangu. kipindi ninaye sasa akawa anatafutwa na baba yake ingawa mama yake alikuwa anajua na hii inatokana na kwamba baba mkwe na mama mkwe walishatengana kwa hiyo wako mikoa tofauti, na mimi nilikuwa nawasiliana na mama mkwe ila baba mkwe nilikuwa siwasilani naye kutokana na kuogopa, ila mama mkwe akawa ananisisitizia niende nikajitambulishe na nili mhakikishia mama mkwe kuwa nitaenda.

Baada ya miezi tisa mke wangu akajifungua mapacha na wakati huo baba mkwe alishajua mtoto wake yuko kwa mwanaume na akawa anawasiliana na mtoto wake huku akimwambia anipeleke nikajitambulishe.

Ikabidi tupange kuwa watoto wakikomaa inanilazimu niende kwa baba mkwe na hii ilikuwa tumepanga mwezi december 2013.Ghafla kwa bahati mbaya mama watoto akafiwa na baba mdogo wake kwa hiyo hapa sikuwa na jinsi ikabidi tuongozane wote kwenda msibani huku mawazo tele nikimwogopa baba mkwe.

Baada ya kufika msibani huku nikiwa nimeongozana na kaka yangu pamoja na watu wengine watatu tulipokelewa vizuri.Baada ya muda ukaanza utambulisho, watu wangu wakajitambulisha kuwa sisi ndo tumezaa na mwanao na ndo tunakaa naye, upande wao wakakubali na tukaweka bahasha yenye pesa ndani.

Sasa akili yao yote kutokana na kuwa nimekaa na mtoto wao kwa muda kama mwaka mmoja na nusu bila kujitambulisha basi wakajua nimekwenda kumaliza kila kitu yaani mahari wakati mimi haikuwa hivyo ila nilijua watanipimia kiasi cha mahari halafu ndo tujadiliane muda wa kutoa.

Baada ya muda wakaja na kiasi cha jumla ya shilingi milioni 4 .Tukawaambia hatujajiandaa kwa kutoa mahari, tuliwaambia hivi tukitaka kwanza watupe muda halafu baada ya hapo ndo tujitetee kiasi hicho kipungue,lakini wakaja juu huku wakisema tuna wadharau.Ikabidi tuwape akina shangazi mtu ambao ndo walikuwa wako juu kiasi cha sh. elfu 50 kama tu kupooza.

Baada ya hapo ikabidi watuambie mwakani(2014) mahari tunatakiwa kutoa, kutokana na hali ilivyokuwa pale ikabidi tukose hata kujitetea ikabidi tukubali tu. Baada ya kama siku mbili nikamfuata mke wangu na nikarudi naye sehemu ninayofanyia kazi huku baba mkwe akisisitiza mahari.

Sasa 2014 ndo imeingia na baba mkwe anataka mahari lakini kwa kiasi cha sh.milioni 4 ni nyingi sana na nimejaribu kumuuliza mke wangu kuwa labda aongee na akina shangazi lakini jibu alilo nipa mke wangu kwa kweli lilinihuzunisha.
Mke wangu ananiambia nitajuana na ukoo wangu hapa akimaanisha kuwa eti mahari labda nitalipiwa na mtu yeyote kwenye ukoo wangu,wakati siyo kweli ,mke wangu anajua hali halisi kuwa mahari itatokana na mshahara wangu kwa kuwa baba alishafariki.

Kwa hiyo wana MMU ninaomba ushauri nianzie wapi ili hicho kiasi kiweze kupungua angalau hata milion 2.

Mkeo ni mtu kutoka mkoa gani?
 
kweli 4m mahari? wazee wengine bana kujidharaulisha tu..we tafuta mzee mtu mzima ikibidi wawili waambie mahari mwisho laki 5 ndio uwezo wako..kama hawataki basi wamchukue binti yao na wakuachie watoto wako..uone kama watasubutu..khaa wazazi wengine nuksi kweli
sisi nyumbani kwetu mahari anataja mtoto wa kike mwenyewe mahari yake na anapewa mwenyewe muolewaji na wala mzazi hachukui senti, binti akiamua ndio anampa/anawagawia wazazi kidogo lkn sio lazima.. wazazi wao wanapewa sijui blangeti, shuka, jembe n.k ambayo hata haifiki elf 40

Mia mia
 
Huyo mkweo asikuchoshe

Kwanza mahari sio lazima iishe

Halafu milioni 4 anatafuta mtaji

Wagonge laki tano waambie nyengine mtamalizia then kaandikisheni mfunge ndoa

Wazazi wengine wanadhani shoda zao ItamaliWa na mahari???
 
Dah, sipati picha, ingekuwa mimi ningefanya kituko cha mwaka. Anyway, tunatofautiana, mimi nilitoa 150,000/= tena miezi sita baada ya ndoa. Siku nimeenda kujitambulisha, cha kwanza walisema vijana wamependana wakafunge ndoa, hayo mengine baadaye.

Siku hizi watu wanatafuta kuolewa, huyo naona anatafuta kuachika
 
Wanataka kukugeuzaa mtaji,kwan mahali nyingi inasaidia nin mahusiano yenu
Wewe cha kufanya piga kimyaa mpaka wanyookee
 
Dadangu alienda kutambulisha mchumba, na ukoo ukampangia mahari kubwa sana, kijana akawa mkali , na kususa ,kesho yake asubuhi sana wazzee walienda kumgongea wakimwomba asibadili uamuzi wake, na mahari waliyokuja kuipokea haikufika hata robo ya ile waliokua wanaitamani. Jaribu njia hii inaweza kukusaidia, sometimes wazee wetu wanakuaga na tamaa sana pasibokujua uwezo wa mtu, wakishajua kijana ana kazi na kagari kamoja bassss watakuliza kwenye mahari. Ila ukiona mkeo anakua upande wa wazee wake ujue hilo ni tatizo, anatakiwa awe upande wako maana yeye ndio anajua uwezo wako.
 
wote ni wanyakyusa wa mbeya ingawa yeye baba yake ni wa tukuyu na mama yake ni wa dodoma na yeye kakulia dodoma na mimi ni wa kyela

Kwa wanyakyusa mashangazi ndio wanaletaga ujinga. Tena usiombe wawe maskini, watataka kutajirika kupitia kwako. Waambie wakupe mchanganuo wa hiyo mahali uone wamepanga nini. Na njia rahisi ni kutoa vitu vya muhimu tu! Mfano mkaja wa mama, blanketi, majembe, mashuka, mbuzi wa mjomba, mbuzi wa shangazi. Hivyo vingine unawaambia najipanga ntakuja kuleta na ndio mwisho wa mchezo. Wala hata wasikuumize kichwa
 
Wakati mwingine hizi mira zetu za Kiafrika zinaturudisha nyuma sana. Baba kashaona mtaji huo! We kauka endelea kula vitu, mama akitaka kuleta za kuleta unamwambia utaacha watoto hapa umfuate baba yako. Hapa mzazi inabidi awe mpole tu mwanae kashatoa utamu na thamani imeshapungua.
 
Back
Top Bottom