Nimekuja kwenu kuomba ushauri

Nimekuja kwenu kuomba ushauri

Duuh ngoja na mim nitazaa majike tupu alafu mahari yake....lazima niwe mengi mdogo
 
Na wakipatwa na shida wanakimbiaga kweli kukutafuta. Nachukia sana wazazi wanaopanga mahali isiyokuwa realistic. Mi sinunui mtu, nahitaji mtu ambaye tutaishi na kuyasogeza maisha mbele. Haya mambo ya kutaka kutajirika kupitia watoto wa kike ni upuuzi mtupu.
 
Mahari mil..4? Duh! Langu jicho!!
Umeona eeeeh wazazi hawa walivyo wabaya khaa halafu baadae wakiwa na shida kijana wa watu akiwafungia viooo wataanza kulalamika na hata mke hatokumbuka haya. Wanasahau kabisa kwamba huyu anaenda kuwa kijana wao. Halafu binti anashangaza hicho anachoshadadia utazani pesa kaambiwa atapewa yeye yote..
 
Yaani huyo unayemuita mkeo (ukweli ni kwamba ni mzinzi mwenzio tu) ni wa kushikisha adabu tu. Anapata wapi ujasiri wa kuwa upande wa familia yake kwenye suala kama hili???!!! Hivi ukiamua kumwambia unajua nini, mimi kuoa kwa sasa naona bado, inabdi kwanza nijipange, ataenda wapi?? Watu wengine wanacheza na maisha aisee.

Kwa upande mwingine huyo mwanamke sio. Kama ishu ya msingi kama hiyo anashindwa kushirikiana na wewe, tegemea matatizo zaidi mbele ya safari hata kama ukifanikiwa kulipa hiyo 4M. Kuna mdau hapo juu kakushauri siku nyingine ufuate utaratibu wa Mungu, mimi pia naungana naye.
 
Aache ujinga, badala ya kukusaidia mpunguze hizo gharama maisha yaendelee yeye anapigia msumari?

Mpige biti, mwambie huna hiyo mil.4 kwahiyo hamna utambulisho rasmi, kuhalalisha ndoa wala harusi mpaka siku utakapoipata na hujui hiyo siku itakuwa mwaka gani.
nimeona like tu haitoshi! i LIKE comment yako!
 
Ungeuliza vizuri labda milioni nne ya Zimbabwe...
 
Aache ujinga, badala ya kukusaidia mpunguze hizo gharama maisha yaendelee yeye anapigia msumari?

Mpige biti, mwambie huna hiyo mil.4 kwahiyo hamna utambulisho rasmi, kuhalalisha ndoa wala harusi mpaka siku utakapoipata na hujui hiyo siku itakuwa mwaka gani.
Ukizingatia mwanamke mwenyewe alishatoa wazo la kutoa mimba..... Sijui hao watoto anawaangaliaje yailahi toba??? Hivi wakifa atalia kweli??????
 
Habari wana MMU!
Pamoja na kwamba ni member jf na msomaji wa maoni yanayotolewa hapa MMU lakini sikuwahi kupost chochote hapa MMU,lakini leo nimekuja kwenu kuomba ushauri.

Mimi ni kijana niliye na mke na watoto wawili mapacha ingawa bado sijafunga ndoa.Huyu mke alikuwa ni mpenzi wangu wa siku nyingi. Baada ya mimi kumaliza chuo nikawa nimepata kazi mkoa tofauti na aliko mpenzi wangu,sasa katika kuondoa upweke nikawa namtumia nauli anakuja kunitembelea.Baada ya muda akiwa amerudi kwao akaniambia ana ujauzito, kwa kweli sikubisha ingawa kuoa nilikuwa bado hii inatokana na kuwa nilikuwa bado sijajipanga kabisa.

Baada ya kama wiki moja hivi akaniambia anataka atoe ule ujauzito mimi nilimkatalia na bahati nzuri certificate yake aliyokuwa anasomea alikuwa ametoka kufanya mtihani wa mwisho,ikabidi nimwambie aje kwangu. kipindi ninaye sasa akawa anatafutwa na baba yake ingawa mama yake alikuwa anajua na hii inatokana na kwamba baba mkwe na mama mkwe walishatengana kwa hiyo wako mikoa tofauti, na mimi nilikuwa nawasiliana na mama mkwe ila baba mkwe nilikuwa siwasilani naye kutokana na kuogopa, ila mama mkwe akawa ananisisitizia niende nikajitambulishe na nili mhakikishia mama mkwe kuwa nitaenda.

Baada ya miezi tisa mke wangu akajifungua mapacha na wakati huo baba mkwe alishajua mtoto wake yuko kwa mwanaume na akawa anawasiliana na mtoto wake huku akimwambia anipeleke nikajitambulishe.

Ikabidi tupange kuwa watoto wakikomaa inanilazimu niende kwa baba mkwe na hii ilikuwa tumepanga mwezi december 2013.Ghafla kwa bahati mbaya mama watoto akafiwa na baba mdogo wake kwa hiyo hapa sikuwa na jinsi ikabidi tuongozane wote kwenda msibani huku mawazo tele nikimwogopa baba mkwe.

Baada ya kufika msibani huku nikiwa nimeongozana na kaka yangu pamoja na watu wengine watatu tulipokelewa vizuri.Baada ya muda ukaanza utambulisho, watu wangu wakajitambulisha kuwa sisi ndo tumezaa na mwanao na ndo tunakaa naye, upande wao wakakubali na tukaweka bahasha yenye pesa ndani.

Sasa akili yao yote kutokana na kuwa nimekaa na mtoto wao kwa muda kama mwaka mmoja na nusu bila kujitambulisha basi wakajua nimekwenda kumaliza kila kitu yaani mahari wakati mimi haikuwa hivyo ila nilijua watanipimia kiasi cha mahari halafu ndo tujadiliane muda wa kutoa.

Baada ya muda wakaja na kiasi cha jumla ya shilingi milioni 4 .Tukawaambia hatujajiandaa kwa kutoa mahari, tuliwaambia hivi tukitaka kwanza watupe muda halafu baada ya hapo ndo tujitetee kiasi hicho kipungue,lakini wakaja juu huku wakisema tuna wadharau.Ikabidi tuwape akina shangazi mtu ambao ndo walikuwa wako juu kiasi cha sh. elfu 50 kama tu kupooza.

Baada ya hapo ikabidi watuambie mwakani(2014) mahari tunatakiwa kutoa, kutokana na hali ilivyokuwa pale ikabidi tukose hata kujitetea ikabidi tukubali tu. Baada ya kama siku mbili nikamfuata mke wangu na nikarudi naye sehemu ninayofanyia kazi huku baba mkwe akisisitiza mahari.

Sasa 2014 ndo imeingia na baba mkwe anataka mahari lakini kwa kiasi cha sh.milioni 4 ni nyingi sana na nimejaribu kumuuliza mke wangu kuwa labda aongee na akina shangazi lakini jibu alilo nipa mke wangu kwa kweli lilinihuzunisha.
Mke wangu ananiambia nitajuana na ukoo wangu hapa akimaanisha kuwa eti mahari labda nitalipiwa na mtu yeyote kwenye ukoo wangu,wakati siyo kweli ,mke wangu anajua hali halisi kuwa mahari itatokana na mshahara wangu kwa kuwa baba alishafariki.

Kwa hiyo wana MMU ninaomba ushauri nianzie wapi ili hicho kiasi kiweze kupungua angalau hata milion 2.
anza na huyo binti kwa mkwala kama alivyosema lizzy, halafu fuatia na mama mzazi wa binti kwakua umesema yeye mlikua mnawasiliana kabla ya baba mkwe na ueleze vile ambavyo hali yako kiuchumi ilivyo! ikishindikana tafuta watu wazima wa ukoo wako ama sehemu unayoishi huwezi kukosa wenye busara zao washirikishe hapatakosekana solutions ikiwezekana tafuta wazee wa kabila la baba mkwe!
 
Ushauri wangu ni kwamba kama wewe na,mkeo mnapendana hiyo ni hatua muhimu.

Mahari sio mauzo ya mke bali ni heshima tu kwa wazazi. Hivyo hakuna mahari kubwa wala ndogo.

Mahari inatolewa kutokana na uwezo wa familia. Pia si lazima uitoe iishe yote.

Nakushauri kama wazazi wamegomea mil 4 basi kibaliana nao. Ila waambie kwa sasa huna uwezo wa kumaliza yote. Waeleze kiasi ulichonacho na kiasi kingine utamalizia baadae.

Watu wengi hata matajiri sana hawajamaliza mahari walizopangiwa.

Asante
 
a bride price does not validate the marriage, its only a free will, and her response to you its a green light, am doubt if you will once regret to cohabit with her, you better hit the road and live a celibacy life its so sweet and stress free
 
Mtafute mtu wa familia yao mwenye busara mpe hali halisi kwamba,ina lski tano tu.

Then hiyo diku unalipa laki 4 laki wata kudai huyo mzee kwanza inaonekana anamatatizo yeye nwenye mke amemshindwa wameachana je alilipa mahari kiasi kikubwa hivyo.
 
4mil siyo mahari peke yake, hapo umepigwa na faini, ungemuoa kabla ya kumzalisha ungeambiwa laki mbili au tatu, tatizo hapo umezalisha.

Jaribu kubargain nao, wakigoma toa kiasi kidogo na kinacho baki mpaka Yesu arudi.
 
Ukizingatia mwanamke mwenyewe alishatoa wazo la kutoa mimba..... Sijui hao watoto anawaangaliaje yailahi toba??? Hivi wakifa atalia kweli??????
ha!ha!haa Aspirin umenchekesha kweli loh!hajielewi huyo dada mwenzangu
 
afu unakuta mtu unakaa nyumba ya kupanga afu hawa wakwe wanataka pesa 4m,hapo kama mim utaishia kuniona hivi hivi sitoe hata mia si wanafanya watu B.O.T
 
Kwa wanyakyusa mashangazi ndio wanaletaga ujinga. Tena usiombe wawe maskini, watataka kutajirika kupitia kwako. Waambie wakupe mchanganuo wa hiyo mahali uone wamepanga nini. Na njia rahisi ni kutoa vitu vya muhimu tu! Mfano mkaja wa mama, blanketi, majembe, mashuka, mbuzi wa mjomba, mbuzi wa shangazi. Hivyo vingine unawaambia najipanga ntakuja kuleta na ndio mwisho wa mchezo. Wala hata wasikuumize kichwa

sawa mkuu nashukuru kwa ushauri
 
Hahahahaa, Lizzy nimekupenda ghafla (ila kama wewe ni mwanamke!)
Aache ujinga, badala ya kukusaidia mpunguze hizo gharama maisha yaendelee yeye anapigia msumari?

Mpige biti, mwambie huna hiyo mil.4 kwahiyo hamna utambulisho rasmi, kuhalalisha ndoa wala harusi mpaka siku utakapoipata na hujui hiyo siku itakuwa mwaka gani.
 
Last edited by a moderator:
pole sn mkuu hapo wa kupewa dozi ni huyo mwanamke km vp achape lapa kwa maisha bora yapi ya kutoa 4m as mahari hapa tz?! pima kauli za mkeo pia uckute naye kakugeuza mtaji coz nijuavyo mm mwanamke ana nguvu kwenye maamuzi ya mahari, ye hawazi hao mapacha wake watakula nn anawaza kuwapa kina shangazi 4m? soo stupid!
 
Bwana mdogo pole kwa yote! Wewe ndo BABA chukua maamuzi ambayo uko na maslahi nayo Kwamaana yackuumize!
 
Back
Top Bottom