Nimekuja kwenu kuomba ushauri

Nimekuja kwenu kuomba ushauri

man dunga

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2013
Posts
3,521
Reaction score
6,069
Habari wana MMU!
Pamoja na kwamba ni member jf na msomaji wa maoni yanayotolewa hapa MMU lakini sikuwahi kupost chochote hapa MMU,lakini leo nimekuja kwenu kuomba ushauri.

Mimi ni kijana niliye na mke na watoto wawili mapacha ingawa bado sijafunga ndoa.Huyu mke alikuwa ni mpenzi wangu wa siku nyingi. Baada ya mimi kumaliza chuo nikawa nimepata kazi mkoa tofauti na aliko mpenzi wangu,sasa katika kuondoa upweke nikawa namtumia nauli anakuja kunitembelea.Baada ya muda akiwa amerudi kwao akaniambia ana ujauzito, kwa kweli sikubisha ingawa kuoa nilikuwa bado hii inatokana na kuwa nilikuwa bado sijajipanga kabisa.

Baada ya kama wiki moja hivi akaniambia anataka atoe ule ujauzito mimi nilimkatalia na bahati nzuri certificate yake aliyokuwa anasomea alikuwa ametoka kufanya mtihani wa mwisho,ikabidi nimwambie aje kwangu. kipindi ninaye sasa akawa anatafutwa na baba yake ingawa mama yake alikuwa anajua na hii inatokana na kwamba baba mkwe na mama mkwe walishatengana kwa hiyo wako mikoa tofauti, na mimi nilikuwa nawasiliana na mama mkwe ila baba mkwe nilikuwa siwasilani naye kutokana na kuogopa, ila mama mkwe akawa ananisisitizia niende nikajitambulishe na nili mhakikishia mama mkwe kuwa nitaenda.

Baada ya miezi tisa mke wangu akajifungua mapacha na wakati huo baba mkwe alishajua mtoto wake yuko kwa mwanaume na akawa anawasiliana na mtoto wake huku akimwambia anipeleke nikajitambulishe.

Ikabidi tupange kuwa watoto wakikomaa inanilazimu niende kwa baba mkwe na hii ilikuwa tumepanga mwezi december 2013.Ghafla kwa bahati mbaya mama watoto akafiwa na baba mdogo wake kwa hiyo hapa sikuwa na jinsi ikabidi tuongozane wote kwenda msibani huku mawazo tele nikimwogopa baba mkwe.

Baada ya kufika msibani huku nikiwa nimeongozana na kaka yangu pamoja na watu wengine watatu tulipokelewa vizuri.Baada ya muda ukaanza utambulisho, watu wangu wakajitambulisha kuwa sisi ndo tumezaa na mwanao na ndo tunakaa naye, upande wao wakakubali na tukaweka bahasha yenye pesa ndani.

Sasa akili yao yote kutokana na kuwa nimekaa na mtoto wao kwa muda kama mwaka mmoja na nusu bila kujitambulisha basi wakajua nimekwenda kumaliza kila kitu yaani mahari wakati mimi haikuwa hivyo ila nilijua watanipimia kiasi cha mahari halafu ndo tujadiliane muda wa kutoa.

Baada ya muda wakaja na kiasi cha jumla ya shilingi milioni 4 .Tukawaambia hatujajiandaa kwa kutoa mahari, tuliwaambia hivi tukitaka kwanza watupe muda halafu baada ya hapo ndo tujitetee kiasi hicho kipungue,lakini wakaja juu huku wakisema tuna wadharau.Ikabidi tuwape akina shangazi mtu ambao ndo walikuwa wako juu kiasi cha sh. elfu 50 kama tu kupooza.

Baada ya hapo ikabidi watuambie mwakani(2014) mahari tunatakiwa kutoa, kutokana na hali ilivyokuwa pale ikabidi tukose hata kujitetea ikabidi tukubali tu. Baada ya kama siku mbili nikamfuata mke wangu na nikarudi naye sehemu ninayofanyia kazi huku baba mkwe akisisitiza mahari.

Sasa 2014 ndo imeingia na baba mkwe anataka mahari lakini kwa kiasi cha sh.milioni 4 ni nyingi sana na nimejaribu kumuuliza mke wangu kuwa labda aongee na akina shangazi lakini jibu alilo nipa mke wangu kwa kweli lilinihuzunisha.
Mke wangu ananiambia nitajuana na ukoo wangu hapa akimaanisha kuwa eti mahari labda nitalipiwa na mtu yeyote kwenye ukoo wangu,wakati siyo kweli ,mke wangu anajua hali halisi kuwa mahari itatokana na mshahara wangu kwa kuwa baba alishafariki.

Kwa hiyo wana MMU ninaomba ushauri nianzie wapi ili hicho kiasi kiweze kupungua angalau hata milion 2.
 
Aache ujinga, badala ya kukusaidia mpunguze hizo gharama maisha yaendelee yeye anapigia msumari?

Mpige biti, mwambie huna hiyo mil.4 kwahiyo hamna utambulisho rasmi, kuhalalisha ndoa wala harusi mpaka siku utakapoipata na hujui hiyo siku itakuwa mwaka gani.
 
Haya mambo ya mahari za kukomoana ni mabaya sana. After all huyo mkeo hujamjua vizuri... Ngoja ufunge ndoa ndio utamjua vizuri. Laiti Mungu angekuwa anatuonyesha mbele miaka kadhaa hali itakuweje... Pengine usingekubali kabisa hata kuoa. Mke anatakiwa afungamane na wewe katika kukusaidia ninyi kuungana na kutengeneza familia. Ukishaona anashabikia mambo ya kwao ujue hapo hamna kitu. Sasa cha msingi we nenda huko ukweni waambie hiyo hela huna na swala la kuoa basi. Nakuambia watakubembeleza hata kwa mahari ya laki 3. Haya mambo tumeshayaona sana cha msingi,ni kujiamnini tu.
 
We HIKAUSHE TU! Tena mkeo/ suria akikuuliza mambo ya ndoamwambie 4M IS NOT A JOKE! Bado unatafuta! Hivo hivo. Siku ukiamka vizuri mwambie MKABARIKI NDOA KANISANI (Kama wakristo!). Ndo nitoleeeeee hiooo! Mi namshangaa sana mtu ana watoto mapacha ukimuacha ataenda wapi? Badala afosi ndoa anataka kutajirika na mahari! Atashaaaaaaa!

Wala usijistress wewe ndo umeshika mpini! Kama vipi mzalishe tena! Au tuma MSHENGA akawapige tantalila
 
Aisee!! ngoja waje waliokwisha yapitia haya mambo ya ndoa kwa kina!!
 
kwani ukiwaambia huna hyo m4 watafanyaje? na tayari binti yao ana bendi ya mapacha? by zeway mil 4 nyingi, bora nikanunue ka corola kangu nipige nacho misele ntawapata wengi tu, kuliko kwa m1.
 
kausha tu mtu wangu....baba mkwe anataka mahari kwani ye ndo anaenda kuolewa?.....anakomaa wakati bintiye kaishazaa.,,we nyuti itajulikana mbele huko..
kitakachotokea atamchukua bintie ataanza kumhudumia yeye na wajukuu mwishoe atashindwa utaitwa uta mchukua mkeo bureeeeeeeeeeeeeeee..........
siku nyingine usifuate utaratibu wa shetani,...fuata utaratibu wa Mungu hutadhurika kamwe........
 
Mkuu pole sana kwa yaliyokukuta ila cha msingi nenda na kiasi ulichonacho hawatakataa mkuu, hiyo ni mikwara mkuu wape 1 milion halafu waambie hiyo nyingine utamalizia
 
Duh, huyo mzee anataka kutajirikia kwako., Mkuu kama mkeo naye anaonekana ku-side na baba yake mrudishe kwao waambie ngoja kwanza utafute hiyo m4c kwanza. Ukitoka hapo usigeuke nyuma kamwe maana huyo mwanamke hakufai. Ila uwe unatuma hela ya matumizi ya watoto.
 
We HIKAUSHE TU! Tena mkeo/ suria akikuuliza mambo ya ndoamwambie 4M IS NOT A JOKE! Bado unatafuta! Hivo hivo. Siku ukiamka vizuri mwambie MKABARIKI NDOA KANISANI (Kama wakristo!). Ndo nitoleeeeee hiooo! Mi namshangaa sana mtu ana watoto mapacha ukimuacha ataenda wapi? Badala afosi ndoa anataka kutajirika na mahari! Atashaaaaaaa!

Wala usijistress wewe ndo umeshika mpini! Kama vipi mzalishe tena! Au tuma MSHENGA akawapige tantalila

nakupenda sana lala hadi na mimi nitakuoa kwa staili hiyohiyo ,yaani nakupiga kitu..........wakinitajia kubwa natafakari hujakaa sawa kitu.........hadi baba mkwe akiniona awe ananuna na kubadili njia
 
Mahali 4min? uwanja unao? mchane baba mkwe anataka kutajilika kupitia wewe nini?maisha hayako hivo ,hizo M 4 ingekua investment ya madini sawa tunajua after 1 year ungevuna zaidi ya hiyo
 
Hiyo 4m... unaoa na Ukoo mzima au? washakufanya kitega uchumi
 
Aisee pole sana...huyo ba'mkwe mbona analazimisha mahari kiasi hicho afu 4m jamani kwa usawa upi wa maisha?! Hata kama ungetoa nusu bado ni nyingi sana au anataka binti yake arudi nyumbani? Huyo mkeo ndo angekuwa wa kuongea na hao mashangazi zake/ndugu wanaohusika wa upande wake hilo dau lipungue na umwambie wewe unaweza kutoa kiasi gani....

Usikute nawe msibani ulienda ukiwa umeuvalia suti..mweeeeh

Mahari imekuwa mtaji khaah
 
duuuh!!wamekugeuza mtaji
na mke badala akutetee ye anagongea msumari
kuoa sio lazima,waambie hiyo hela huna,4mil kwa kipi?
kama mtoto wao wamchukue tu,we utalea wanao mke gani
hana huruma na wewe khaaa!!
 
Mmh huyo mke wako sio....cha msingi we komalia tu hiyo 4 million hunaa!! Huyo mke atajirudi tu.. heeee wamekufanya mtajii!!??Hata mke huruma hana!!! Huyo hakupendi kwa dhati...
 
M4 ni nyingi sana duh wazazi wengine bwana sijui wakoje au mkeo amewaambia wewe uko juu sana nini. Peleka kiasi unachoweza kulipa halafu zitakazobaki waambie bado unatafuta. Kama wakikataa basi kaa na mkeo jadilianeni cha kufanya. Ukiona na yeye hana mwelekeo basi mwambie arudi kwao mpaka utakapoweza kulipa hiyo mahali uone atasemaje.
 
Kumbe ndo maana umejificha siku zote hizo unakula kamzigo.
 
Mahari mwisho 500000 hyo 4m si mtaji kabisa?

Huyo mzee ashageuza mwanae kitega uchumi.

Kaa kimya, akikutafuta mwambie huna hyo hela labda 500000. Na ukishampa tangaza ndoa kesho yake.
 
Back
Top Bottom