masai dada
JF-Expert Member
- Dec 29, 2013
- 17,581
- 20,218
Achana nae
anza kutumia jina la pili la mumeo
Futa jina lake
anza kutumia jina la pili la mumeo
Futa jina lake
kumbe unavyojiita "strong woman" ni kwamba unajikakamua kuficha uchungu ulio nao ndani? Kuwa strong kweli. Baba hajawahi kuwa sehemu ya maisha yako leo unaanzaje kumshirikisha mambo yako wakati toka mwanzo alishaonyesha hataki?
Usimlazimishe "babako" kitu asichokitaka. Umelelewa na mama sawa, lakini watoto wengi wa kiafrika wa nje au kabla ya ndoa hawalelewi na mama bali na ukoo wa mama (babu, bibi, wajomba na mama wakubwa na wadogo). Katika hao huna wa kuwashirikisha mambo yako ya ndoa mpaka iwe baba?
Hii ni changamoto ya kawaida. Muamini mama yako, halafu umsamehe babako uendelee na maisha yako, vinginevyo usishangae hata hao watoto wako wa kike waka-experience kitu kinachofanana na hicho. Hujaona kama umeanza kuvaa viatu vya mama yako?
Mamako alizaa kabla ya ndoa mapacha wa kike, akakataliwa. Wewe umezaa mapacha wa kike kabla ya ndoa na unakataliwa na babako. Sitaki kutabiri kuhusu wewe na huyo baba watoto wako. Negative energy attracts negative energy. Muachie baba yako uishi maisha bora na mapacha wako wapate "future" nzuri. Umeelewa? Forgive and move on.
Muda mwingine kuna vitu ukiona haviend unapaswa kuviacha ili mambo mengine yaendeleeKwa nini unang'ang'ania kumtafuta mtu asokutafuta???? Asokujali??????
Pambana na maisha yako....
Tupa kule
Unao wajomba si Ndio Simama nao pamoja...
Strong woman kweli???? Maneno mengine yanatufanya hata tuandike humu jf bila kupenda. Just imagine, mtu sasa unataka kuolewa, umempata mwanamune aliye tayari kukutwaa. Tangu uzaliwe, hujawahi ona sura ya mwanamume aliyeleta hata sukari home kwa mamako. Kibaya zaidi, mamako alikuambia, huyo dingi wako kishakufaga miaka, hata kaburi lilishasahaulika.
Ati unaenda kutafuta maiti, aje akajitwaliye mahari kwani mama kafariki, ukamwita akakujibu vizuri tu, siji wala usinitafute tena. BADO UNALILIA AWE BABAKO? Leo umenipa mpya kabisaaa!! Unamtakia nini mtu huyo?? Njoo kwangu, tena nina shape nzuri sana ya kuitwa baba niwe tu babako. Hakuna jasho lolote unalotoa kwangu ila jina la babangu tuu??
Pole zako, huenda huyo dingi ana nafasi kuubwa mahali flani, huenda anataka kutangaza nia kesho ndo maana hataki swaga mbofu mbofu. Tafuta maisha yako na huyu bwanako mtarajiwa, fanya mbinu mfunge pingu zenu za maisha, endelea na maisha aliyo kukuta nayo bado akakupenda.
Sahau huyo kichaa unayemwita babako. Hata ukikutana naye hapo, sahau ka uliwahi sikia ni babako. Kikitokea kuwa safi upande wako, mwenyewe atajilengesha kwako tu, ndipo umpe adhabu ya kuandika gazeti la nipashe ukurasa wa mbele historia yake na mamako.
Huyo, namhukumu, HAFAAIIII kuitwa baba. Ni hiyo spe.rm yake ilipotea na kujiunga na Ova.ry ya mamako tu kwa bahati mbaya ndo maana mkawa twins. Usijiaibishe tena kuomba ushauri kwani hakuna wa kukuambia kamlilie akukubali wakati mama hayupo.
Muda mwingine kuna vitu ukiona haviend unapaswa kuviacha ili mambo mengine yaendelee
kumshikilia baba yake kuna muumiza sana huyu dada na huku kuna mfanya asiweze kusonga mbele ama kufanya ya maana katika maisha yake
Asante mkuu... Yani napumua pumzi ndefu ndefu sana sijui kwa mini.dah nakuonea huruma manake adi mwandiko wako unaonekana umeandika ukiwa na huzuni adi kushindwa kuandika vizuri.
Acha kuwa mwoga wa maisha, acha kuogopa maisha, acha kujihisi ni mkosi ama balaa (bastard)
wewe ni wa thaman, mbele za macho ya watu ndo mana nje ya hili bandiko hakuna anayejua kwamba ulikataliwa na baba.
Songa mbele waza yako, na uendelee, mibaba kama hii ndio inayochumisha watu dhambi.............
afu siku kapigikaa anarudi ooh naomba msaada, msaada my foot.
Give yourself heart and go on, achana naye, so far hakunaga duka linauza bidhaa kwa wale wenye baba tu na wasio na baba wasiende kushop apo..........wala hakunaga magari yaliyoandikwa yaendeshwe na wenye baba tu wasokuwa nao wasiendeshe. Kama ndivyo basi maisha yako fair sana, kila kitu utaki -access ukiwa na pesa lkn si ukiwa na baba.
Mkuu Mimi dorini na pacha wangu dorisi (majina si ya kweli) tulizaliwa pacha na baba yetu akatukataa.mm ndo nataka kuolewa siku za karibuni.Sio yeye ana mapacha! Yeye ndo pacha na mwenzie na yeye ndo anataka kuolewa!
Duuuuh! Pole mkuu mbona ka Umepaniki hiv
Cha ajabu kuish8 maisha yake yote bila baba... sasa kinachompa kihoro sijui ni nini.
Baba ambaye hujamwona toka utoto
Hajui ukiumwa
Ukilala na njaa au ukishiba
Hajui unasoma au la
Ndie akuoe presha
Pyeeeee
Huyu binti anatakiwa awe busy na maisha yake......
Asante mkuu... Yani napumua pumzi ndefu ndefu sana sijui kwa mini.
Mkuu Mimi dorini na pacha wangu dorisi (majina si ya kweli) tulizaliwa pacha na baba yetu akatukataa.mm ndo nataka kuolewa siku za karibuni.
Sio yeye ana mapacha! Yeye ndo pacha na mwenzie na yeye ndo anataka kuolewa!
Duuuuh! Pole mkuu mbona ka Umepaniki hiv
Nhhh nimeamini maneni ya mama kuwa baba yenu hakuraka watito wa kike sasa mimi nimezaa wakike wawili daaah jamani nimeumia sana nachozi tu yananibubujika