Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,660
- 1,801
Juzi nilipita Uturuki nikidhania paspoti yangu ya Tanzania itaniruhusu kuingia bila visa, au kwa kupata visa uwanjani.
Itakumbukwa kuwa rais wa awamu ya nne, JK, alikubaliana na mwenziwe Ordogan kuwa raia wa nchi hizi waweze kutembea katika nchi mbili bila visa.
Waturuki wanaingia Tanzania bila visa. Ila nilipojaribu bahati yangu nikakumbana na uhakika. Afisa Uhamiaji wa Uturuki aliniambia hakuna kitu kama hicho.
Mwenzake aliyekuwa akijua suala hili vizuri akasema, kweli paspoti ya Tanzania hukubaliwa kuingia Uturuki bila visa lakini kwa sharti paspoti hiyo iwe ina visa ya moja ya nchi za Umoja wa Ulaya, au msafiri apate visa ya bure Ubalozi wa Uturuki Bongo!
Katika uwanja wa ndege wa Istanbul kuna orodha ya nchi ambazo zinaweza kupata visa uwanjani hapo, ikiwemo Tanzania. Nikaenda kwenye mashine ya visa ya elektroniki na kweli, baada ya kujaza fomu, mashine ikatoa visa.
Hata hivyo nilipofika tena kwenye Uhamiaji, afisa alikataa kata kata na kusema pamoja na kuwa nimepata visa kutoka kwenye mashine hiyo baada ya kulipa dola 50, ila sharti linabaki pale pale kuwa lazima ndani ya paspoti yangu kuwe na visa ya moja ya nchi za Muungano wa Ulaya.
Niliona wazi kuwa huu ni ujanja wa kukiuka makubaiano yaliyofikiwa. Kwa sababu sharti hii haimsaidii Mtanzania kwa vyovyote. Pengine ni kweli ukifika Ubalozini kwao hupewa visa ya bure, ila niliona wazi kuwa hilo ni kama kiini macho pale nyumbani.
Kuna Watanzania wengi wanaishi ughaibuni, hivyo mpangilio huu hauna maana sana.
Kwa wahusika wa uhamiaji: naomba mchunguze hili na kuchukua hatua za mithili kwa raia wa Uturuki na raia wa nchi nyingine wenye masharti kama hayo, na kufanya tit for tat- muamala wa mithili.
Mara nyingi tunadhani kuwa ni sisi tu tunaohitajia nchi za watu, na kwamba nchi nyingine haziihitajii Tanzania. Kutokana na mawazo hayo potofu, tunaacha nchi yetu iwe rahisi kuingia wakati raia wa Tanzania hupata usumbufu mkubwa katika nchi nyingi watumiapo paspoti za Tanzania.
Ukweli wa mambo ni kuwa raia wa nchi nyingi wana mafao makubwa Tanzania kuliko Watanzania wanavyofaidika katika nchi za nje.
Wakati umewadia wa kuondokana na akili za kitumwa na kuleta/rudisha heshima ya Tanzania kuwa ni nchi ambayo inawajali raia wake. Pindi tukifanya hivyo, na nchi nyingine zita reciprocate.
Siku zote, ukitaka kuheshimiwa kwanza jiheshimu mwenyewe. Hakuna hasara yeyote itakyopatikana kwa hili. Na hata kama iko, heshima ni muhimu sana kuliko maslahi ya kiuchumi ya muda.